Search This Blog

Thursday, June 27, 2013

MJADALA:NINI MAONI YAKO BAADA YA UONGOZI WA SIMBA KUTANGAZA KUTOMSAJILI TENA JUMA KASEJA!

Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja akiwa na kocha wa timu hiyo Kim Poulsen.

53 comments:

  1. Simba iachiwe ifanye maamuzi yake.. Kaseja alivyo iacha Simbasc akaenda Yanga haikua habari.. Ila SimbaSc kumuacha kaseja ndio habari kwasababu tu ni rafiki yenu? Waandishi ndio adui wa kwanza wa maendeleo ya soccer tanzania.. Mlimsifia kinje kumpa maisha simba kwakua mmekua pamoja huko temekr/vituka sasa mnataka kumsajili Kaseja kwa nguvu.. Acheni unafiki Dhaira atacheza badala ya Kaseja..

    ReplyDelete
    Replies
    1. unafiki unatoka wapi sasa..je una masilahi binafsi kwenye uamuzi ulochukuliwa na viongozi wa Simba? we toa maoni yako acha kushambulia watu..

      Delete
    2. Unafiki unakuja hivi.. Umewahi kusikia mwandishi anaandika kumshutumu Mchezaji kwa kuitosa timu yake? Kaseja aliitosa Simba ikiwa ina kipa dida na barthez wakiwa wageni kwenye ligi ikabid imtafute Amani Simba alie kua anaelekea kustaaf.. Hakuna alie msema kaseja zaid ya kumpongeza.. Kelvin Yondan kaja simba akitoka kusiko julikana leo kaitosa tim hakuna mwandishi alie piga kelele.. Na wengine wengi kama hao mbona hawatetewi? Abdi kassim katupiwa virago Azam ila kwakua hawana maslah nae sio rafiki yao hawajasema kitu.. Iweje kaseja wamshupalie? Akatafute maisha mbele ya safari.. Kipa mzuri sio lazima acheze simbasc

      Delete
    3. Well said Mr Salim Hassan, kwani kaseja kuachwa ni jambo la ajabu jamani au ni lazima aidakie simba tu, Kaseja ni mzuri sawa lakini simba wameamua kumuacha nayo ni sawa. Shaffih anashangaa nini sasa kuachwa kwa kaseja haoni huko ulaya wachezaji wakubwa wanaachwa na maisha yanaendelea.Simba ilikuwepo kabla ya Kaseja na itaendelea kuwepo hao ambao wanaona simba wamekosea kumuacha basi wamsajili wao kwani tatizo likuwapi.
      Awe ameachwa na viongozi ama kocha mwisho wa siku tunasimama pale pale Hakuna marefu yasiyo na mwisho.Shaffih Jipange acha kuleta mada zisizo na maana.

      Delete
  2. nadhani kuna haja ya kuwa waelewa na wavumilivu tatizo kwa kaseja sio kiwango ila la kwanza ni kupotez uaminifu ndani ya wana somba pili. i mtu wa majungu na kuwagawa wenzake kwa kuzingatia ushawishi wake mkubwa.na zaidi ya hapo alipewa nafasi kubwa ya kuamua na kwa umri hatumtarajii zaidi ya miaka miwili mbele sasa hela zote za nini alitaikiwa kabla hajatazam ihsani ya wanasimba kwake atazame ihsani yake kwetu alikwenda yanga kipindi tunamhitaji na akasema amefata hela akarudi tukampokea hiyo peke yake ihsanikawaida wengi huzingatia mwisho na amalizae ndio huwa mbaya kaseja hatufai na hatuna imani nae

    ReplyDelete
  3. Yaap..!Simba itabaki Simba tu...!sio lazima player achezee timu carrier yake yote..uongozi/kocha wameona hana nafasi katika timu so wafanye nini sasa..?Abel Dhaira yupo

    ReplyDelete
  4. Yaap..!Simba itabaki Simba tu...!sio lazima player achezee timu carrier yake yote..uongozi/kocha wameona hana nafasi katika timu so wafanye nini sasa..?Abel Dhaira yupo

    ReplyDelete
  5. Simba viongozi wameshindwa kazi sasa wanazuga kwa kutupia lawama wachezaji usajili walifanya na wanafanya tena mwaka huu timu kila siku inabadili backline yake tunasajili wa kuokoteza wala c wa viwango vya Simba viongozi hawana huwezo wamebaki majungu unafiki na umbea wa kuckiliza maneno ya mitaani na wala hakuna ubishi Manembe ndio ameshinikiza kuachwa kwa kaseja hivi kweli timu kama Simba mwenyekiti wake wa ufundi anaweza Kuwa Manembe?ni aibu sana alileta kipa anaitwa Mweta ni ndugu wa kisesa pale mwanza akitaka awe kipa namba moja wakati hana huwezo sasa hapo ndio alipoanza kushinikiza kuachwa kwa kaseja maana anajua kabisa kwenye usajili wa mtu kama kaseja hakuna ganji maana wao wamezoea kusajili wachezaji ambao wanakula ganji zao wana Simba wote wakae wakijua tunafulia tena mwakani we viongozi wanauza mchezaji toka January mpaka sasa tunakwenda July hela hakuna wakati yeye mwenyekiti alisha kula ganji yake kule muda mrefu Leo tunamuona kaseja hafai lakini tukae tukijua kabisa yule Dhaira hawezi kudumu Simba yule ni mchezaji wa malengo makubwa na Simba Magumashi matupu huwezi kutoa senior players wote kwenye timu kubwa Simba kwa ghafla kama hivi yanga walijaribu mwaka 1995 wakashindwa mwaka uliyofuata waliwapigia magoti wenyewe akina marehemu Kizota sasa sijui kama mashabiki wa Simba watakuwa tayari kwa vipigo msimu ujao wanachama wa Simba mkutano Mkuu unakuja mwezi ujao twendeni tukawapige chini viongozi wote wale kwa maendeleo ya Simba

    ReplyDelete
  6. shaffih nakuheshimu kama mchambuz mfuata upepo wa michezo,lkn ktk hili la kaseja sikuelewi kabisa.uhusiano wa kaseja na simba ni wa kimkataba.kama simba hawatak huduma ya kaseja sio issue ya kujadili,ni uamz wa simba na unapaswa kuheshimiwa,sio kitu cha ajabu.timu ziko nyingi ktk ligi ya tanzania achague moja achezee,wala kuwa capt timu ya taifa sio kigezo,2006 capt wa Angola worl cup hakuwa na timu baada ya kumaliza mktaba wake na timu moja ya uarabuni,agrey moris na erasto nyon wamecheza timu ta taifa mda mrefu huku wakiwa hawana timu ya kuchezea baada ya kusimamishwa na azam,kuchezea timu moja kwa mda mrefu sio kigezo cha kutoachwa.japo kwa upande wa simba sikubaliani na sababu za kusema kuwa kiwango kimeshuka,wangesema tu kuwa anataka hela kubwa ambayo hawana hela ya kumlipa.lakin kumuacha kaseja ni sahih ili akina abou hashim na wao waweze kuonekana na andrew ntalla.mourinho sasa hamtak david luiz lakin hakuna mjadala sasa kaseja ana nn?aende hta nje akajaribu bahat yake.unapigia kelele sana proffesionalism ktk football,so hata kumuacha staa ktk timu ili kujenga timu yenye spirit tofaut ni ueledi pia

    ReplyDelete
  7. Nadhani busara ingetumika zaidi kuliko kumwondoa kwa malumbano yasiyo na maana. Hakuna asiyejua alichofanya Kaseja Kwa Klabu ya Simba. Na itakuwa shida kubwa kwa mpira wa tanzania kuwa na wachezaji wakongwe wenye mapenzi na klabu zao kama tunavyoona wakistaafu kwenye vilabu vya majuu na hata kuitana na kucheza kwa furaha na ari na upendo kwa timu zao kama ilivyotokea wakati wa mechi ya legendary wa Man U na Real Madrid. Nani aliyetuloga watanzania kuwa na chuki zisizo na maana? Michezo cyo vita ni amani na upendo. Kama Ronaldo angeondoka kwa matusi na malimbano anayopata Kaseja sasa, kweli angekuwa akifikiria tena kurudi MAn U kwa sasa? Pevukeni kuweni wanamichezo wa kweli acheni chuki zisizo na maana. Hata kama kuna madai kuna Kaseja kapungua uwezo wake bado kungeweza kufanyika namna ya kumuenzi na kuujali mchango wake klabuni. Haya endeleeni na malumbano yasiyo na maana lkn mwisho wa ck tutakuwa tukisimulia mpira wa majuu kwa mia moja ijayo! Amkeni!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi Mwameja asingestaafu pamoja na kuwa alikuwa bado na uwezo Kaseja angejulikana lini, wacha apishe watu wengine nao wajaribu wakishindwa watatafutwa wengine kama yeye alivyopatikana

      Delete
  8. Ni kweli Mr Salimu Hassan umesema kweli Simba iachwe ifanye maamuzi yake kwani kaseja c pia aliiacha simba katika mataa akaenda jangwanii? sasa gogoro ni simba kumuacha kaseja halikuwa gogoro kaseja kuiacha simba na kwenda jangwani kwa ajili ya maslahii? na vile vile maslahi hayo hayo ndo yameifanya simba kumuacha kaseja. hatukatai ameifanyia makubwa simba lkn c bure ni mikataba na vile vile simba imemfanyia makubwa kwani nyota yake ilianza kung'aa alipokuwa msimbazi. simba ilikuwepo bila kaseja na ikaendelea kuwepo na kaseja na itazidi kuendelea bila kaseja vp watu kulalama? hivi kaseja kipindi kama hiki angeamua kuhamia Azam na kuitosa Simba watu pia wangepiga kelele kwa nini ameitema simba?









    ReplyDelete
  9. Sijawaelewa simba maana kama Kaseja bado ni kipa namba moja Tanzania hiyo ina maana uwezo wake upo juu so ni wakati wa kubadilika na kuacha siasa. Brazil kipa namba moja Julio Cesar anacheza QPR na timu imeshuka daraja lakini still kocha anaamini uwezo wake na ndo maana tunamwona anaendekea kung'ara katika timu ya taifa. Umri wa kaseja si tatizo maana kwa nafasi ya Golikipa tumeona wengi wanacheza katika umri mkubwa. Tatizo Simba Viongozi ni wanasiasa na sio watu wa mchezo wapo hapo kwa kufanikisha mipango yao binafsi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umetoa mfano mzuri wa Cesar timu yake imeshuka daraja, nae atafute timu hata kama ni ndogo akacheze kama ni mzuri kocha wa stars ataendelea kumuona tu sio lazima SImba.

      Delete
  10. mi naona we shafii una agenda yako c bure coz unavyomtete uyo kaseja utazan anakulipa..!!

    ReplyDelete
  11. Dah, nimeumia sana lakn, ingawa ukweli unabaki palepale, kuna methali ya kiswahili inasema akufukuzae hakuambii toka, naishindwa niigeuzeje i-fit kwa Kaseja kwani kwa yeye kuwaambia Simba anataka milioni 60 na wao wakawa tayari kutoa m40 bado akakataa ni dhahiri shari kwamba yeye haitaki Simba kwa sasa na alikua anachomoa kiana, iweje kwa kushuka ka rekodi kiasi hicho, ukiwa kama Nahodha kuifamya timu ishike nafasi ya 3 tena kwa maogoli mengine ya izembe kama lile la Hussein Javu Morogoro, bado udai kiasi hicho? hakuna value for money hapo, kuna habari nimezipata kwa rafiki yake wa karibu kwamba Juma hataki mpira kwa sasa anatalka ajikite kwenye biashara zake,.....huenda kuna link hapa...all in alll atabaki kuwa kipa wa kukumbukwa Simba kwa moyo wa kujituma sana licha ya kasoro kadhaa ambazo nyingi ni hear say, hata hivyoi licha ya kwamba anajiuliza ameifanyia mengi Simba akumbuke pia na Simba imemfanyia mengi..........

    ReplyDelete
  12. Tuache unafiki,ushabiki na unazi ktk hili.Anayetangaza kutomuhitaji mchezaji ni benchi la ufundi au uongozi wa timu.?Tumeshuhudia makocha wengi wakiwaacha wachezaji kwa sababu ya kuwa majeruhi sana,pia kutokuwa ktk mipango yake au kutokuwa na mchango ktk timu,.Sasa kwa hili la Juma,limeamuliwa na mwalimu Kibaden au uongozi..?Kwa ubora wa Juma hapa TZ,hakuna kocha yeyote awe wa ndani au nje ya nchi asiyetaka kufanya nae kazi,kwa kuzingatia hili ndio maana sishangai KIM kumpa unahodha wa TAIFA.Tatizo sio kuachwa kwa Juma,ameachwa kwa sababu zipi.?Mwalimu amehusishwa kutoa maoni yake.?Tuanaona duniani kote,Mfano Casilas aliposhuka kiwango alikuwa chaguo la pili,sasa km ni kiwango,kwann asiwe chaguo la pili.? Hapo sasa ndipo linapokuja suala la UELEDI haukuchukua nafasi yake,na badala yake CHUKI,UBINAFSI,UFISADI,UNAFIKI,ndivyo vinavyofanya maamuzi ya kipuuzi,kishenzi na ya kipumbavu km haya.Tunashindwa kuwa wakweeli siku zote kwa kuhofia kunyimwa hela ya konyagi,matokeo yake mtu anapata adhabu asiyostahili,.Kwa hili athari yale lazima Simba itawarudia tu,na Taifa pia lazima litaathirika tu,.Juma asikate tamaa,achukulie ni changamoto ktk kazi yake,adumu ktk nidhamu yake na ibada.Lkn pia liwe funzo kwa wachezaji wengine kuwa kufanikiwa kufikia malengo yako si lazima upitie simba au yanga km alivyofanya Ulimwengu..Mungu ibariki Tanzania..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kujua mpira si hoja pekee, apunguze kugawa timu na kula mlungula

      Delete
    2. Mi sijasikia majungu, nimesikia alitaka pesa nyingi sana. Asisahau dhaira ni Uganda one pia na analipwa hela nyingi na alisajiliwa kwa hela nyingi.

      Delete
  13. Hata hivyo uwezo wa Kaseja sasa umepungua na wapewe nafasi wengine. Udhaifu wake unaonekana wazi.Magoli alizofungwa ktk mechi ya mwisho na Yanga na pia na timu ya Ivory Coast, imethibitisha enzi za kaseja zimefika kikomo.Kila kitu kina mwisho wake.Hakuna ajabu Kaseja kutemwa.

    ReplyDelete
  14. Tatizo la watanzania kila kitu mnachukulia tatizo hili kwa wenzetu sio tatizo hii ni changamoto so kaseja have 2 face it,na huu ndio muda muafaka wa kaseja kwenda kufanya majaribio club za nje tena akiwa mchezaji huru mm naamin kwa kiwango chake anapata timu ya kuchezea tena kwa maslah mazuri kuliko aliyokuwa anayapata simba nilikuwa nafuatilia mahojiano ya njohole ktk gzt la mwanasport anasema huu ni wakati wa kumtumia kaseja anatakiwa asome ukocha wa makipa ili waweze kuvumbua vipaj vipya ktk nafasi hiyo so huu ndio muda muafaka wa kaseja kumtafuta njohole ili waweke mikakati wanalifanyaje jambo hlo all in all kaseja bado yupo vzr akasake timu nje tu kama wanavyofanya wachezaj wa magharib najus mtaj ano kuanzia kipaj mpaka pesa ila kama amezoea kukaa nchin haya ila anatakiwa kujifunza kutoka kwa ivon mapunda yupo kenya na kina golikipa mwengine yupo msumbij wote wanatafuta maslah,maslah sio mpaka simba na yanga,this is time kwa vijana waonekane ili kuwe na changamoto hebu muangalie bartez anaonekana sasa hv baada ya kuachana na simba,let him think twice waandish msimpotoshe ila muuonesha hz ni changamoto tu kila sehemu zipo

    ReplyDelete
  15. Huo ni ubabaishaji tu wa viongozi wetu! TZ 1 mnamuachaje km sio umbumbumbu ktk uendeshaji wa soka la bongo? Timu ya taifa tunaijengaje ili hali wachezaji weu hatuwapi nafasi? Huyo Dhaira hawezi kuwa na mchango mkbw kwa SIMBA km ilivyo kwa Kaseja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tz one sio lazima acheze simba au Yanga. Anaweza kusajiliwa na timu nyingine tu atakayoafikiana nayo maslahi anayoyataka
      Simba imeona tayari ina kipa wa timu ya taifa

      Delete
    2. Mimi nakushangaa unapolalamikia viongozi,KASEJA hakufukuzwa Simba isipokuwa mkataba wake uliisha, pamoja na kwamba alituuza mechi ya Mtibwa, Yanga na Kagera Dar ambapo alipokea hela ya SEIF kupitia kwa MGOSI lakini viongozi wa Simba walimvumilia amalize mkataba wake aondoke kwa amani, leo inakuwaje unawaita wababaishaji, na kama KASEJA angekuwa kipa mzuri miezi 6 kabla ya kumaliza mkataba wake tungeona vilabu vingeanza kummendea kama ilivyokuwa kwa NIYONZIMA, KAPOMBE na KIEMBA lakini ilikuwa kimya mpaka leo hii anasubiri huruma ya Simba, huo u TZ one anaupata kwa NDUMBA zake alizofuata Kigoma za kuwafunika wenzake, mbona leo hii BARTHEZ anan'gaa. na kwa hili la KASEJA pia SHAFII umejishusha tumekugundua ni mtu wa Majungu na Unatumika Simba wamepita makipa wangapi kina IDDI PAZI, MAHADHI na MAMBOSASA walifia Simba? Kaseja amekupa nini mpaka umeshupaa namna hiyo? kama ni mema hata Simba imemfanyia makubwa, angechezea Ashanti basi tuone kama angepata huo mkataba wa PEPSI

      Delete
  16. Aje yanga atakuwa kipa namba mbili akimsaidia aliyekuwa msaidiz wake barthez

    ReplyDelete
  17. Bila kaseja simba itaendelea kuwepo!

    ReplyDelete
  18. mi nadhan simba wamefanya mistake kumuacha kaseja,cdhan kama kiwango cha kaseja kimeshuka kihivyo mpaka asi deserve kuwa mchezaji wa simba.

    ReplyDelete
  19. nyie wote mikia tu mnaogoopa kipa wenu akiondoka mtabaki na pazia golini, jengeni kujiamini ndio maana kila mechi anadaka yeye hata mechi zisizo na tija ni yeye tu hadi barthez akasepa yanga, huyo kaseja ashakua babu acheni damu changa nazo zije zitoe mchango kumbukeni kaseja kapokea kijiti kwa mwameja kama sijakosea, wote akina mhagama kelvin walisota benchi kwa ajili yake, kipa anamiaka 13 ndani ya timu akitemwa mnalalamika, mbona wenzake alioanza nao soka wakina mbuna walisha sahaulika ingawa kunatimu wanazitumikia bado??????? acheni kucrame kuwa golini bila juma k juma hakuna kitu thats very wrong..

    ReplyDelete
  20. It is not necessary for kaseja to be simba sc player for all of his goalkeeping carier. Since he is the best in the country,he has to play wherever football is. Why shaffih blames?,is that all your thoughts are perfect?or, Is kaseja born to play for simba sc? Kaseja stil have a chance to play in other teams. So,LET KASEJA GO.

    ReplyDelete
  21. labda ingekua busara kama samba ingeachwa ifanye maamuzi yake bila ya kuingiliwa na mtu mwingine coz hata kaseja alipoamua kwenda yanga aliachwa afanye maamuzi yake,na kumbukumbu zinaonyesha hata aliyekua kocha wake wa timu ya ilala kipindi kile(jamhuri kihwelo) aliwahi kusema kasja aachwe na maamuzi yake na akamshauri akachkue hizo pesa nyingi kwa kipindi kile toka kwa manji....tuiache samba ifanye maamuzi yake,mbona wameachwa wakongwe wengi tu,wapi nyoso,na boban???kwa klijua hilo wameendelea na shughuli zao za kila siku huko kwingineko....maaasalam.....

    ReplyDelete
  22. Watu wengi walijuwa kwamba kuachwa kwa kaseja kwako itakuwa majanga kwani unampenda sanakaseja samahani kwa ilo ila kumbuka kila kitu uwa kinamwisho wake kakakaseja bado ni mzuli atapata timu nyingine namuombea kwa mungu akumbuke mpila sio simba na yanga wapo azam na timu nyingine nyingi

    ReplyDelete
  23. Hivi kaseja kaachwa au mkataba umeisha, alijua wakati anasaini kuwa ni muda gani, sasa mwajiri hataki kuongeza kwa sababu zake sasa liko wapi? Simba Inajenga Timu Na kujenga Timu Kuna Factor nyingi Na Sio uwezo Mchexaji Na Historia Yake. Baada Ya Kutangazwa Kuachwa Kaseja Nilifanya research Fupi Kuwauliza Baadhi Ya Wachezaji Waliocheza Nae Simba Na Taifa Stars kila Mtu Kasema Kaseja Ana Roho Mbaya Sana Hataki mchezaji Hata Mmoja Awd Juu Kidogo Sasa Nafikiri Hawa Jamaa Wanataka Kujenga Kikosi Kimoja Bila Kumtegemea Mtu Mmoja. j
    Jamani mi Yanga Nawauliza Jamaa Zangu Hawa Wanaenda Kufanya Nini Kila tunisia dili La Kuuza Mchezaji Lilikwisha Na Mchezaji Anacheza, Au Ndo Wanataka Kufuata Hela Kwenye Mfuko Wa rambo Kama Taifa? Hapo Mnapigwa Changa La Macho Tu

    ReplyDelete
  24. KUONDOKA KWA KASEJA KULISHAJULIKANA MWANZO TU WAKATI VIONGOZI WA SIMBA WANAJADILIANA NA MZEE KIBADEN. KIBADEN ALIPOHAKIKISHIWA ULAJI AKAWASHAURI SIMBA WAMSAJILI NTALLA. KWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU UNAELEWA TU KWAMBA KOCHA ABDALAH KIBADEN HAKUPENDA KUJA KUFANYAKAZI NA KASEJA. KIBADEN NI SIMBA DAMU NA KAMA KUNA MAJUNGU AMA HABARI ZA SIRISIRI PIA ZITAKUWA ZILIMFIKIA KOCHA KWAKUWA YEYE NI MWANACHAMA WA SIMBA NA HIZI TAARIFA ZA CHINI NAE ANAZIPATA KAMA MWANANCHAMA.

    SASA ILI KUEPUKA YOTE HAYA KOCHA AKAONA BORA AJENGE TIMU YAKE AMBAYO YEYE ATAWEZA KUIONGOZA VEMA NA MWISHO IKAFANYA VIZURI PASIPO KUSHAWISHIA (INFLUENCE) NA WATU WENGINE. HIVYO ANAJUA FIKA SIMBA YUPO DHAIRA KIPA MZURI SANA, ANAJUA KASEJA KAMALIZA MUDA WAKE NA ANGEWEZA KUWAAMBIA VIONGOZI WAMSAJILI KASEJA KABLA HATA YA NTALLA, LAKINI KWAKUWA AMEFANYAKAZI NA NTALLA HIVYO ANAJUA UWEZO WAKE NA NIDHAMU YAKE NDIO MAANA AKAMPA NAFASI YA KWANZA MBELE YA KASEJA.

    HIVI KIUKWELI KASEJA HATA ANGESEMA ANAJISAJILI SIMBA BURE UNAZANI ANGESAJILIWA? JIBU NI HAPANA!!! KAMA KOCHA AMEONYESHA ANAMKUBALI DHAIRA NA NTALLA SASA KASEJA ATACHEZA WAPI?!!

    TUACHE USHABIKI NA MANENO MENGINE, UKWELI NI KWAMBA SIMBA MSIMU ULIOPITA HAWAKUWA NA WAKATI MZURI NA KASEJA ILIFIKIA HATA KASEJA BAADA YA KUONA HALI SIO NZURI AKAOMBA APUMZIKE KWENYE BAADHI YA MECHI!!!

    SASA LEO HII SIMBA KUKATAA KUONGEZA MKATABA WA KASEJA SI AJABU MAANA HATA INGEKUWA KASEJA YUKO KWENYE PICK KUBWA SANA LEO HII AKAAMBIWA ABAKI SIMBA AU AENDE TIMU NYINGINE YENYE MALIPO MAZURI ASINGEBAKI SIMBA. SABABU KUBWA NI YALE MATUKIO YA MSIMU ULIOPITA.

    MIMI NAMSIHI KASEJA ATAFUTE TIMU HATA NJE YA NCHI KAMA INAWEZEKANA YEYE NI KIPA MZURI UMRI BADO UNAMRUHUSU. MBONA IVO MAPUNDA ANACHEZA MPIRA MPAKA LEO. IVO MAPUNDA NA KASEJA NANI ANA UMRI MKUBWA? NANI ANAKIWANGO KIZURI? JIBU NI KWAMBA JUMA KASEJA ANA UMRI MDOGO KULIKO IVO MAPUNDA, JUMA KASEJA ANA UWEZO MZURI KULIKO IVO MAPUNDA.

    KASEJA NI MUELEWA SEMA HII IJADALA YETU NDIO ITAMFADHAISHA (FRASTUATE). ILA KAMA SISI TUKILIONA HILO TUKIO NI CHANYA(POSITIVE)NA YEYE PIA ATAKUWA CHANYA ILI AWEZE KUENDELEA MBELE YA SAFARI.

    MSIMU UJAO NDIO UTAONYESHA UMUHIMU AMA MAPUNGUFU YA KASEJA KWA SIMBA. VINGINEVO TUSIJADILI TENA KUHUSU KASEJA KUACHWA NA SIMBA. KWANI AKIRUDISHWA NA WAKATI SIMBA WENYEWE HAWANA UPENDO KWAKE ITAKUWA KAZI BURE. MAJI YAMEMWAGIKA KWENYE MCHANGA HAUWEZI KUYAZOA TENA.

    TUFUNGUE UKURASA MPYA MAISHA BILA KASEJA NA KASEJA BILA SIMBA. LETS OPEN ANOTHER CHAPTER FOR KASEJA'S FUTURE AS APROFESSIONAL GOALKEEPER.

    MUNGU AKUBARIKI KASEJA MUNGU AIBARIKI SIMBA MUNGU AIBARIKI AZAM CAF, MUNGU AIBARIKI YANGA KLABU BINGWA MUNGU IBARIKA TAIFA STARS CHAN.

    ReplyDelete
  25. naomba niwakumbushe kidogo nyuma simba ni simba na kaseja sio simba kaseja anabaki kaseja na simba ni simba sioni kioja wala ajabu yoyote kaseja kuachwa na simba haitayumba kwa kumkosa kaseja.mwaka 1986simba hiii yetu ilipotez wachezaji wote mashuhuri na tulicheza ligi bala matatizo waliondoka idi pazi akaenda sudan marehemu kiwelo musa athuman maulidi big man .tobias nkoma.lila shomari zamoyoni mogela.hasmisi gaga.mtemi tanadhani twalib hilali zuber magoha mohamed chopa je hii si timu nzima iloondoka?tulicheza ligi ubingwa tukaukosa mahakamani kwa rufaa ya costal union kuhusu mchezaji francis.mwikalo na yanga tuliwa funga aakiwa kamili.sasa naomba tuwaache vongozi aafanye walivyopanga ili kama mambo yatakua tafauti tuwe na uwezo aa kuwahoji kila kitu.kwa upande wa kaseja asilaumu mtu ila alaumu nafsi na mwelekeo wake tulimpenda na kumuweka juu ya vichwa vyetu na tumemvumilia sana nae kwa hili atuvumilie tulimuamini akapoteza uaminifu kosa lake mwenyewe asilaumu ila nafsi yake

    ReplyDelete
  26. Kaseja acha aondoke kwani timu ni simba tu au shaffih umelazimishwa kuipenda simba maana unakuwa unaanzisha mijadara ya kijinga, nafikiri ukiwa km mwandishi uchwara na mchambuzi feki wa habari za michezo ungewaacha simba wakaamua mambo yao wenyewe na si kukaa unawasemea. kocha Abdallah King Kibadeni mwenyewe alisema kwasasa hamhitaji tena kaseja na akaongeza kusema kuwa kwasasa kaseja hana mvuto tena ndani ya club kwa ushauri wake akamwomba akaangalie maisha kwingine lakini wewe kwa ushamba wako na upeo wako mdogo wa akili umeona ni kama issue kubwa sana ya kukaa unaijadili. waache watu wenye mapenzi mema na simba na wenye kuipenda simba waendelee na simba yao chagua timu ushabikie mbona zipo nyingi tu na si simba peke yake. Chukua time wewe shaffih

    ReplyDelete
  27. David Beckham,aliachwa na Manchester,Drogba ameachwa na Chelsea na wote wanamchango mkubwa kwa hizo timu lkn mabadiliko yalikuwa lazima. Maximo aliwaacha Kaseja,Amir Maftah , na boban alieleza wallichokosa? Mnashangaa simba kumuacha Kaseja!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inaonekana hujui hata unaloandika, hawa wote hakuachwa wao ndo walitaka kuondoka. Kama hujui kitu funga bakuri lako, ufiche ujinga wako

      Delete
  28. Hakuna lolote bwana Simba hawajengi timu wanabomoa timu wanaokoteza wachezaji ambao wameachwa na timu zao huko wanasajili wachezaji wa bei poa alafu wanakata ganji zao hakuna viongozi njaaa na majungu uswahili umbea huyo Ntala mwenyewe hakuwa namba moja kagera sema kibadeni anajulikana tabia yake ukikaa vibaya unaumia kweli kwa yule Mzee na bado atamleta na julie mrope muda c mrefu Msomali kala ganji la okwi anajifanya kukaa kimyaa sasa wenzake nao muda wao ndio huu wa kula ganji na kusajili magarasa pale kinesi sasa ndio nimeamini kweli Rage Yanga +Manembe na wenzake hawa viongozi ndio walijiibia mapato ya mechi pale sinza alafu wakadai majambazi kumbe pamba alipiga dili mashindano ya kimataifa Simba mpaka 2020 viongozi wote wale hawafai ni wa kupiga chini July

    ReplyDelete
  29. Ndo yale yale. Kuku anakunya ila bata anaharisha

    ReplyDelete
  30. Maoni yangu ni hivi bwana shaffih, kwanza kabisa hii sio sahihi kwa timu ya Tanzania kumuacha golikipa namba moja kwenye timu ya taifa, nadhani wamefanya kumkomoa na kikubwa ni ushawishi wa kisiasa. kila mtu anajua awezo wa kaseja na mchango wake katika timu ya simba, inashangaza sana na jinsi wanavyomuacha kizarau kiasi hiki wakati hajafanya baya la kufanya wasahau Mazuri yake. Pili namtakia kilala kheri katika fani yake bado yuko vizuri hizi habari zisimvunje moyo acheki timu yoyote ile ali wajicheke baadae kwa maamuzi yao. Namjua kaseja pamoja na maslahi lakini alikua na damu na simba, hivyo tatizo kubwa la soka yetu ni uongozi thabiti na maisha ya ubabaishaji ndo maana hawadumu kwenye nyazifa zao, sasa wanataka hata wachezaji waenekane kama wao. Kuhusu mashabiki kumkataa hiyo sio issue, walimkataa Rage still bado yupo sasa inakuaje kwa kaseja?Mwisho kabisa Wanaijenga simba ambayo itakuwa na wachezaji wanaoangalia maslahi tu bila mapenzi sasa hii ni hatari sana. Leo wanamuona msaliti na mtaka pesa wamesahau kuna wachezaji pale wapo kimapenzi kama Boban, Kaseja na wengine ila sometime wanachoka na viongozi na mashabiki wengi hawajaenda shule hivyo ndomaana wanatoa hadi matusi kwenye mjadala huu wakati inabidi tuonyeshe mawazo yetu, wengine wanafananisha nakina Beckam, Ronaldo na manchester united sasa hii wapi na wapi?mtu timamu huwezi fananisha simba na manchester kwa mtazamo na kwakila kitu. ndo hayo tu shaffih

    ReplyDelete
    Replies
    1. mpira co maneno ya mashabiki; timu haiwezi kuongozwa na mashabiki wote, Kaseja uongozi umemwona haumuhitaji, kwa hiyo amepewa uhuru wa kwenda popote, sasa cielewi heshima gani watanzania mnataka apewe .hebu hacheni kuckiliza maneno ya fitina ya waandishi wa habari km hawa. Kaseja kaisha ukweli km huu haupingiki; suala la yeye kuwa ktk timu ya taifa haimaanishi kuwa ni bora, kaseja ni bora kwa wajinga,tanzania hii ya leo haina makipa wazuri ndo maana anaonekana ni bora. Mwameja kaifanyia simba mambo makubwa zaidi ya kaseja ila kaiacha simba

      Delete
    2. Moja, unataka kuniambia kwa mazingira yoyote yake timu ya Tanzania haitakiwi kumuacha mchezaji kwa kiwa tu ni wa timu ya taifa? Hapa umachemka sana kwa sababu bado zipo timu za ndani na za nje zinazoweza kumsajili. Huwezi kuilazimisha simba kusajili mchezaji ambaye mkataba wake umeisha na wameshindwa kuafikiana tena.
      Pili,suala la kuachwa kaseja sio kitu cha ajabu, unaongea kama vile amefukuzwa au ameonewa. Mkataba wake umeisha na yeye na simba wameshindwa kuafikiana, ameonewa nini sasa.
      Tatu simba ina wachezaji wengi tu toka timu Yao ya vijana ambao wataendelea kuwa na mapenzi na simba

      Delete
  31. Kadiri umri unapoongezeka makipa ndio huwa mahiri zaidi. Kwa suala la Kaseja nadhani ni zaidi yanayosemwa kuwa mara umri wake mkubwa, mara kiwango chake kimeshuka, mara anataka dau kubwa zote hizo ni blah blah tu. Kuna ajenda ya siri nyuma ya kuachwa Kaseja ambayo kwa bongo hatuwezi kuambiwa na viongozi ila ingekuwa Ulaya tungejulishwa.

    ReplyDelete
  32. Kumbuka simba imekuwa na bahti na makipa wazuri.hilo halina mjadala.umefika kaseja aondoke simba ili kupisha wengine.si kwamba kiwango chake kibovu ila ushawishi wake ndani ya klabu umekwisha.wapo wachezaji aliondoka simba kwa ajili yake.simba itaendelea kuwa simba na kaseja ataendelea kuwa kaseja. Makipa waliopo ni wazuri sana tu na wana umri mzuri tu.ushauri kaseja nenda nje ya nchi ukacheze soka.

    ReplyDelete
  33. Tunamshukuru sana Kaseja, ameshindwa kufikia muafaka na mwajir wake.. OFF HE GOES.. na km mshabiki wa Simba sijutii..

    ReplyDelete
  34. LAITI KAMA KELELE HIZI MNGEPIGA WAKATI JUMA KASEJA ALIVYOACHWA NA MAXIMO KWENYE NATIONAL TEAM NINGEWAONA WA MAANA SANA. TATIZO LENU UNAFKII UMEWAJAA

    ReplyDelete
  35. Wabongo kila kitu SIASA,Hongera UONGOZI kwa uhamuzi,hacha wengine nao watoke.Nyie si mlikuwa mnaongelea MAN U Mchezaji akizidi kichwa FEGI ana UZA.nikama vile simba walivyofanya

    ReplyDelete
  36. Mimi naomba niendeleee na mjadala wa kaseja kwa ufupi ni kuwa kaseja hatufai katika simba kwa kuwa hatuna imani nae tena kutokana na yeye mwenyewe kuvunja uaminifu wake.ametuhujumu mara nyingi kwa aina na namna mbalimbali kwa sasa basi wenye kuona kama wanamhitaji wamsaidie kutafuta timu nyingine si lazima simba yamehsa mwagika basi yamepita.nawaomba wana simba tuachane na mjadala wa kaseja tupange upya mipango yetu tuendelee kuborehsa timu yetu.wanao mtetea kaseja wote hao yanga aatupu wanaona duka lao linafungwa hawana pa kununuwa ndio shida inayowaumiza hawana lolote na simba sio timu ya kifalme kuwa kaseja tuu mpka afe hapana aodoke awapishe wenzake tuna makipa wazuri sana hatumtaki asiwapige misumari kwa babu yake wa mafia na aende tukuze vipaji kwa faida ya simba na taifa letu

    ReplyDelete
  37. Simba wameharakisha kumwacha Kaseja ,bado ni golikipa mzuri na ni hazina kwa simba na taifa kwa jumla.
    Bora simba wangemtumia ili hapo baadaye aje kuwa kocha wa makipa hapo simba.

    ReplyDelete
  38. Hivi Juma Kaseja alikuwa ni Mungu mtu katika Simba? Mbona tunakuza sana habari yake! Nilishangaa sana jana Clouds Fm wamepoteza kama dakika 20+ kumjadili Kaseja,mpaka tukaambiwa tupige simu kuongelea suala la Kaseja!

    Sikuwahi kusikia Simu zinapigwa kujadili kuachwa kwa Uhuru Selemani,Mohamed Banka,Juma Nyoso,Haruna Moshi Boban,Lino Masombo,Gervais Kago na wengine wengi. Jamani tubadilike sio kila kitu mpaka kipewe popularity kiasi cha kuwekana roho juu.

    Mimi ni Mshabiki na mnazi wa Simba,chama langu hilo. Lakini kwa hili sioni tatizo kubwa kihivo. Na wala Simba haijaanzia kwa Kaseja kuacha wachezaji! Nilisikia baadh ya watu wanasema eti Ooh Kaseja ameisaidia sana simba,angepewa heshima kama ya Giggs! Kha! Ina maana alikuja Simba asiisaidie? Au alikuwa anaisaidia bure? Juma Kaseja alikuwa analipwa Mshahara,Posho na marupu rupu mengine. Mambo ya kulipana fadhila kwenye kazi ndo yametufikisha hapa tulipo kama nchi.

    Na siyo kwamba aliambiwa hatukutaki,ila ni kwamba aliambiwa aamue mwenyewe anatakaje! Yeye akataka eti milioni 40 ndo asaini,basi na Uongozi ukasema kama ni hvo basi atafute timu,Simba haina uwezo wa kumpa hizo hela kwa kiwango chake. Hivyo hajachwa hivi hivi,ila wameshindwana maslahi,ikabidi kila mtu achukue 50 zake.

    Simba ilikuwepo kabla ya Kaseja,ikawepo na Kaseja,na itaendelea kuwepo bila Kaseja. Hawa Andrew Ntala na Abel Dhaira ni magoli kipa wazuri sana tu! Tumeacha Tanzania One,tumechukua Uganda One,na katika Viwango vya Fifa Uganda ipo juu sana zaidi ya Tanzania. Sasa tatizo liko wapi!?

    Kama kaseja kaisaidia sana Simba,basi na Simba imemsaidia sana. Hukuwepo bure pale. Na kama kumtema golikipa namba moja wa taifa stars ni ishu,basi tunaye namba moja mwingine wa The Cranes 'Ugand'
    Tuache porojo nyiingi za kulaumu,tuangalie na upande wa pili wa shilingi. Kwanza Simba ina Operesheni ondoa wakongwe,tengeneza timu kwa damu changa! Nadhani hata hilo limemkuta kaseja.

    Tunamshukuru kwa kipindi chote alichokuwa Unyamani,takribani miaka 9+ hivi,mungu ambariki huko aendako! Na aendelee kuwaombea Simba ifanye vizuri msimu ujao na ijayo japo hatokuwa nayo,huo ndo uanamichezo.
    MWISHO.

    ReplyDelete
  39. Watu mnachanganya mambo! issue c kuachwa kwa Kaseja ila issue anaachwaje? Na porojo zimekuwa nyingi ndiyo maana hata sababu za kuachwa hazieleweki kila mtu anasema lake mara kiwango mara bei nani kawaambia?. Na kuhusu issue ya kuongelea timu za juu ni sahihi kwani ndiyo kioo chetu! kuna mabaya tucyopswa kuyaiga lkn kwa hbr ya soka wenzetu wako mbali na c kosa kuwaiga kwa mazuri! Na kilichoelezwa ni namna ambavyo wachezaji wanaachana na timu zao bila majungu ya kiswahili kama haya ya kwetu. Kuhusu kaseja kuhamia yanga c issue kuna wachezaji wengi tu waliowahi kuchezea timu zote mbili kwa mafanikio na bado wanathaminiwa hadi leo na wapo wengi tu c lazima tuwataje kama huwajui basi wadau watakusaidia. Hata Kiemba tunayetamba naye c katoka yanga? kwa nini tusingemkataa kuwa huyu kawahi kucheza YAnga? Kuchezea mojawapo ya timu hizi kwa mchezaji yeyote ni issue ya kawaida tu na mtu asihukumiwe kwa kitendo hicho! Kaseja aachane na simba kwa amani na utulivu na siyo kwa malimbano ndicho nachosisitiza!Na mnapomtuhumu kwa kufungisha magoli ya kizembe c sawa! mbona hamuoneshi kaokoa magoli mangapi?. Muhimu hapa ni kukubali kuachana na Kaseja katika mazingira ambayo kila mmoja atabaki na heshima yake na cyo kumzodoa mtu kwa maneno yanayoonesha kutomjali au kumdharau mtu. Hicho ndo cha amani. Na kwako Kaseja wewe ni mchezaji mkubwa na suala la kuachwa kwa sababu yoyote ni kitu cha kawaida kwa mchezaji yeyote. kaa chini tulia tafakari tafuta timu endelea na maisha bila sababu ya kurusha maneno yoyote mabaya. Kila la kheri kwa Simba kwa uamuzi wenu na kila la kheri Tanzania one K.Juma. Maisha yataendelea tu bila Simba na Simba itakuwepo tu bila Kaseja hkn sababu ya kutukanana kwa uamuzi huo. Lkn kwa tabia hii narudia itatuchukua miaka 100 na zaidi kuwafikia wenzetu maana nachokiona ni chuki zisizo na maana kwa viongozi na kumbe ht mashabiki hawana tumekumbwa na mkumbo huo! Tuache jazba tutoe nafasi kwa Simba na Kaseja kufanya mambo yao bila kushushiana heshima! bye bye wadau!

    ReplyDelete
  40. tatizo la waandishi wa habari wa nchi ni makanjanja, uwezo wao mdogo. wanaandika vitu kishabiki sana!!!. mpira una nyakati zake ndo maana leo mwameja na akina mogela hawapo simba. rud va nestory hayuko man u. huu ndo mpira. kuna mwaka kaseja alienda yanga kwa kina dauda shaffii ile ilikua deal. alienda kutafuta maisha. ila leo imekua nongwa? ingekua anatakiwa yanga akina dauda wangesema hiyo ni deal. wapuuuzi sana hawa. wakati kila mtanzania alipokua anamlalamikia maximo kwa kumuengua kaseja kwa sababu tu alikua simba waandishi walimpa sapoti maximo bila kuangalia mashabiki wanataka nini. leo wapuuzi hawa hawa kwa kuwa simba imemtema wanataka kuvuruga amani klabuni. kila mwandishi anaandika makala kuonesha jinsi simba walivyokosea. Simba imemtendea haki kaseja tena kuliko mchezaji yeyote. kwa cv ya kaseja ni kipa namba moja wa taifa, ni captain, ana uzoefu wa kutosha. kutemwa maana yake simba wamempa nafasi ya kutengeneza hela ndefu. kila timu duniani inamtaka kipa bora. arsenal. madrid nk. aende huko.

    ReplyDelete
  41. Si muda wa kumjadili JK kwa kuwa behind the scene perfomance inaweza kuwepo ila maadili na uzalendo kwa Klabu ukawa hakuna.Asingetoa masharti magumu kwa Klabu anayoipenda na anayoihitaji kuendelea.

    ReplyDelete