Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013
|
Timu
ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars
mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach
5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri
wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi
Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.
Mabingwa
hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo
walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa
katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho
wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35),
Rashid Ngone (dk 38 na 71) na Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja
walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati
iliyopigwa na Steven Munyu.
Jijini Mbeya, timu ya Mbasco ilitoshana
nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya kutoka sare ya 3-3
katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising Stars. Mbasco walipata
magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na 50) na Joel Kasimila
dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha Magereza Mbeya.
Kwa
upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga
(dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).
Mjini Morogoro;
timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa
Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul
Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.
Katika
mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi
mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu
iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu
hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89
Mkoa
wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars
ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza
vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa
Nyamagana jana (leo).
Programu
hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la
kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana
wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment