Kwa mujibu wa mwakilishi wa Primetime Promotion Shaffih Dauda ni kwamba sasa mradi huo umefikia katika hatua nzuri ya ujenzi wa viwanja vitakavyotumika katika michuano ya mchezo huo.
"Kwa sasa tumeanza kazi ya kutengeneza viwanja pembezoni mwa ufukwe wa bahari hindi katika eneo la Mikocheni ulipo mgahawa wa Escape 1. Tunashukuru ushirikiano mzuri tunaopata kutoka kwa TFF chini ya mkurugenzi wa ufundi Sunday Kayuni. Kama maandalizi na mipango yote ikienda kama ilivyopangwa tunategemea michuano hii itaanza mwishoni mwa mwaka huu."
Utengenezaji wa viwanja ukiendelea Mikocheni pembezoni mwa bahari ya Hindi. |
No comments:
Post a Comment