Kuondoka kwa wachezaji wengi kwenye ligi kuu ya Spain ni kitu kizuri kwa timu yao ya taifa lakini sio jambo jema kwa ligi yao ya nyumbani, kwa mujibu wa beki wa kimataifa wa Barcelona na Spain Gerard Pique.
Jesus Navas amekuwa mchezaji mwingine wa timu ya taifa ya Spain kuhamia nje ya nchi hiyo alipoondoka Sevilla na kuungana na mwenzie David Silva ndani ya Manchester City.
Wachezaji tisa wa kikosi cha sasa cha Spain kilichopo kwenye michuano ya Mabara huko Brazil sasa wanacheza nje ya Spain - Laliga.
Vigogo Real Madrid na Barcelona, klabu zinazoingiza mapato makubwa kabisa duniani wana uwezo kuwa na wachezaji wazuri wawatakao na matokeo yake ndio wanaotawala La Liga. Wana wachezaji 13 kwenye kikosi cha timu ya taifa.
Ingawa, vilabu ambavyo vina matatizo ya kifedha kama Atletico Madrid, Valencia na Sevilla vimekuwa vikilazimika kuuza wachezaji wao muhimu kutokana na matatizo ya kifedha.
No comments:
Post a Comment