Kiingilio
cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) itakayochezwa Jumapili
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
kijani.
Viti
vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000
viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni
sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897
ni sh. 10,000.
Viingilio
vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni
sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A
yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
Tiketi
kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza
kuuzwa siku mbili kabla ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo
vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa
wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Katika
vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia
yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Tunapenda kuwakumbusha
watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo
yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya
kushuhudia mechi hiyo.
Utaratibu
katika mechi hiyo utakuwa kama ilivyokuwa katika mchezo wa Simba na
Yanga, ambapo magari hayataruhusiwa kuingia uwanjani isipokuwa kwa yale
yatakayokuwa na sticker maalumu kutoka TFF.
nimeamin hatuko siriasi na kufusu kombe la dunia vingilio vikubwa sana kwa mechi kama ii za kufuzu kombe la dunia
ReplyDeleteWakati wao huu wa kupata pexa akina tenga...cyo kuangalia hali halis ya wanamichezo.!
ReplyDeletepesa mbele...ushindi baadae, wanataka kulipa madeni na nakumalizia muda wao kwa neema
ReplyDeleteIla mbona wa2 wa bagamoyo road wametengwa sn,kuanzia Mwenge,tegeta hadi Bunju hakuna k2o ht ki1 cha kuuza tket,yawezekana market cyo kubwa bt sambazen kulingana na makadirio yenu,Kila mech wa2 wa mitaa ya huku wanapata tabu na pengne kukosa tket.(Mbez bch,Africana,Kunduchi,Tegeta,Boko,Ununio,Wazo,Bunju n.k)at least ki2o kiwepo tegeta kubalance distance ya kufuata tket.John Mwakalebela
ReplyDeletekhsu hizo bei naona zimekuwa maalum hazibadiliki
ReplyDeleteHawa TFF wananichefua tu kwanini huku wilaya ya kinondoni imetengwa sana hapo ukitazama vituo vya mauzo kilichopo wilaya ya kinondoni ni kimoja tu kama sio viuwili BMM NA UBUNGO. na kama kinachoa ngaliwa ni mkusanyiko wa watu kunasababu gani ya kutokuwepo na kituo Mwenge. na Tegeta ??
ReplyDeleteShaffih na wewe hebu sema katika hili uenda ukaeleweka.