Search This Blog

Friday, June 14, 2013

FAHAMU A - Z KUHUSU MICHUANO YA KOMBE LA MABARA INAYOANZA WIKIENDI BRAZIL -

Muda unazidi kusogea kuelekea michuano mikubwa kabisa ya soka, lakini kabla ya kushuhudia World Cup 2014, kwa sasa hivi tunaanza kuonja utamu wa michuano ya kombe la mabara inayowakutanisha mabingwa wa mabara yenye wanachama wa FIFA.

Kutokea June 15-30, timu nane zitagombania utawala wa ubingwa wa mabara nchini Brazil, kuelekea kwenye michuano hiyo inayoanza wikiendi hii  tujaribu kuangalia takwimu/mambo kuanzia A-Z kuhusu michuano hii.

A - Adriano. Mnamo mwaka 2005 akiwa na miaka 23 alikuwa ni mmoja ya washambuliaji hatari katika ulimwengu wa soka. Mabao yake matano kwenye kombe la mabara mwaka huo yaliyoifanya Brazil kubeba ubingwa na Adriano akatwaa kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora na mchezaji bora wa mashindano.

B - Brazil. Michuano ya 2013 itachezwa nchini Brazil na Selecao wataenda kutafuta ubingwa wao wa nne wa mabara baada ya kushinda michuano miwili iliyopita mwaka 2005 na 2009 pia walishinda mwaka 1997.

C - Cafusa. Mpira rasmi utakaotumika kwenye michuano hiyo umetengenezwa na Addidas na unaitwa Cafusa. Jina hilo linatokana na maneno matatu (carnival, football and samba).

D - Denilson. Wakati fulani huko nyuma akiwa mwanasoka ghali zaidi duniani, Once the most expensive player in world football, mbrazili huyo alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya mwaka 1997. 

E - Eight.
Michuano hii inahusisha washindi wa mabara sita ya yenye wanachama wa FIFA - UEFA, CONMEBOL, CONCACAF, CAF, AFC na OFC, pia nchi mwenyeji na washindi wa kombe la dunia.  


F - final. Mashabiki wapatao 78,000 waliokaa, wataangalia mchezo wa fainali utakaopigwa kwenye uliofanyiwa matengenezo wa Maracana.

G - Golden Ball, Golden Shoe na Golden Gloves. Hizo ni tuzo tatu zinazotolewa kwa mchezaji bora wa mashindano, mfungaji na kipa bora.

H - hat-tricks. Vladimir Smicer, Ronaldo, Romario, Cuauhtemoc Blanco, Marzouk Al-Otaibi, Ronaldinho, Luciano Figueroa na Fernando Torres ndio wachezaji nane pekee waliowahi kufunga hat trick katika michuano hii.

I - Italy.  Azzurri wana nafasi ya kuwa timu ya tatu baada ya Argentina na Ufaransa kushinda makombe yote matatu makubwa yaliyo nchini ya FIFA, wameshashinda ubingwa dunia na Olympic. Uruguay na Spain pia wanaweza kuweka rekodi hiyo endapo watabeba ubingwa huo.

J - Japan. The Samurai Blue wanacheza michuano hii kwa mara ya 5 wakifuzu kama mabingwa wa bara la ASIA. Mwaka 2001 walishika nafasi ya pili.

K - King Fahd Cup. Saudi Arabia mwanzoni waliandaa na kushiriki michuano hii wakati hiyo waliipa jina la Kingh Fahd Cup mwaka 1992 & 1995 na ilishirikisha baadhi tu ya mabingwa wa mabara na baadae ikabadilishwa jina na kuitwa kombe la mabara.

L - Luis Fabiano. Mshambuliaji wa Sao Paulo alikuwa ndio mfungaji bora katika michuano ya 2009 na mmoja katik ya wabrazili 5 wanaounda kwa kufunga mabao mengi katika historia ya michuano hiyo, wengine Alex, Romario, Ronaldinho na Adriano.

M - Majaabu ya wamexico. Maarufu kwa jina la ‘Cuauhtemina’ auna staili yake ya kuruka na mpira katikati ya mabeki wawili - Blanco yupo sawa na Ronaldinho kwa kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja wa michuano hii. Alifunga mara tisa na kuiwezsha Mexico kubeba ubingwa huu mwaka 1999.

N - Nielsen. Richard Moller Nielsen aliiongoza Denmark kubeba ubingwa wao wa kwanza wa mabingwa mnamo mwaka 1995. Waliwafunga Argentina 2-0 kwenye fainali.

O - OFC. Ubingwa wa mwaka 2012 wa mataifa ya OFC ulibebwa na Tahiti, hivyo kumaanisha kisiwa hicho kidogo kinakuwa taifa kuiwakilisha Oceania kwenye kombe la mabara.

P - Proffessional. Ni mchezaji mmoja tu wa kikosi cha Tahiti, mshambuliaji wa Panathanaikos  Marama Vahirua, ndio anacheza soka la proffessional nje ya nchi yake. Wachezaji wote waliobakia wanacheza ligi ya nyumbani wakicheza ligi daraja la kwanza.

Q - qualified. Brazil, Japan, Mexico na Italy watapambana katika kundi A ili kupata nafasi katika kugombania nafasi moja ya kucheza nusu fainali, wakati  Spain, Uruguay, Tahiti na Nigeria pia washindana katika kundi B.

R - record. Wastani wa mashabiki 60,625 waliangalia michuano ya mabara nchini Mexico mwaka 1999.

S - sita. Michuano hii itachezwa kwenye viwanja sita tofauti ndani ya nchi ya Brazil.

T - technology. Goal-line technology itatumika, huku kampuni ya kijerumani GoalControl GmbH ndio itatoa 14 high-speed cameras – saba kwenye kila goli.

U - Uruguay. Kikosi cha Oscar Tabarez ndio timu ya pili kutoka Amerika ya Kusini kwa pamoja na wenyeji Brazil, kufuzu michuano hiyo - walibeba ubingwa wa Copa America mwaka 2011 - lakini hawajawahi kubeba ubingwa wa mabara katika historia yao.

V - vuvuzela. Vifaa hivyo vya kushangilia vimepigwa marufuku  - Brazil walitengenezwa vya kwao walivyovipa jina la caxirola, vimepigwa marufuku kutokana na kelele zake kuumiza kichwa.

W - winners. Brazil wana matumaini ya kuondoka na ubingwa huu - wamebeba mara tatu kombe la mabara (1997, 2005 na 2009), lakini Selecao wameishiwa kuwa washindi wa pili na robo fainali mara mbili huku kombe la dunia likiwa limepangwa kufanyika mwaka unaofuatia.

X - Xavier Samim. Golikipa wa Tahiti Xavier Samim atapambana na Mickael Roche kugombania nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya kumpokonya namba wakati wa michuano ya OFC Nations Cup.

Y - Vicente Yanez. Mhispania huyu anaaminika kuwa mtu wa kwanza kutoka ulaya kutia mguu ndani ya nchi ya Brazil huko katika miaka ya 1500.  Je timu ya taifa ya Spain watamuenzi mhispania mwenzao kwa kubeba kombe ndani ya nchi ya Brazil?

Z - Zagallo, Mario Zagallo. Kocha huyu raia wa Brazil mwenye miaka  81 aliiwezesha Brazil kubeba ubingwa huo mwaka 1997, Pia aliiongza Selecao kubeba ubingwa dunia mwaka 1970.

NOTE *Italy wamefuzu kushiriki michuano hii baada ya kuwa washindi wa pili wa Euro 2012 . 

No comments:

Post a Comment