Siku kadhaa baada ya Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati - CECAFA kuidhinisha michuano ya kombe la Kagame kuchezwa mjini Darfur -Sudan, serikali ya Tanzania imetoa tamko kuhusu timu za Simba na Yanga kwenda kushiriki michuano hiyo huko Sudan kwenye eneo ambalo limekuwa likiandamwa na vurugu kwa miaka kadhaa sasa.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga ni kwamba serikali haidhani ni busara kwa vilabu vya Simba na Yanga kwenda kwenye eneo hilo kushiriki Kagame Cup kutokana hali mbaya ya usalama iliyopo Darfur.
HIVI NDIVYO ALIVYOANDIKA KAMWAGA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.
Ezekiel Kamwaga
Breaking
News...... Serikali imesema haioni busara ya Kagame Cup kupigwa
Darfur.... Hakuna hoteli ya maana na watu wanashauriwa kutembea na
fulana zinazozuia risasi kupenya... Nadhani hii ndiyo stori kubwa ya
kimichezo kwa leo.... Je, mnadhani itakuwa busara kwa Simba na Yanga
kushiriki?
Kwa hili sijawahi kuelewa toka mwanzo, huyu msonye na tenga hawawezi kuwa serious kwa hili, yanga walitaka uhakika wa usalama toka serikalini labda haya ndo majibu yake, tatizo nyie wenye mic mnainterest zenu, kwenye suala serious hili mkalinyamazia. Nakumbuka ilipotangazwa mara ya kwanza maestro alisema msonye anatania then ikawa kimya kama ni mahari salama. Serikali ishasema dafjr sio mahali salama tusipeleke watoto kule, guest za kule ni klntena hakufai kila mtu ana bunduki ya kivita
ReplyDeleteyaani kwa hali hiyo wasiende kwanai uhai haununuliwi nazi ndio zinazonunuliwa na hawa CECAFA kwanini wamepeleka mashindano hayo huko wakati wanajuwa hali si shuari
ReplyDeleteyaani tuseme labda wachezee kule mtwara.
ReplyDeleteMh! Ivi kumbe? Lkn kuna tofauti sana na huku kwetu? Maana hatu huku watu wanakufa ovyo tu mbona.
ReplyDeleteI have never trusted Musonye and I will never treat him as a serious man.......tangu day one mimi nikajua he was in a process to make followup kuhusu huko Sudan but ikawa kimya....dah Tenga anamaliza TFF majanga anamaliza CECAFA majanga WHY....!!!!?
ReplyDelete