Usiku wa kesho dunia itapata nafasi ya kushuhudia mechi ya kukata na shoka kati ya timu za mtaifa mawili zenye utajiri wa vipaji na historia nzuri katika soka la kimataifa. Spain vs Brazil ni mechi ambayo ilikuwa ikisubiriwa sana na wapenda soka hasa wa kizazi cha sasa.
Brazil ilitawala sana miaka mingi iliyopita wakiwa mabingwa wa mara tano wa kombe la dunia, lakini sasa Spain La Roja ndio timu inayotawala kwenye soka la kimataifa - wakiwa hawajafungwa kwenye mechi yoyote ya kimashindano tangu mwaka 2010 - wakichukua makombe makubwa matatu (Euro 2008, World Cup 2010, Euro 2012) katika kipindi cha miaka ipatayo mitano, na kesho wapo katika harakati za kuandika historia ya kutwaa makombe yote manne makubwa watakapocheza fainali ya kombe la mabara dhidi ya Brazil kwenye uwanja wa Maracana - Rio de Jeneiro. Je Brazil watarudisha utawala waliopoteza au Spain wataendelea kushikilia usukani mwa soka la kimataifa?.
HISTORIA
Katika michezo nane ambayo timu hizi zimekutana, spain wameshinda mara moja tu - zamani sana mwaka 1934. Lakini kipindi hicho Spain lilikuwa taifa dogo sana kwenye soka - Brazil na Uholanzi wakiwa wapo juu. Mechi yao ya mwisho iliyozikutanisha timu hizi mbili ilikuwa mwaka 1999, iliisha kwa sare 0-0. Brazil kwa sasa hawapewi nafasi kubwa ya kuifunga Spain - ingawa usiwadharau Selecao ambao hawajafungwa kwenye ardhi yao katika mechi nne za kimashindano dhidi ya Spain - wakishinda mechi 3 na kutoa sare 1.
JE WAJUA?
- Brazil wameshinda 11 mfululizo za kombe la mabara. Pia wameshinda michuano micwili iliyopita ya mashindano haya (2005 and 2009), na hii ni fainali yao ya 3 mfululizo.
- Spain wamecheza mechi 29 za mashindano bila kufungwa - hawajapoteza mechi tangu walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza ya kombe la dunia 2010.
- Spain ndio timu inayoongoza kupiga pasi zilizokamilika katika michuano hii - asilimia 92. Wamepiga pasi 3052 ukilinganisha na Brazil waliopiga pasi 1783. Watani wa 84.5%.
- Spain wameruhusu mashuti nane tu yaliyolenga lango lao katika michezo minne waliyocheza kwenye michuano hii mpaka sasa.
- Torres amefunga mabao nane katika historia ya kombe la mabara. Ni Cuauhtémoc Blanco (Mexico) na Ronaldinho (Brazil) ambao wamemzidi kwa kufunga mabao (9).
- Fred amefunga mara nane katika michezo 10 aliyoichezea Brazil. Matatu kati hayo 10 ameyafunga kwenye michezo miwili iliyopita kwenye kombe la mabara.
No comments:
Post a Comment