Siku chache baada ya vilabu vya Simba, El Merreikh na Al Hilal kusema havipo tayari kushiriki michuano ya Kagame Cup iliyopangwa kupigwa nchini Sudan kwenye eneo la Darfur kwa kuhofia usalama wao, leo hii Tusker F.C ya Kenya wamesema rasmi kuwa
wamejiondoa kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuanza
mwezi ujao.
Wanasema eneo hilo sio salama.
Hatua ya kilabu ya Tusker, inakuja licha ya hakikisho kutoka kwa Bwana Magdi Shams Eldin katibu mkuu wa wa ligi ya soka ya Sudan katika barua iliyoandikwa kwa vilabu vyote tarehe 23 Mei mwaka huu.
Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda la Kenya, Sam Nyamweya amethibitisha kuwa, amepokea ombi kutoka kwa klabu ya Tusker ikielezea wasiwasi wa usalama wakisema kuwa hawawezi kuruhusu wachezaji wao kucheza katika eneo lisilokuwa na usalama na ni juu ya CECAFA kutafuta sehemu nyingine iliyo salama kwa wachezaji kutoka vilabu vyote kuweza kushiriki michuano hiyo
No comments:
Post a Comment