Mpango wa kumuuza Kiemba umekuja baada ya
mashushushu wa timu hiyo ya Morocco kuridhishwa na kiwango alichoonyesha
wakati akiichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu
Kombe la Dunia mwakani.
Katika mchezo huo, Stars ilifungwa mabao 2-1, huku
Kiemba akifunga bao nzuri la kufutia machozi kwa kiki ya mwendo mrefu
nje ya boksi la hatari.
Zakaria Hanspope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili
Simba, amelithibitishia gazeti la Mwananchi jana kuwa, mazungumzo ya awali ya
kuuzwa kwa kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga yako hatua za mwisho
kukamilika.
“Ni kweli, mazungumzo ya awali yameshafanyika kati
ya Simba na uongozi wa Wydad Ac Casablanca, leo tunamalizia
tulipofikia,” alisema Hanspope.
“Niko Morocco kufanya mazungumzo ya mwisho na
uongozi wa Wydad Casablanca, natumaini tutafikia mahala pazuri Mungu
akijalia,” alisema Hanspope.
Mmoja wa vigogo wa Kundi la Friends of Simba ndiyo
aliyeushtua uongozi juu ya mpango huo, ambao nao waliharakisha
kumsainisha mkataba mpya kabla ya kumuuza. Juzi, Simba ilimsainisha
Kiemba mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh35 mil.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
ni vizuri wakumbuke tu na wao kusajili,la sivyo nafasi ya kumi msimu ujao.
ReplyDeleteNafasi ya kwanza mbona hawauzi...Bora ipi kuwa wakumi nyumbani alafu nje kwenye viwango vingi kuwa wa kwanza...ndo hapo mimi napo aminigi kuwa yule wa kwanza hapa zile siyo juhudi binafsi..anakuwaga na msahada wa vile vyama vyetu viwili...team nzuri ina maana unakuwa na wachezaji wazuri sasa wewe team itakuwaje inashinda then wachezaji hawajuwi kucheza?????hahahhaha au ndo yale mambo ya kuitana KAPETO I mean wa HAPA HAPA...
ReplyDeleteAin't no court me wrong!!!ni mtazamo tu yaani mawazo tu.