REAL MADRID jana usiku imetoa tamko rasmi kwa Tottenham: Tunakuja kumnunua Gareth Bale.
Raisi Florentino Perez alikiri kwa mara ya kwanza kwamba Real Madrid wapo tayari kumsaini Bale na akitoa ishara kwamba watatuma ofa ya kwanza siku chache zijazo.“Inabidi tukiboreshe kikosi chetu tena kwa umakini mkubwa - hilo litafanyika ndani wiki chache zijazo.”
Perez pia alikiri kwamba ameshakutana mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy mwaka jana kuzungumzia juu ya usajili wa Bale.
Aliongeza: "Bale ni mmoja ya wachezaji wakubwa barani ulaya na Real Madrid siku zote timu yetu imekuwa na wachezaji wakubwa wa soka.
"Nilikutana na mwenyekiti wa Tottenham mwaka jana na haki na majukumu ya kutetea maslahi ya timu yake.
"Kuhusu bei iliyozungumziwa kuhusu Bale, wachezaji hawana bei kubwa au ndogo - wao ni kama uwekezaji kwenye biashara ya soka.
"Wachezaji wenye gharama zaidi ni wale ambao mara zote huwa ni uwekezaji kwenye biashara, na ikiwa watacheza vizuri basi lzima watengeneze faida kwenye uwekezaji huo."
Maneno ya Perez yanabeba uzito mkubwa ukizingatia ndio mtu aliyefanikisha dili kubwa kabisa kwenye historia ya soka duniani za usajili wa Luis Figo, Zinedine Zidane, David Beckham, Kaka na Cristiano Ronaldo.
No comments:
Post a Comment