Search This Blog

Thursday, May 30, 2013

USAJILI WA KISHABIKI/KUKOMOANA WA SIMBA NA YANGA UNAIDHOOFISHA TAIFA STARS



SIMBA na Yanga zote za Dar es Salaam zimeanza kuchuana kuwania saini za wachezaji nyota, lakini tayari hisia za ushindani, kukomoana na kuonyeshana jeuri ya fedha zimeanza.

Yanga imeingia Msimbazi na kumnyakua kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa ambaye alikuwa akiichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Azam FC. Simba iliwahi kutangaza kumsajili mchezaji huyo lakini imepigwa bao.

Muda mfupi tu baada ya dakika 90 kumalizika katika mchezo kati ya Yanga na Simba 18 Mei mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Yanga ikiwa imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, mashabiki wa klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani walimbeba Ngassa juu juu kama vile ndiye shujaa katika mchezo ule huku wakiwa wamemvalisha jezi ya rangi ya njano na kijani inayoyotumiwa na timu hiyo.

Hizo zilikuwa dalili za wazi za Yanga kumsajili Ngassa kwa mkataba wa miaka miwili. Saa 48 baadaye, Ngassa alitambulishwa mbele ya waandishi wa habari kwamba amejiunga na Yanga.

Baada ya pigo hilo, Simba nayo ikawa inafuatilia saini ya kiungo wa Yanga aliyemaliza mkataba na klabu hiyo, Haruna Niyonzima ili aweze kutua Msimbazi. Mengi yalisemwa lakini mwisho Niyonzima alionekana mbele ya waandishi wa habari akitangaza kuwa ameongeza mkataba Yanga.

Yanga imemsajili Ngassa, je, anakwenda kucheza wapi? Nani ataathirika na ujio wa mchezaji huyo?

Nafasi anayokwenda kucheza Ngassa ndiyo pia anacheza Simon Msuva kwa sasa. Hii ina maana ili Ngassa acheze, inabidi ama Msuva awekwe benchi au kiungo Frank Domayo apumzishwe. Ikitokea hivyo itabidi Niyonzima arudi kucheza kama kiungo wa kati halafu Ngassa na Msuva wagawane winga kila upande.

Kwa hali hiyo, ni wazi nafasi ya Domayo inaweza kuathiriwa siyo katika klabu yake tu, bali hata timu ya taifa kwani atakuwa akicheza kwa muda mfupi mno katika kikosi cha Yanga.

 
Hivi ndivyo alivyopotezwa Nizar Khalfan katika Taifa Stars; alipokosa nafasi ya uhakika katika kikosi cha Yanga, akakosa fursa ya kuonekana na akakosa kuitwa Taifa Stars.

Yanga inaendelea na usajili ambao kwa hakika umejaa zaidi ushabiki na ushindani na timu nyingine bila kuzingatia mahitaji ya timu. Hivi sasa Yanga inafanya kila linalowezekana kumsajili Kabange Twite aweze kuichezea timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu ya Bara, baada ya kushindwa kuitumikia timu hiyo msimu uliopita.

Ilipomsajili awali, Kabange kutoka FC Lupopo ikashindwa kumtumia kutokana na hitilafu katika uhamisho wake. Yanga ikikamilisha usajili wake, Kabange ataungana na viungo wengine kibao waliojazana kikosini hivyo kuendeleza kujaza wachezaji wa aina moja kikosini.

Kabange ataungana na Nizar, Nurdin Bakari, Niyonzima, Athuman Idd ‘Chuji’, Domayo, Ngassa, Msuva, Omega Seme, Hamis Kiiza (kama atabaki kikosini kwani mkataba wake umeisha) na wengineo ambao hadi sasa wangali wanawania nafasi ya kucheza.

Atakayekosa nafasi ya kwanza atakosa pia uwezekano wa kuitwa Taifa Stars.

  

Simba nayo imeshaanza harakati za usajili na tayari imeshamsajili kipa wa Kagera Sugar, Andrew Ntala, kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Ibrahim Twaha, Zahor Pazi na beki Issa Rashid wa Mtibwa Sugar.

Kwa usajili huu, Simba imefanya kitu kizuri lakini inaweza kuwa imechemsha kwa kipa Ntala ambaye hadi ligi inaisha, alikuwa kipa namba moja katika kikosi chake. Sasa ni wazi hatakuwa na nafasi mbele ya makipa Juma Kaseja na Abel Dhaira anaowakuta kikosini.

Kipaji cha Ntala sasa kinaelekea ukingoni, vinginevyo Kaseja aondoke sasa kikosini huku Dhaira naye akiachana na timu hiyo, nje ya hapo Ntala atakuwa mchezaji wa akiba msimu mzima. Uwezekano wa Ntala kuwa kipa nambari wani uko kwenye mikono ya aliyekuwa kocha mkuu wa Kagera Stars, Abdallah Kibadeni ambaye pia anahamia Msimbazi.

Kiungo Pazi anaweza kucheza kwani kwa nafasi yake na uzoefu alionao vinaweza kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji nyota watakaokuwa hawakosi nafasi kikosi cha kwanza kama itakavyokuwa kwa beki wa pembeni, Issa Rashid.

Tunaweza kuipongeza Azam FC kwa kutangaza mapema kwamba haitafanya usajili wowote mkubwa zaidi ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake ambao inao sasa huku mikataba yao ikiwa imeisha.

Kocha wa Azam, Stewart Hall na uongozi mzima wa timu hiyo, ni watu wanaoheshimu uamuzi wa kila upande kulingana na hali halisi tofauti na Simba na Yanga, ambazo hata shabiki anaweza kusajili.

MAKALA HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI

14 comments:

  1. Kwani Yanga wamesajili wangapi mpaka sasa,Usimba tu unawasumbua,Man U walimsajili RVP wakati wana washambuliaji kibao,tumechoshwa na makala zenu za kishabiki nyie waandishi wa Bongo.Mchezaji wa kawaida tu mtaandika BONGE LA MCHEZAJI LA SAJILIWA,SHAME ON U!!!!!

    ReplyDelete
  2. Shaffih,
    Hapa naona unachanganya, kuwa na wachezaji wazuri wengi ni nzuri kwa timu, kwani inaongeza ushindani kwenye timu. Si yanga tu, je unataka kutuambia Barcelona, Madrid , Bayen Munich, man u, na wengine wote hawa wapofu kwa kusajiri ?

    ReplyDelete
  3. Hakuna tatizo hata kidogo, kwani hata kwa wenzetu ulaya hayo tunayaona yakitokea sana, wachezaji kama Barrack,Kaka, Chamack, Kolo Toure, Sturridge,Song, Fabregas,Santacruz,Arshavin n.k yamewakuta, suala sio club, tatizo ni wachezaji wenyewe kutojua nini wanachoenda kukifanya na katika timu yenye watu wa namna gani?

    ReplyDelete
  4. Namkumbuka saaana sredojec milutin micho. Kocha wa sasa wa timu ya taifa ya uganda. Ktk moja ya mechi zilizochezwa hapa kwetu alipokuwa anafundisha yanga
    Aliombwa atoe ushauri wake kwenye matokeo ya timu ya taifa.yy alitoa kauli ambayo mpaka leo naikumbuka na kuipenda saaana hivyo napenda kuwakumbusha wapenda soka wenzangu baada ya kuisoma makala hii. Micho alisema alichogundua kwa wapenzi wa soka tz kila mtu ni Kocha
    Hivyo hata mimi ktk makala hii ni vyema aulizwe kocha atawatumiaje wachezaji hawa kwa manufaa ya timu na wao wenyewe ktk kuendeleza vipaji vyao.mbona unawasifu azam kwanini usihoji hawasajili wachezaji wengine huku msimu ulioisha wameshindwa kuchukua ubingwa lkn wanaona bado timu yao ni imara huku zingine zikijiimarisha zaidi wasiwasi wangu uhamaji wa ngassa umekuuma saana kwa mtizamo wa kishabiki nizar kaachwa timu ya taifa kabla ya kujiunga yanga kwa kupisha damu changa jiulize mbona nditi kaachwa naye kasajiliwa simba na yanga rai msubiri brandts muulize kitaalam utaelimisha wengi kiueledi.

    ReplyDelete
  5. Duuu, sasa mmezidi hili suala ngasa mkela sana sasa, kwa makala yako huna lolote unataka kumzungumzia ngasa. Bayern inaviungo bora kabisa na imefunga magoli mengi kuliko timu yoyote ila tayari imewasajili gotze na lewandowsik, unaseme simba safi hamuoni kama nafasi za hao mnaowaita chipukizi zitachukuliwa. Shaffii tunakuheshimu sana punguza unazi. Timu kubwa zote ulaya zinafanya usajiri itakua azam? Inawezekana ssb anataka kuiacha timu, timu mbovu ile tofauti na ya mwaka jana ndo isisajiri? Achane ujinga sio kila kitu wanachofanya azam ni kizuri, wana makosa mengi na wabinafsi sana

    ReplyDelete
  6. Thanx for a hot discussion coz Im so interested with it! Shaffih mm huwa kuna wakati nakubaliana nanyi na vivyo hivyo upo wakati ambao nakuwa mbali sana na ww kimtazamo, usajili wa Ngasa Yanga haujanistua sana ila kaa ukijua dogo Msuva bado hajafikia karba ya Ngassa xo kuja kwake kunamfanya aongeze juu na kufika kiwango kinachotakiwa! Wakati anacheza hadi anazomewa kocha aliendelea kumvulia kwa sababu hakuwa na mbadala, mm kwanza narejea kwenye suala ambalo linapelekea timu ya taifa kuwa mbovu ni sheria za kipuuzi kuhusu usajili wa wachezaji wa kigeni, TFF wanapoweka timu isisajili foreign playes zaidi ya watano ndo inaua mpira wenyewe coz kuna wachezaji wa kibongo wanacheza premier wakiwa hawastahili. Jambo hlo hlo ni sawa na utumbo utokeao wizara ya Elimu, kila mtu aende sekondari huku hana uwezo kiakili na haandaliwi vizuri! Hapa matokeo mazuri ni ndoto na mkiendelea kuandika kishabiki hv hamna mnacholisaidia soka la bongo. Mwacheni mwenye uwezo asajili wachezaji anaowahtaji suala la kuanza kuhoji atacheza wapi hlo haliwahusu coz hamna kocha anaetaka timu yake ifungwe, mbona hamhoji Mario Gotze atacheza wapi Bayern Munich na hata kusajiliwa kwa Pizaro na Manduzik mlisifu ilihali mshambuliaji nimpendae kuliko wote ulimwengu Super Mario Gomez alikuwa fomu ya hatari? Huko kwao timu za taifa haziathiriki ama vp? Ishu ya soka la bongo ni TFF na utoto wa wachezaji wenyewe, haya mengne waachie kina Brandts na Stewart wafanye kazi zao bila bughuza!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mkubwa umeongea point tupu hakuna cha kuongeza hapo. timu nzuri lazima iwe na kikosi cha pili imara na linapokuja suala la sub ni kutoa jembe kuweka jembe thus why tunaona timu kama madrid, man city barca na zingine zikifanya vizuri..ni lazima kuwe na ushindani wa namba ndani ya timu ili kuweka morali kwa wachezaji.

      Delete
  7. Shaffi sijakuelewa kabisa....!!!

    ReplyDelete
  8. Japo ni mawazo yako na unao uhuru wa kuyatoa, ila hapa Dauda sikubaliana na analysis hii uliyoitoa. Nimeisoma kwa umakini mkubwa na hoja hapa ni Ngasa kujiengua Simba. Kimsingi kusajili ni jambo moja na wasajiliwao kugombania namba ni jambo jingine. So acha timu zisajili na maswala ya technical aspects ni ya makocha maana wao ndo wanaotoa ushauri.

    Alamski.

    ReplyDelete
  9. Wachangiaji wamechangia vzr ila nao wameweka hisia mbele kama muandishi wa makala hii,mmemshambulia shaffih wakat hausiki ukisoma mwisho wa makala kuna jina la muandish na sio shaffih,kuna mtaalamu wa mambo ya hbr anasema sio kila kitu hbr zingine unasoma unaelewa na kuziacha au kuzipuuza tu,suala la ngassa kwenda yanga haziwezi athir timu ya taifa ila itampa changamoto kocha pmj na wachezaj wakomae zaidi wanapopewa nafasi ili waonekane,utakumbuka wakati simba inamsajil kapombe walimsajil kama bek wa kat na kipindi hicho simba akikuwa nyosso,kelvin yondan wakamsajil obadia,kapombe anaulizwa utacheza nafas gan alimwambia muandish kuwa mm naenda simba kucheza mpira....today hachez?taifa staz hayupo?muachen ngasa akapate changamoto kutoka kwa msuva na msuva apate changamoto kutoka kwa ngasa,kama canavaro anapopata changamoto timu ya taifa kutoka kwa agrey na ndivyo hivyo wanapopata changamoto bahanuz na teget kutoka kwa mrundi,that is football huwez kusema rooney kaisha cos ya rvp ndio maana ba na torres unawaona wanavyochemshana.

    ReplyDelete
  10. wakati ngassa anasajiliwa Simba nani alikuwa anamjua Chanongo,watu walikuwa wanasema kuwa huku Ngassa kule Okwi.na sasa Chanongo yupo Taifa Stars,na Ngassa mwenyewe akahamishiwa katikati,huku wakati mwingine akianzia benchi.Kwa hiyo suala la Msuva atacheza au la ni la kocha na bidii ya Msuva mwenyewe,suala la Ngassa atacheza nafasi gani ni la kocha na bidii ya Ngassa mwenyewe

    ReplyDelete
  11. Good, suala hapo ni ngasa kwenda yanga ndio imemuuma mwandishi wa makala. Mbona msuva na ngasa wote kwa pamoja wanaitwa staz. Brandts anajuwa nini anafanya yanga na viongozi wa yanga wanajuwa nini wanafanya. Usajili wa ngasa pekee yanga umekuwa gumzo mbona simba imesajili sijui kumi wale hamuifanyi mada?

    ReplyDelete
  12. Ucha kuzidisha unazi kupita kiasi na wewe una uhakika simba imesajili wachezaji kumi kanuni gani ya TFF inayoruhusu kipengele hicho? Kwa mtazamo wangu kama hili tunalijua tuache kulidumaza soka la bongo kwa kwa kukumbatia unazi wa Usimba na Uyanga wachezaji wetu watafanikiwa ndoto zao,lkn hapo ukimuuliza kila mchezaji hawezi kukwambia malengo yake ya mafanikio ya kucheza soka yaishie simba na yanga atakwabia nje ya nchi hii na hata bara.Sasa kwa swala la ngassa halina kificho ni mchezaji mzuri lkn kwa mfumo huu wa timu zetu hizi mbili simba na yanga linamuua soka lake hawezi kufanikiwa malengo makubwa ya soka analo kusudia.Hivi sasa mimi na wewe tungejisikia faraja TANZANIA ina wachezaji 10 wa kimataifa nje ya AFRICA.Lkn sasa tunao wategemea 2,SAMATA n ULIMWENGU sababu za tatizo hili ndiyo haya ya kukumbatia ujinga kama huu.Hivyo ni vizuri kuwashawishi wachezaji wetu wajaribu kuacha mfumo wa kizamani mpira ni ajira kubwa Duniani siyo hapa Tz.Shafii yuko sahihi unapomkosoa mtu hukurupuki una sababu za msingi za kumjenga na si unazi makusudio yake Ngassa alikua hastahili acheze tena hapa BONGO kwa jinsi anavyojituma. Pia Ngassa kinachomuaribu anapenda kuendeshwa na baadhi ya watu badala ya kujianglia yeye thamani yake.Kwahiyo hiyo mchango wangu ni huo maana mtazamo mkubwa uliongelewa humu ni wa USIMBA NA UYANGA kwa kumlaumu SHAFFII lakini yeye anamjua ngassa vizuri klko wewe unayemtetea.

    ReplyDelete
  13. Kwakweli mi' sikulaum mwandishi wa makala hii, ila nakupa pongezi kwani naamini umetoa changamoto kwa mchezaji, kwani pindi mchezaji mhusika akisoma makala hii atajifikiria na atajua wazi kuwa sasa anakwenda kwenye ushindani wa namba. vilevile kuwa na vikosi viwili vikali itakuwa faida kwenye timu. salamu kwenu MSUVA, DOMAYO, NIYONZIMA, NGASSA na CHUJI.

    ReplyDelete