Takwimu mbalimbali kutoka kwenye mchezo wa fainali ya Champions League kati ya Borussia Dortmund na Bayern Munich Wembley Stadium.
- Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes amekuwa kocha wa nne kushinda ubingwa wa ulaya na klabu mbili tofauti kufuatia kushinda ubingwa huo na Real Madrid mwakak 1998. Wengine waliofanya hivyo ni Ottmar Hitzfeld, Ernst Happel na Jose Mourinho.
- Bayern wamecheza fainali 10 za European Cup wakishinda tano na kufungwa tano - vikiwemo vipigo viwili katika fainali 3 za Champions league zilizopita.
- Bayern wanaungana na Liverpool kwenye listi ya timu zilizoshinda makombe mengi ya European, zikishinda mara 5 kila timu, wakiongozwa na Real Madrid waliobeba mara 9, AC Milan waliobeba mara saba.
- Dortmund wameingia fainali mara mbili wakishinda mara moja na kufungwa mara moja.
- Bayern wanaendelea kuikaribia rekodi ya kushinda makombe matatu ndani ya msimu mmoja. Wakiwa tayari wameshinda Bundesliga pia wapo njiani kucheza fainali ya kombe la Ujerumani June 1.
- Kikosi kilichoanza cha Bayern kilikuwa na wachezaji saba walioanza kwenye fainali ya mwaka jana dhidi ya Chelsea, wengine wanne Arjen Robben,
Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller - walicheza mwaka
2010 walipofungwa na Inter.
- Bayern imekuwa timu ya pili kushinda ubingwa huo baada ya kufungwa kwenye fainali ya msimu wa nyuma, AC Milan walifanya hivyo mwaka 1994.
- Ilikuwa fainali ya kwanza ya timu za Ujerumani na fainali ya nne kuktanisha timu zinazotoka kwenye taifa moja.
- Ushindi wa Bayern unamaanisha kwamba watakutana na mabingwa wa Europa msimu huu Chelsea ambao waliwafunga mwaka jana kwenye fainali ya champions league. Pia kuna uwezekano mkubwa vita ya Josep Guardiola dhidi ya Jose Mourinho ikatokea tena ikiwa Mourinho atapewa jukumu la kuiongoza Chelsea.
No comments:
Post a Comment