Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
57406 Watazamaji si kweli hata kidogo.Tulikaa hadi kwe ngazi za kuelekea kwenye viti. Jamani huu wizi wa wazi ivi uta isha lini jaman? uwanja huu una uwezo wa kuchukua watu elfu 60, au izi ticket 2594 ndo zile za waingia bure? Kwa upoo wa macho yangu tu watu walio inguia uwanjani jana si chini ya elfu75. Ila kwa utaratibu huu hatutafika mahali, kama mambo haya yata endelea huku wachache wakinufaika.
ReplyDeleteSimba na Yanga pamoja na team nyingine jengeni viwanja vyenu, huo mgawanyo wa mil mia si kitu. Endapo mchezo wa jana unge chezwa kwe kiwanja cha simba, mana wao ndo walio kua wenyeji. wangenufaika sana na mapato.
Mimi binafsi kama mdau wa soka, sikubaliani na hizi statistics hata kidogo.
Asante.
naungana nawe, vilabu vingejenga uwanja wao.. Vinginevyo mhuu
Delete