Search This Blog
Monday, May 20, 2013
NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia ku
malizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.
Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na kunishangilia pia.
Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngsa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Binafsi sikubaliani na mawazo yaliyotolewa jana na kipindi cha michezo cha clouds hasa jeffy siku zote mmekuwa mkionyesha kuwa mnajali zaidi proffesionalism na kuisisitiza na kuamini kuwa ipo hapa kwetu na ikubaliwe na mkasisitiza kuwa hamuoni tatizo kwanini refa israel nkongo abadilishwe kwenye mechi ya yanga vs simba mliamini na mkatuaminisha kuwa kwa kufuata weledi hakuna ambacho kingeharibika sasa iweje jana jeffy amtake mrisho ngassa awaombe radhi wapenzi na wanachama wa simba kwa kusaini yanga huku akiichezea simba kwenye mechi muhimu dhidi ya yanga .cha ajabu jeffy anaona wachezaji wa dortumund waliosajili bayern huku wakiwa na mechi muhimu dhidi ya timu hizo mbili nauliza nyinyi watangazaji mnaloliamini hamtaki litendeke tanzania bali ulaya tu. Kwangu mm naona jeffy anapaswa amuombe radhi ngassa vinginevyo aueleze umma mapungufu ya makusudi ya ngassa ktk mechi ile vingine vyo jeffy usimba na weledi wako vinakinzana
ReplyDeleteTatizo watangazaji mnaweka mbele kuhadithia mambo yanayotokea kama kwamba nasi hatujui.ninyi watakiwa kutoa habari zenye weledi wa kujenga,kukosoa na kuelekeza.
ReplyDeletefmimi ni simba damu but simlaumu ngasa na wala sijachukia ngasa kurudi yanga bado namkubali ni mchezaji mzuri namtakia mafanikio mazuri but angejipanga pindi anaongea kwa tv cuz hata kama unaichukia timu usionyeshe hadharani ongea ki profeshino na young africa wangejipanga kabla ya kukurupuka kumtambulisha mchezaji alie kwenye mazungumzo ya awali i ain't mad @ you young africa..just a thoughts
ReplyDelete