May 21st
2003 ni tarehe ambayo Jose Mourinho akiwa na kikosi cha
FC Porto alishinda ubingwa wa UEFA Cup kwa kuwafunga Celtic. Tangu
wakati huo alienda na kushinda makombe mawili ya Champions League na
makombe ya ligi katika nchi nne tofauti. Kunaweza kukawa na ubishani
mdogo tu kwamba ndiye kocha aliyetawala katika kipindi cha miaka 10
iliyopita,
japokuwa muda wake ndani ya Madrid umeisha vibaya.
2013 umekuwa mwaka wa mwisho wa zama za makocha wengi na wachezaji. Kwa baadhi yao wamekuwa wakisifiwa kwa kazi zao ingawa kwa mtu mmoja -
Special One,wakati wake ndani ya Madrid unaangaliwa kama wakati ambao umemfelisha Mourinho kama kocha.
Baada ya kipigo kutoka kwa Atletico kwenye fainali ya Copa Del Rey Jose
Mourinho aliulezea msimu huu kama ndio m'bovu kuliko yote kwenye maisha yake ya soka. Ulikuwa wa shetani kwa Madrid huku michezo miwili ikiwa imebakia, Mourinho alitolewa nje kwa kumtusi mwamuzi akiiacha Madrid ikiwa imeghafirika dimbani dhidi ya wapinzani wao wa jadi. Mafanikio pekee aliyoyapata ndani ya msimu huu ni ubingwa Spanish SuperCup.
Msimu uliopita Madrid walikuwa makini, wenye hamu ya kufanikiwa na wakiwa na umoja katika kuuvunja utawala wa Barcelona. Pointi zao walizopata kwenye LA LIGA zilivunja rekodi, walifunga mabao mengi na wangeweza kuzidisha idadi hiyo kama wangekuwa makini. Wangeweza kufanikiwa zaidi msimu uliopita kama wangeshinda kwenye penati kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya - kufungwa kwao usiku ule ulikuwa mwisho wa umoja wao. ere driven, determined and importantly
together in their quest to overcome Barcelona.
Madhara ya kutokuwa na umoja yalionekana msimu huu. Hamu ya kutaka kufanikiwa ulaya zaidi ilizaa sumu iliyokuwa ikimtafuna Mourinho, ligi ikaonekana haina umuhimu hivyo ndivyo atleast kiwango na matokeo yalivyokuwa yakionyesha. Real walikuwa kwenye kiwango cha kawaida sana kwenye ligi wakikosa nguvu na muamko. Kama mlengo ulikuwa ni UCL, basi approach haikuwa sahihi, nguvu nyingi zilitumika mwanzoni na wakati wakielekea mwisho ndivyo nguvu ilivyopungua. Kiwango walichoonyesha kwenye mechi dhidi ya Manchester United na Galatasary kilikuwa cha wastani, aibu ikawakumba kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Dortmund waliocheza kitimu dhidi ya Madrid waliokuwa wakicheza kibinafsi
NUSU FAINALI 3 ZA CHAMPIONS LEAGUE HAYAKUWA MAFANIKIO NDANI YA MADRID
Nguvu ya Mourinho ilianza kufifia mwaka uliopita, tabia yake ilianza kuchosha na kutambua kwake kwamba msimu huu utakuwa wa mwisho kwake ilizidi kufanya hali kuwa mbaya. Alianzisha vita ambazo zilikuwa ngumu kwake kushinda na mwishowe wake zikaleta mgawanyiko kwa wachezaji na yeye mwenyewe.
Kama hii ilikuwa ndio plan yake ya kulazimisha kuondoka Madrid anaweza akawa amefanikiwa. Timu yake ilikuwa imesambaratika msimu mzima na anaiacha klabu hiyo kwenye hali mbaya. Ndio kuna wachezaji wa kiwango cha dunia kwenye timu hii ya sasa, lakini inahitaji kuundwa upya iwe kitimu zaidi. Kuondoka kwa Mourinho ni jambo zuri kwa pande zote
Kipigo cha Copa Del Rey kimeonyesha kwa picha safi nini kilikuwa tatizo msimu huu na Mourinho ndio mtu wa kulaumiwa. Ataondoka Madrid mwishoni mwa msimu huu, na mabaya yake yamemfanya kuonekana amefeli kufanya kile alicholetwa kufanya ndani ya Madrid. Jukumu kubwa lilikuwa kushinda ubingwa wa Champions League ambao ameshindwa, nusu fainali 3 zinaweza zikawa rekodi nzuri kwa timu nyingine lakini sio Madrid.
Kombe moja la ligi ndani ya miaka 3 na moja la Copa Del Rey ni mafanikio kidogo kwa kocha wa aina yake aliyepewa matumaini makubwa kutokana na kauli zake mwenyewe. Mourinho ni kocha anayejijali yeye zaidi kuliko timu yake, napenda kuwa juu ya klabu - hii inatajwa kuwa sababu mojawapo iliyomnyima kazi Manchester United. Anakosa ujuzi au hali ya kujtaka kujenga timu kwa malengo ya muda mrefu. Hili ndio limemwangusha ndani ya Madrid.
BARCELONA
Ukweli ni kwamba sababu nyingine kuu iliyomleta Mourinho Bernabeu ilikuwa ni kuuvunja utawala wa Barcelona. Alijaribu lakini hali imerudi vilevile sasa hivi wamerudi kwenye kivuli cha wapinzani wao. Alipowasili Santiago Bernabeu alikumbana na kipigo kibaya cha 5-0 na matokeo yake yake mbinu za mchezo wa Mourinho zikabadilika ndani ya Madrid.
Mbinu zake za kucheza dhidi ya Barcelona zilibadilika kabisa na badala ya kufanya mabadiliko kadhaa kwenye timu yake, alikiri kwamba timu yake ni haiwezi Barca na njia pekee ya kucheza dhidi yao na kuwashinda ilikuwa kwa mbinu chafu za vurugu na udanganyifu.Ikiwa tu angeweza kuiendeleza timu yake kwa mfano wa Dortmund na Bayern Munich labda tayari angeweza kuumaliza utawala wa Barcelona kwa kupata mafanikio zaidi hata kwa kubeba kombe la ulaya.
Baada ya majaribio kama 10 kwa mbinu zake Mourinho akaanza kufanikiwa lakini alikuwa ameshachelewa. Barca walionyesha kuwa na mentallity na imani kwenye aina ya mchezo wao na kuwa na mchezaji aina ya Messi waliweza kufanya visivyowezekana pale ilipohitajika. Pamoja na vita ya umalaika vs ushetani baina ya Mourinho dhidi ya Guardiola uliifanya El Classico izidi kuandamwa na vituko, lakini mwisho wa siku Guardiola alimshinda mpinzani wake.
Vita hii ilimfanya Mourinho aonekane mkorofi mwenye mbinu chafu hata ushindi wake ulikuwa wenye malalamiko. Huyu hakuwa kocha mwenye heshima bali mwenye wivu na majivuno. Mourinho aliwasili Santiago Bernabeu akiwa bingwa wa ulaya kama ilivyokuwa wakati akiwasili Chelsea ingawa muda huu alikutana na kiboko yake ambaye hakumpata England.
Alidhalilishwa na Guardiola, aliyekataa kucheza mchezo alioutaka Mourinho. Hivyo ikazaliwa vita ya class vs fashion kati yao. Katika miaka iliyopita Mourinho alionekana kama kocha kijana mnadhifu mwenye kuvaa Armain Suit lakini bado Guardiola alimshinda hata kwenye vita hiyo. Ukweli ni kwamba Barcelona na Guardiola walionyesha dhahiri ya ubovu wa Mourinho.
VITA BINAFSI MBELE YA MASLAHI
Vita ya Mourinho dhidi ya Barcelona, ilipelekewa na mreno huyo kunyimwa kazi mwaka 2008, alisahau kuweka umakini wake kwenye klabu yake aliyoifundisha kwa miaka 3. Vita yake na Barcelona haikuharibu sifa yake binafsi bali pia na ile ya Madrid.
Unaweza ukajaribu kubisha kwa namna alivyoileta uimara kwenye ambao haukuwepo miaka mingi iliyopita, lakini Pellegrini angeweza kufanikiwa zaidi ikiwa angepewa nafasi ya kuendelea kuwa kocha baada ya msimu wake aliomaliza na pointi 96. Pia Pellegrini asingeweza kusababisha migongano na matatizo kwa wachezaji na klabu kwa ujumla.
Ndio maana haikushangaza kuona wachezaji wake wenyewe wakikosana nae - pia haikushangaza kuona wale wachezaji wanaoijua Madrid haswa kiundani walianza kutofautiana nae. Wachezaji ambao tayari walishakuwa na medali za ubingwa wa dunia waliambiwa wacheze mchezo ambao hawakuupenda ili kuweza kuwashinda Barcelona. Haikuwa kama ilivyokuwa kwenye vilabu alivyopitia huko nyuma ambapo aliweza kuwashawishi kuamini kwenye mbinu zake. Kwa sababu tofauti na Porto, Chelsea na Inter, wachezaji wa Madrid tayari walishakuwa washindi. Na baadhi ya wachezaji wa kihispania walikuwa kwenye timu ambayo inasifika kwa kucheza soka safi kuliko timu zote ulimwenguni.
Kwenye macho yao waliona mbinu za Mourinho zilikuwa zinatofautiana na utamaduni wa Spain na ule wa Madrid. Ugomvi wake na Ramos na Casillas ulikuwa kielelezo tosha. Alipoteza imani ya wachezaji muhimu ndani ya timu, matamanio ya Mourinho yalikuwa kuwadhibiti wachezaji hao ili kuweza kutawala vizuri. Lakini hili ndio likazidisha tatizo, wachezaji hawa haswa Casillas alikuwa mkubwa na mwenye umuhimu ndani ya klabu kuliko Mourinho. Kama ingetakiwa mmoja aondoke baina yao basi Casillas angebaki.
Ndio mwanzoni alipewa rungu na akaweza kumuondoa Raul, lakini kadri siku zilizovyokuwa zikienda ndivyo alivyozidi kugundua Casillas ni kizingiti kikubwa katika utawala wake - na hii ni moja ya sababu zilizomuangusha Mourinho ndani ya Madrid.
Ingekuwa Mourinho angeweza kumtumia vizuri kipa basi angeweza kujiletea mafanikio binafsi na ya timu lakini badala yake akaamua kuwa na vita nae . Ukosefu wa umoja na ushirikiano ndani ya kikosi ndio sabau kuu ya anguko la Madrid msimu huu na mtu wa kumlaumu ni Mourinho mwenyewe.
Sio "Special One" tena
Mwanaume huyu aliyewasili mwaka 2010 akiwa bingwa wa ulaya, The Special One anaondoka Madrid akiwa amefeli na chini ya kivuli cha kocha aliyefanikiwa zaidi kwenye kipindi cha miaka 10 iliyopita. Swali ni - je tumeshaona ubora wote wa Mourinho? Makocha kama Guardiola na Klopp wanaonekana kuwa makocha wa kisasa zaidi wenye kujiheshimu. Tunashuhudia kizazi cha makocha wapya na nina mashaka kwamba Mourinho atapata mafanikio yoyote yatakayokaribia mafanikio aliyoyapata muongo mmoja uliopita.
Ikiwa atarudi Chelsea kama inavyotegemewa itadhihirika kwamba amefeli kwenye levo ya juu, ndio alikuwa bora kwa miaka kadhaa iliyopita lakini amefeli ndani ya Madrid na kuvionyesha vilabu kama United, Barcelona na Bayern Munich kwamba hafai kuwa kiongozi ndani ya timu zao. Hata Man City ambapo wafanya maamuzi ni watumishi wa zamani wa Barca inaonekana hawataki kujihusisha nae. Ukweli ni kwamba Madrid imempotezea sifa yake kama kocha bora kutokana na kufeli kufanya kazi kama ilivyopaswa.
Sio kocha mbaya sana kinachomwangusha ni tabia yake ya ukorofi mpaka kwa wachezaji wake mwenyewe! Anapenda sana kile afanyacho yeye kiwe sahihi 100% kitu ambacho kwenye soka sio sahihi sana maana yeyey kama kocha haingii kucheza mpira yeye anaingia kama mwalimu wa mpira na kumlazimisha mchezaji kufanya atakavyo yeye wakati yeye hauchezi mpira anakosea sana hapo! Na hii ndio sababu madrid hawamtaki tena maana anadharau ma legendary wa pale na ni tabia yake toka huko alikotoka
ReplyDeleteShaffih mie napingana na hoja yako yakusema mourinho ameshindwa na ndio mwanzo wakupotea kwake, Ukosefu wa umoja na ushirikiano ndani ya kikosi ndio sabau kuu ya anguko la Madrid msimu huu ila naamini kuwa mourinho nikocha mahiri na anae weza kutumia wachezaji tofauti kutengeneza timu bora, nadhani madrid ya msimu uliopita sio ile tulio iona msimu huu...!! ndio yale yanayosababishwa na ungozi wa club kuingilia maamuzi ya makocha
ReplyDelete