Search This Blog

Wednesday, May 8, 2013

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC VS MGAMBO

Full time Simba 1 - 0 Mgambo

Dk 90 Zimeongezwa dakika tatu za nyongeza.

Dk 88 Simba inaendelea kumiliki mpira na hakuna dalili ya kusawazisha bao.

Dk 81 Simba imefanya mabadiliko ametoka Messi ameingia Salim Kinje. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 75 Haruna Shamte wa Simba anamchezea rafu Fully Maganga wa Mgambo.

Dk 73 Kandulu wa Mgambo anachezewa faulo nje kidogo ya lango la Simba.

Dk 65 Messi wa Simba anaichambua ngome ya Mgambo lakini anashindwa kupiga shuti langoni. Simba 1-0 Mgambo

Dk 59 Mgambo wanafanya mabadiliko ametoka Chande Magoja ameingia Musa Ng'unda.

Dk 56 Issa Kandulu wa Mgambo anakosa bao la wazi akishindwa kuunga mpira kwa kichwa. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 45 za kipindi cha zinaanza Simba inafanya mabadiliko anatoka Chollo ameingia Omar Salum.

Dk 45 HALF TIME! Simba 1-0 Mgambo.

Dk 45 zimeongezwa dakika mbili. Simba 1-0 Mgambo.

Dk 40 YELLOW CARD..! Chollo anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.

Dk 30 Simba inafanya mabadiliko anatoka William Lucian ameingia Rashid Mkoko.

Dk 25 YELLOW CARD....! William Lucian wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya beki wa Mgambo!

Dk 20 Amri Kiemba anashindwa kuunganisha krosi safi ya Chollo akiwa peke yake na kipa wa Mgambo, Mmassa.

Dk 19 Peter Mwalyanzi wa Mgambo anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini kipa Juma Kaseja anaudaka mpira.

Dk 15 Kipa wa Mgambo, Godson Mmassa anagongana na Chollo mpira unasimama kwa muda ili kipa atibiwe.

Dk 14. Simba inapata kona lakini wanashindwa kuitumia vyema.

DK 8 Haruna Chanongo anaipatia Simba bao la kuongoza.

Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa.

Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Miraji Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian, Amri Kiemba, Ramadhan Chanongo 'Messi' na Haruna Chanongo.

Mgambo JKT; Godson Mmassa, Salum Mlima, Ramadhan Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.

2 comments:

  1. "MALKIA NA RAGE TUAMBIENI KWELI TAFADHALINI"

    1.Hivi Di Canio Na kikosi chake Hiki Kilichobaki Ligi Kuu Kuna Nafasi ya hawa Viumbe kucheza?

    2.Di Canio Anahitaji Aina ya Wachezaji wa UBORA kama NGASSA na KAPOMBE kushindana BALE na Kina PODOLSKI?

    Hivi Sunderland Walivyosema INVEST IN AFRICA walimaanisha Kuchukua LOW CLASS?

    NB: Di Canio "FASCIT" Ni Meneja Mwenye Msimamo Hakurupuki kwenye Hili.

    Angalia Squad Hii kisha Sema Nani Atawekwa Benchi hata kama Wakifuzu NGASSA NA kAPOMBE.

    Sunderland FC Squad List
    Goalkeeper
    20.Keiren Westwood

    Defence
    2.Phil Bardsley
    5.Wes Brown
    12.Matt Kilgallon
    16.John O'shea
    19.Titus Bramble
    24.Carlos Cuellar
    42.John Egan

    Midfield
    .Danny Rose
    6.Lee Cattermole
    7.Sebastian Larsson
    8.Craig Gardner
    14.Jack Colback
    15.David Vaughan
    18.David Meyler
    21.Adam Johnson
    23.James Mcclean
    28.Stephane Sessegnon
    37.Adam Reed

    Forward
    9.Fraizer Campbell
    10.Connor Wickham
    17.Dong-Won Ji
    25.Louis Saha
    26.Steven Fletcher
    38.Craig Lynch

    RAGE NA MALKIA TUAMBIENI UKWELI TAFADHALINI KAMA MNATALII TUJUE LAKINI MIPANGO HIYO SAHAU KABISA.

    ReplyDelete
  2. Comment yako na hii habari vinahusiana nini? Halafu we ni wa zamani sana ambaye hata hujiulizi kina adam nditi, mariga, wanyama, nonda, mayuka na olirch wamewezaje kucheza mpira kwenye ligi kubwa. Endelea kuamini kuwa wachezaji wa kitanzania hawawezi kucheza nje.
    Kitu kingine ambacho naona hujui kuhusu mpira wa kulipwa ni kuwa si lazima mchezaji akienda aingie kikosi cha kwanza moja kwa moja, inaweza kuchukua muda kidogo, pengine hata ikibidi atatolewa kwa mkopo kwenda timu ndogo zaidi.
    Kwa hyo acha kabisa kuchanganya siasa za kina rage na uwezo wa wachezaji wetu. Mchezaji kama Kapombe akipata mkufunzi mzuri anaweza kufika mbali. Kama hawataenda ni kwa sababu hakujawa na mpangilio mzuri na wala si vipaji. ACHA KABISA KUVUNJA MOYO WACHEZAJI WA KITANZANIA KWA KUSEMA HAWAWEZI. ACHA KUVUNKA MOYO WACHEZAJI WA KITANZANIA KWA SIASA ZENU ZA KIJINGA.

    ReplyDelete