Kwenye mchezo wa mwisho wa kihistoria wa Alex
Ferguson mbele ya mashabiki zaidi ya 70000 ndani ya Old Trafford aliamua kumcheza Paul Scholes na kumuacha Wayne Rooney katika timu yake ya siku hiyo. Alisema kwamba alihisi akili ya Rooney ilikuwa sehemu nyingine baada ya mara nyingine kuomba kuondoka Old Trafford. Ferguson alisema amekataa ombi hilo na anaamini Rooney anahitaji muda tu kufikiria kwa kina kuhusu uamuzi wake, lakini naamini Rooney ni tatizo ambalo kocha mpya hahitaji.
Wayne
Rooney alikuwepo uwanjani huku akicheka na kufurahia na wenzie kwa kuimba nyimbo za ushindi. Alionekana kuwa na furaha kabisa. Ulikuwa ni ushangiliaji ule ule ambao aliokuwa nao siku walipothibitisha ubingwa wao kwa kuwafunga Aston Villa alipokimbia na kwenda kumdandia mabegani Van Persie. Huyu hakuwa mchezaji ambaye hakuwa na furaha na mwenye kutaka kuhama, kwa hakika usingeona kama alikuwa na tatizo lolote. Lakini huwezi kuwajaji wacheza soka kwa ushangiliaji wao uwanjani bali ni uchezaji wao na ukweli ni kwamba katika miezi kadhaa iliyopita kiwango cha Wayne Rooney kimeonyesha kwamba mchezaji huyo hana furaha na maisha yake ndani ya Man United.
Wakati Rooney
alipoibuka kwenye ulimwengu wa soka alionekana kuwa na kila kitu cha kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani. Kwenye Euro 2004 alionekana kuwa na kasi, mwenye njaa ya mafanikio na adui mkubwa wa nyavu za wapinzani. Uhamisho wa kwenda United ulionekana sahihi kabisa - sehemu nzuri zaidi ya kukuza kipaji chake, lakini ikiwa karibia muongo mmoja umepita unaona kwamba Rooney hajafikia kule alipotakiwa kuwa. Kipaji ambacho kilitoa ahadi kubwa kimekosa msimamo imara.
Je Ferguson ameharibu kipaji?
Unaweza kumlaumu Alex Ferguson kwa kufeli kwa Rooney kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani. Cristiano Ronaldo alichaguliwa kuwa mtoto wa kipekee ndani ya United wakati wawili hao wakiwa chipukizi na Rooney akawa mlishaji wa Ron kuliko kuwa mchezaji ambaye timu inamzunguka. Ndio Rooney alikuwa bora, lakini bado Ronaldo alipewa uhuru wa kuwa mchezaji muhimu wa timu na kujijenga kuwa mchezaji bora kabisa. Rooney akawa Robin kwa Batman.
Je Ferguson angeweza kujenga timu kwa kumzunguka Rooney na kumsaidia kumjenga kuwa bora kabisa kama alivyotegemea baada ya Euro 2004? Inawezekana kabisa. Lakini Ferguson ni mtu ambaye anaangalia zaidi timu kuliko mchezaji binafsi na imani yake ilimtuma kwamba mafanikio ya timu yangekuja kwa kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji muhimu wa timu. Ni vigumu kubisha ukiangalia namna United walivyopata mafanikio Ronaldo alipokuwepo kama mchezaji anayecheza akiwa huru kwa timu kumzunguka yeye.

Sina mashaka kabisa kwamba kiwango cha Rooney kiliathiriwa na kucheza kwenye kivuli cha Ronaldo kwa muda mrefu na akakosa kuwemo katika ile miaka ya kujiendeleza ambayo ni wachezaji wachache wanapata. Hivyo si sawa kujaribu kwa sasa kumfananisha na wachezaji aina ya Messi na Cristiano. Pia Rooney amekuwa akitumika kama 'kiraka' na hilo nalo likamdumaza chini ya Ferguson.
Sio wachezaji wengi ambao wanaweza kuwa na ubora wa Rooney - kuweza kucheza popote pale mwalimu wao anapowataka kufanya hivyo, lakini hilo bado halikuweza kumfanya kuwa mchezaji wa daraja la juu kabisa duniani.
Kuomba kwako uhamisho
Mwaka 2010 wakati alipoongea hadharani kuhusu timu kukosa hamu ya mafanikio kwa kutosajili wachezaji wa daraja la juu, aliiweka United kwenye hali ya utata. Mwaka mmoja baada ya kuwapoteza Tevez na Ronaldo na kuwaleta wabadala Owen na Valencia ilikuwa wazi kabisa United walishuka kiubora. Ni kweli alichosema Rooney kuhusu timu yake lakini pia jambo hilo lilikuwa kinyume kabisa na utamaduni wa United.
Unaweza ukafikiria namna maoni yale ya Rooney yalivyomkasirisha Ferguson na kibaya zaidi hakuwa na namna zaidi ya kufanya liwezekanlo na kumbakisha mchezaji wake tegemeo kuliko kumpoteza kwa Man City - ingekuwa ni tukio baya sana kwa United na mashabiki wake. Rooney akabakia United, na akishinda vita yake dhidi Fergie aliyejifanya mdogo na kumuomba Wayne abaki na tofauti na sera yake ya kuwafukuza wachezaji mastaa waliojiona wakubwa kuliko timu kama akina Beckham, Keane na Stam. Tangu wakati huo Rooney amekuwa sehemu ya timu japokuwa sio tegemeo kama ilivyokuwa huku nyuma.
Kwa matatizo yote ambayo yameonekana kuwepo baina ya Fergie United wameweza kubeba kombe lao msimu huu. Kwa kifupi msimu huu imeonekana wazi United hamhitaji Rooney kuweza kucheza vizuri. Usajili wa Robin van Persie na Shinji Kagawa ulileta maswali ya haraka haraka. "Ni wapi Rooney atacheza?" na ingawa Ferguson amefanya kazi nzuri katika kubadilisha kikosi chake ni wazi kwamba Van Perise ndio kiongozi wa mashambulizi ya timu na Kagawa na Welbeck wapo tayari kucheza kama wasaidizi wake.

Mechi dhidi ya Madrid zilionyesha wazi; Ferguson aliamua kumtumia Kagawa kwenye mechi ya kwanza na Welbeck katika mechi ya pili, Rooney alionekana kuwa angefaa zaidi kucheza kwenye jukumu la kuilinda timu katika mchezo wa pili. Fundisho lilonekana dhahiri, ikiwa utamkera Ferguson usidhani atasahau. Msimu wa 2010-11 Ferguson alimhitaji Rooney, lakini David Moyes ndani ya mwaka 2013 hamhitaji.
Rooney hahitajiki tena
Ferguson amemuachia Moyes timu nzuri sana yenye mchanganyiko mzuri wa wachezaji wenye uzoefu na wanaochipukia kuwa wanasoka wenye vipaji vya hali ya juu.
Kagawa atakuwa bora zaidi msimu ujao na kama akifikia ule uwezo aliokuwa na Dortmund basi mashabiki wa United wategemee makubwa zaidi.
Ndio Moyes ataweza kupata changamoto za kuondokana na uzoefu ndani ya timu katika miaka inayofuatia; Scholes sasa ameondoka, Giggs, Ferdinand, Evra na hata Vidic wanaweza wakafuata nyayo za Paul Scholes misimu ijayo lakini bado kuna wachezaji chipukizi ndani ya Old Trafford ambao wanaonekana kuwa hatma nzuri ndani ya timu.
Swali kwa Moyes, je Moyes na United wanamhitaji Rooney? Ferguson amesema kwamba Rooney mwenye uwezo wa 100% angecheza kila dakika lakini bado siwezi kuacha kufikiria kwamba ooney hatoweza kufia uwezo wake kwa 100% akiwa ndani ya United na Ferguson anajua hili. Uhusiano wake na klabu kwa ujumla wakiwemo mashabiki umefikia pabaya. Maombi mawili ya kutaka kuondoka ndani ya miaka mitatu inaonyesha hali hali ilivyo.
Angeweza kuendelea kukaa na kuwa gwiji wa klabu ilivyo kwa akina Scholes au Giggs, au pia angeweza kuvunja rekodi hata ya Bobby Charlton ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu na kujitengenezea ufalme ndani ya klabu kubwa kabisa duniani. Lakini uweledi mdogo wa Rooney ambao hauvumiliki ndani ya klabu ya aina ya United utamuondoa ndani ya klabu hiyo. Ameshapewa nafasi nyingi za kuwa mchezaji mwenye uelwedi ambaye United wanahitaji lakini ameshindwa. Hali ilivyo sasa kidogo inafanana na ilivyokuwa miaka ya mwisho ya David Beckham ndani ya Old Trafford.

United ni kubwa kuliko mchezaji yoyote na Ferguson ameonyesha hilo miaka yote akiwatimua bila huruma wachezaji kama Ince, Keane, Stam, Beckham na Van Nistelrooy. United
waliendelea kupata mafanikio wakati wachezaji wakiwa hawapo na hakuna mashaka kwamba United wataendelea kufanya vizuri bila Rooney.
Ni bora zaidi kama ataondoka Old Trafford wakati huu. Moyes atataka kuja kwenye klabu bila kuwepo kwa msongamano wa habari na tetesi zinamhusu mchezaji mmoja kuliko timu yake kwa ujumla. Moyes anahitaji kumwambia Rooney hatoweza kumpa Rooney nafasi anayoitaka ndani ya timu. Kiukweli mfumo wa Van Persie/Kagawa unatoa ishara nzuri zaidi kwa mafanikio ya timu huku Welbeck na Hernandez wakitafuata muda zaidi wa kucheza, Rooney kubaki kutafanya mambo yazidi kuwa magumu kwa Moyes.

Ni muda wa kukiri kwamba muda wa Rooney ndani ya United umefikia mwisho. Tena inawezekana amekaa kwa muda mrefu zaidi ilivyotakiwa. Lakini kabla ya msimu huu United wamekuwa wakimhitaji zaidi Rooney lakini sasa umuhimu huo umepungua. Hii inanikumbusha sakata la Ronaldinho na Barcelona mwaka 2008, alikuwa na misimu miwili ya nyuma ambayo alianza kupoteza fomu yake na ubora na Guardiola alijua kwamba ili kuendelea mbele ingebidi mbrazili huyo aondoke. Ni vigumu kuacha kuona ufanano wa suala hili la Rooney na Ronaldinho.
Wapi ataenda? United hawatomuuza kwa timu ya kiingereza, Man United sio Arsenal. Na kuwa mkweli kabisa ada ya uhamisho wa Rooney na mshahara wake unaweza ukaziondoa timu nyingi kwenye mbio za kumsaini ndio maana sitoshangazwa kumuona akijiunga aidha Madrid au PSG msimu ujao.
Nilisemaga msimu uliopita Rooney anahitaji kuondoka United kwa maendeleo yake binafsi kama mchezaji kwa kuwa mmoja ya wachezaji watatu wa kiwango cha juu duniani. Ingeweza kuwa uamuzi mzuri ambao angeweza kuufanya, pia uamuzi huo ungemsaidia yeye kukua kama mchezaji na kuisadia timu yake ya taifa ya England.
United watatengeneza fedha nzuri kwa biashara ya Rooney na kuondokana na mzigo wa kulipa zaidi ya £200,000 ya mshahara. Ni jambo zuri kwa pande zote. Wote wamesaidiana na kufanikiwa katika maisha yao ya pamoja lakini bado ilivyo kwa mahusiano mengine inabidi ujue wakati wa kuachana.
No comments:
Post a Comment