Wiki kadhaa baada ya shirikisho la soka duniani kutuma ujumbe wake kuja kufuatilia suala la uchaguzi mkuu wa TFF uliogubikwa na matukio kadhaa ya utata, leo hii shirikisho hilo la soka duniani limetoa maamuzi ya mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa TFF kuanza upya, kwa maana wale wagombea wote waliokatwa wanaweza kurudi kwenye mchakato wa uchaguzi.
Taarifa nilizonazo FIFA imeshatuma barua ya kuelezea uamuzi kwa TFF na muda mchache ujao TFF inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo wa FIFA.
Kwa taarifa zaidi kuhusu suala hili endelea kutembelea www.shaffihdauda.com
Justice has been saved bila ya kuleta mgogangano wa taasisi. Nadhani sasa Watanzania wanaelewa maana ya Tenga kuomba FIFA waje badala ya yeye kutengua maamuzi ya kamati.. Katiba haimruhusu kwani maamuzi ya kamati ya rufaa ni final. Sasa kamati zifanye kazi bila ubabaishaji kwa sababu wanajua wao ndo wenye uamuzi wa mwisho.. wajirekebishe. Mwisho wakati wa kuchagua kamati nadhani watu wawe makini. Kamati nyingi ubabaishaji.
ReplyDeleteMtanzania X
Tunaomba demokrasia itawale, TFF msiturudishe tena kulekule.Mambo ya kuenguana yamepitwa na wakati.Wajieleze then wapiga kura waamue!!
ReplyDeleteKwa katiba ipi?
ReplyDeleteNi vema tukafafanuliwa bayana juu ya Katiba itakayotumika kuendesha mkutano wa marekebisho ya Katiba na mchakato mpya wa Uchaguzi Mkuu.Je nini hatma ya marekebisho ya Katiba ya TFF yaliyofanywa kwa njia ya Waraka?Je Kamati ya Mtinginjola itaendelea kuwepo sambamba na kamati mpya za maadili?Je nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais wab TFF itagombaniwa?Je wajumbe wa mkutano mkuu waliopo sasa ni halali kikatiba na katiba ipi?inahitaji majibu ya makini bila ya kukupurupuka kama kawaida ya wabongo hasa kwenye soka
ReplyDeleteKwa bahat mbaya walio nje ya uongozi wana upeo na uwezo mkubwa wa uongozi japokuwa wengi wao wakiingia nao hupenda kujaza matumbo yao tu....na waliondan ya uongoz wa sasa wengi wao ni vilaza na fifa wanalitambua hilo...haiitaj akili nyingi kujua hilo.....
Delete