Haukuwa mchezo mchezo ambao Barcelona walionyesha kiwango kikubwa, lakini Xavi alikuwa na usiku mzuri kuliko: akipiga pasi 96 na zote zikiwa zimewafikia walengwa - kwa maana hakupoteza pasi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Paris St Germain.
Wakatalunya walikuwa kwenye hatari ya kukosa kucheza nusu fainali ya Champions League kwa mara ya 6 mfululizo baada ya kuwa nyuma baada ya dakika 50 ya mchezo huo, lakini wakaweza kurudisha goli dakika ya 71 likifungwa na Pedro.
Wengi watazungumzia kuhusu mabadiliko ya timu baada ya Messi kuingia, lakini ilikuwa ni Xavi aliyekuwa kwenye kiwango akikiongoza kiungo cha Barca kupeleka mashambulizi mbele aliyeleta utofauti mkubwa.
Mhispania huyo mwenye miaka 33, alicheza dakika 90 na kufanikiwa kutopoteza pasi hate moja - na kuweka rekodi mpya ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote.
Xavi aliweza kuipita rekodi ya Javier Zanetti dhidi ya Tottenham aliyoiweka miaka mitatu iliyopita, Emmanuel Eboue anashika nafasi ya taut kwenye list ya wachezaji waliopiga pasi nyingi kwenye mchezo mmoja.
Wakati mhispania akikaribia kutimiza pasi 100, Zanetti na Eboue walipiga pasi 72 na 54 katika me chi zao walizocheza.
Wachezaji waliopiga pasi nyingi bila kupoteza katika Champions League tangu wa 2003/04
Match | Year | Player | Passes |
---|---|---|---|
Barcelona v PSG | 2013 | Xavi | 96 |
Inter vs Tottenham | 2010 | Javier Zanetti | 72 |
FC Porto vs Arsenal | 2006 | Emmanuel Eboue | 54 |
Barcelona vs Stuttgart | 2007 | Lilian Thuram | 50 |
Real Madrid vs Man City | 2012 | Cristiano Ronaldo | 50 |
Braga vs Galatasaray | 2012 | Paulo Vinicius | 48 |
Basel vs Barcelona | 2006 | Martin Caceres | 48 |
Chelsea vs Werder Bremen | 2008 | John Terry | 47 |
FC Porto vs Dynamo Kiev | 2006 | Rolando | 45 |
Roma vs Real Madrid | 2004 | Ivan Helguera | 43 |
Real Madrid vs Dinamo Zagreb | 2011 | Sergio Ramos | 43 |
Je ilikuwa ni sahihi kwa Messi kuchezeshwa jana????!!! kwa sababu kama ulimufuatilia vizuri hakuwa mtu wa kujiamini sana, alikuwa anauoga ktk kukata mbuga kama kawaida yake siku zote! u know why???!!
ReplyDelete