KLABU ya Azam FC imetoa 'Go Ahead' kwa Simba kwenda mahakamani kwa madai ya fidia ya kuchafuliwa.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria vikao vya bunge kuwa klabu yake inaandaa barua ya kuidai fidia ya Sh1.5 Bilioni.
Ni kutokana na klabu ya Azam kuwafungia wachezaji wanne kwa tuhuma za kupokea rushwa ambayo ni Sh7 milioni ili wapange matokeo wakati wa mechi ya Simba na Azam FC Oktoba 26, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.
Kauli ya Rage inafuatia taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) ikieleza kushindwa kuthibitisha tuhuma za kupokea rushwa zilizokuwa ziwawakabili wachezaji wanne wa Azam, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Deogratius Mushi na Said Mourad.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassoro Idrisa alisema kuwa, klabu yake haiwezi kuzuia kusudio la Simba
"Kama Simba inataka kwenda mahakamani ni sawa hatuwezi kuwazuia kwani ni haki ya kila moja isipokuwa ninachoweza kusema tupo tayari tukihitajika.
"Azam ina wanasheria ambao watakwenda kukutana nao kwa ajili ya mapambano ya kisheria na huko ndiko tunakapowasilisha hoja zetu,".alisema Idrisa.
Awali, Rage alisema kuwa tayari ameshawasiliana na mwanasheria wa klabu yake baada ya kupata nakala ya hukumu iliyotolewa na Takukuru alisema kuwa klabu yake imefikia uamuzi huo kutokana na kudhalilishwa kwa muda mrefu tangu uongozi wa Azam ulipotangaza kuwafungia wachezaji hao.
Rage huwa una idea nzuri sana sema siasa ndo zinakuharibu coz leo waweza sisitiza jambo lenye mantiki kubwa halafu kesho ukaamka na jingne! Kwa mara ya kwanza naungana nawewe kuhusu kudhalilishwa kwako na hawa Azam.
ReplyDeleteAden utaaibika usione mahakama itakubeba kama ilivyofanya takukuro utafungwa azam wako makini sana, shauriyako simba hatumo nenda mahakamani kwa jina lako sio simba
ReplyDeleteRage unajua fika rushwa ilivyo katika soka hapa bongo na kwenda mahakamani sawa ila hoja una na fidia unayotaka ni kubwa mno mbona hamna kipato cha namna hiyo au ndio pakutokea hapa.
ReplyDeleteUkitumia busara hakuna haja ya kwenda huko utapoteza muda na yapo mengi wanachama wako wanataka uwafanyie yenye tija zaidi.
Rage badala ya kushukuru kesi ya jinai haikufunguliwa mahakamani anakurupuka kama kawaida yake kutaka kuwapumbaza wanachama watiifu kwake wa simba.Hapa aelewe kuwa TAKUKURU siyo mahakama na hivyo haina mamlaka ya kuwasafisha wahusika wa kesi hii,once ukipatikana ushahidi wanaweza kuanzisha upya mchakato huo.
ReplyDeleteHivi nyie mnaosema Rage amekurupuka mna maana gani ?
ReplyDeleteHamuoni kama Azam walihatarisha maisha ya Simba?
Hivi leo hii Azam wangeshinda tuhuma na kuonekana Simba wametoa hongo je kungekuwa tena na Simba?
Azam wanastahili kudaiwa fidia hii sheria ipo dunia nzima ndio mana Watanzania mnadhulumiwa haki zenu kwa sababu ya uhoga wenu mtu unajua kabisa kuwa kitu ni haki yako unaogopa kufuatilia kisa kuna fulani badilikeni jamani.
Hivi kwanza huyu Rage ameshamaliza mapumziko aliyopewa na Daktari baada ya oparesheni ya pili ya mgongo kule India?maana alijitonesha mgongo kule Dodoma siku ile alipokuwa anagombania mlingoti wa bendera na vijana wa Chadema, YEYE PEKE YAKE NDIYO ALIKUWA MZEE.Au kwa vile ameona DILI la fedha ikabidi akurupuke?Hii kesi siyo ya Simba ni ya Nyoni,Morris,Mourad na Dida hawa ndio waliotuhumiwa na ndio waliochafuliwa majina yao kwa kutuhumiwa kupokea rushwa katika mechi baina ya Azam na Simba,sasa sio lazima Simba SC ndiyo iwe iliwahonga hizo hela au Simba SC ndiyo iliyokuwa imeshtakiwa TAKUKURU?.
ReplyDelete