Joto la pambano la kugombea kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya ndani ya dimba la Santiago Bernebau linazidi kupamba moto, na Real Madrid wanaingia kwenye mechi hii wakiwa ndio timu iliyocheza robo fainali nyingi kuliko timu zote kwenye historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya - wakicheza mara 30, na sasa wapo kwenye pambano la kuweza kucheza nusu fainali yao ya 24 katika historia yao ndani ya Champions league.
Sio tu Madrid watakuwa wanapewa sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki wao wanaofikia 80,000 kwenye mechi hii ya kwanza, lakini pia namba zinawapa nafasi Los Blancos: timu hii ikiongozwa na Jose Mourinho imeenda miezi 14 bila kupoteza mechi kwenye dimba lao la nyumbani kwenye michuano ya ulaya. Lakini bado haitakuwa rahisi, Galatasary, wakiwa wanaongoza ligi ya Uturuki wamekuwa na rekodi ya kushinda mechi tatu za ugenini kwenye Champions league.
SAFARI YA TIMU ZOTE KUELEKEA ROBO FAINALI | |||
Real Madrid | Galatasaray | ||
Round | Match | Round | Match |
Group D | R. Madrid 3-2 M. City | Group H | M. United 1-0 Galatasaray |
Ajax 1-4 R. Madrid | Galatasaray 0-2 Braga | ||
B. Dortmund 2-1 R. Madrid | Galatasaray 1-1 Cluj | ||
R. Madrid 2-2 B. Dortmund | Cluj 1-3 Galatasaray | ||
M. City 1-1 R. Madrid | Galatasaray 1-0 M. United | ||
R. Madrid 4-1 Ajax | Braga 1-2 Galatasaray | ||
1/8 (first leg) | R. Madrid 1-1 M. United | 1/8 (first leg) | Galatasaray 1-1 Schalke |
1/8 (second leg) | M. United 1-2 R. Madrid | 1/8 (second leg) | Schalke 2-3 Galatasaray |
Real Madrid imekuwa na rekodi ya kucheza nusu fainali tangu Jose Mourinho alipojiunga na klabu hiyo, Mourinho, ameweza kushinda mechi 13, amepata suluhu mbili na kufungwa mechi 1 katika 16 za mwisho alizoiongoza Real Madrid kwenye UCL. Cristiano Ronaldo amefunga kwenye mechi tatu mfululizo alizoichezea Madrid kwenye ligi ya mbingwa, leo atakutana na mturuki Burak Yilmaz, ambaye kwa pamoja na Lionel Messi wote wana mabao nane kwenye michuano ya ulaya msimu huu.
MECHI ZA NYUMA KATI YA REAL MADRID NA GALATASARAY KWENYE CHAMPIONS LEAGUE | |||
Season | Round | Result | |
2000/01 |
Quarterfinals (first leg) | Galatasaray 3-2 Real Madrid | |
Quarterfinals (second leg) | Real Madrid 3-0 Galatasaray |
No comments:
Post a Comment