Real Madrid imekubaliana mkataba wa miaka minne wa udhamini wa jezi zao ambao watawafanya kampuni ya Emirates kuweka logo yao kwenye jezi ya mabingwa hao wa kihistoria wa Champions League, gazeti la Marca linaripoti.
Gazeti hilo limeripoti kwamba mkataba huo utasainiwa rasmi tarehe 30 mwezi huu na utakuwa na thamani ya Euro 24 million mpaka Euro 26 mill kwa mwaka. Madrid na Emirates tayari wana mkataba wa udhamini wa kampuni hiyo ya ndege kuwa wadhaini rasmi wa usafiri wa anga, mkataba ambao ulisainiwa mwaka 2011 ambao una thamani ya Euro 5mil kwa mwaka.
Mkataba wa udhamini wa jezi wa sasa wa Los Blancos na Bwin unaisha mwishoni mwa msimu huu na ulikuwa na thamani ya Euro 23mil kwa mwaka. Kampuni hiyo ya kamari imekuwa wadhamini wa jez za Madrid tangu mwaka 2007 na Marca wanaripoti kwamba uhusiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili utaendelea lakini sasa Bwin watakuwa wadhamini wa pili.
No comments:
Post a Comment