Search This Blog

Tuesday, April 9, 2013

REAL MADRID NA BARCELONA: MATANGAZO YA TV NDIO MSINGI MKUU WA UTAJIRI WAO UNAOIWEKA HATARINI LA LIGA

Kwanini Real Madrid na Barcelona wanapata mapato makubwa kuliko timu yoyote ya ligi kuu ya Uingereza?Jibu lipo kwenye namna wanavyouza haki zao za matangazo ya Television kwenye ligi ya nyumbani kwao.

Mfumo wa ligi kuu ya Spain unawaruhusu kuweza kujadiliana wao binafsi juu ya mikataba yao na makampuni ya matangazo ya TV. Wakati kwenye nchi nyingine nyingi dili za mauzo ya haki za matangazo ya TV zinakuwa zinasimamiwa na ligi yenyewe husika wanayocheza, na fedha zinazopatikana kupitia mkataba husika zinagawanya kwa kufuata makubaliano yaliyokubaliwa.

Kama washindi wa English Premier League, Manchester United walipokea kiasi cha £52m kutokana na mgawanyo wa mapato ya haki za matangazo ya TV kwenye 2008/9.
Real Madrid - wakiwa nafasi ya pili walipata fedha mara mbili zaidi ya walichopata United kwa kuwa na mkataba wa wa kuuza haki za matangazo ya biashara na kampuni ya Mediapro.

Kwa mujibu wa kampuni ya Deloitte, Real Madrid na Barcelona wote wana mikataba na Mediapro mpaka kufikia 2012/13 ambayo itawaingizia kilo timu kiasi kisichopungua 150m euros ($203m; £136m) kwa mwaka.

Kutokuwepo na usawa
Nchini England mgawanyo wa fedha za matangazo ya television hayana usawa, lakini timu hazipishani sana tofauti na nchini Spain.
Kwa mfano, Manchester City, ambao walikuwa wameshika nafasi ya 10 msimu wa 2008/9 walipokea kiasi cha £40m - wakipitwa kiasi cha £12m na mabingwa Man United.
Na njia hii ya kugawanya fedha hizi imezisaidia timu 7 za ligi kuu ya England kuwemo kwenye listi ya vilabu tajiri 20 duniani. Spain inaingiza timu mbili tu kwenye listi hiyo - huku 18 zilizobaki zikiwa zinaogelea kwenye wimbi la madeni. 

Uwepo wa mgawanyo wa mapato usiopishana sana unasaidia katika kuifanya ligi kuwa ya ushindani zaidi.

Ndio maana ligi ya England imekuwa ikipata wapenzi wengi kutokana na ushindani uliopo ndani ya ligi hiyo tofauti ligi ya Hispania.

Hatari iliyopo
Huku suala la haki za kimataifa za mauzo ya matangazo ya TV likizidi kupata umuhimu mkubwa kama chanzo kikubwa cha mapato huku ligi zikigombania watazamaji duniani kote, mfumo wa ligi ya Hispania unakuwa kwenye hatari zaidi. Tumeshuhudia vilabu kadhaa vilivyokuwa vikitamba miaka kadhaa barani ulaya vikitokea La Liga sasa vimepotea huku vikiwa vina madeni makubwa kiasi cha kufikia kufilisika. Valencia, Deportivo La Coruna, Atletico Madrid, Mallorca, Sevilla na vingine kibao vipo kwenye lindi la madeni huku Real Madrid na Barcelona wakiogelea kwenye dimbwi la utajiri wa fedha ambazo nyingi sana zinatokea kwenye mapato ya matangazo ya TV.

Katika mbio za muda mrefu, mgawanyo wa mapato ya matangazo ya TV unasaidia sana vile vilabu vyenye hali dhaifu ya kiuchumi na kuifanya ligi iwe ya ushindani na yenye kufurahisha kuitazama. 

No comments:

Post a Comment