Search This Blog

Monday, April 22, 2013

PEPE KUWA MAKINI: UWANJA WA DORTMUND UNA SELO MAALUM KWA WAFANYA VURUGU UWANJANI

 

Huku Real Madrid wakikutana na Borussia Dortmund katika nusu fainali ya Champions League, Gazeti la Marca liliamua kufanya tour katika makao makuu ya klabu hiyo ya Ujermani ili kujifunza vitu vingi kuhusu mpinzani huyo wa Madrid kuelekea fainali ya UCL. Kitu cha kuvutia zaidi walichogundua katika eneo uliopo uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo - ni selo mbili zilizowekwa maalum kwa ajili ya wafanya vurugu uwanjani hapo.

Kutoka Marca:
Moja ya vitu vya kuvutia kwenye uwanja wa Dortmund kipo kaskazini mwa uwanja huo, ambapo mita 15 kutoka kwenye kwenye majukwaa kuna kituo kidogo cha polisi chenye selo mbili - moja kwa mashabiki wa nyumbani na nyingine kwa kwa mashabiki wa ya ugenini. "Tumetengeneza selo mbili kwa sababu ya kuepeusha balaa baina ya mashabiki wanaopingana," MARCA waliambia na mtoa melekezo wa uwanja huo.
Kila chumba cha selo kina uwezo wa kuifadhi watu 130, pia vyumba hivyo vimewekewa vizuizi vya sauti ili kuhakikisha wanaoshikiliwa hapo wanakuwa wanaipata adhabu vilivyo wakikosa hata namna ya kusikia kinachoendelea ndani ya uwanja.

Sasa wachezaji wakorofi kama Pepep wajiangalie kesho wasije wakatupwa selo ikiwa wataleta uhuni wao ndani ya uwanja.

No comments:

Post a Comment