Kinda la kihispaniola Pedro alijiunga na timu ya kwanza ya Barca mwaka 2008/09, na tangu wakati ameifungia Barca mabao 66. Lakini tofauti sana wenzie mtoto huyu kutoka visiwa vya Canary amekuwa akifunga mabao sana kwa klabu hiyo ya Catalunya.
Goli la hivi karibuni la Pedro lilikuwa kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya PSG. Barca wakiwa nyuma kwa goli moja lilofungwa na Javier Pastore, watoto wa Paris walikuwa wakielekea kufuzu, lakini akapokea pasi nzuri kutoka Villa na kufunga goli muhimu liloipeleka Barcelona nusu fainali.
Katika fainali ya 2009 European
Supercup, Pedro RodrĂguez alifunga goli pekee na la ushindi kwa Barcelona zikiwa zimebakia dakika 5 tu za muda wa ziada baada ya dakika 90 za kawaida.
Msimu huo aliendelea na kufunga mabao 23, goli muhimu zaidi lilikuja
December 19 wakati Barca walipokuwa wamekutana na Estudiantes katika fainali ya klabu bingwa ya dunia. Huku ikiwa imebaki dakika 1 mpira kuisha, Waargentina wakiwa mbelel kwa bao 1-0, Pedro akawarudisha Barca mchezoni klabla ya Messi kufunga bao la ushindi baadae.
Msimu wa 2010/11 ulikuwa mzuri sana kwake, mwezi May Barcelona walikutana na mahasimu wao Real Madrid katika nusu fainali ya Champions League. Wakiwa wameshashinda 2-0
kule Bernabéu, Pedro akafunga bao katika mechi ya pili na mchezo ukaisha kwa sare ya 1-1, Barca wakaenda Wembley. Na katika fainali wakakutana na Manchester United, Pedro akaendeleza tabia yake ya kufunga mabao kwenye mechi muhimu - akiwanyamazisha waingereza waliojazana kuishangilia timu yao ya United, na mchezo ukaishia kwa Barca kushinda 3-1.
Pedro hakuishia huko, alirudi nyumbani kwenye fainali ya Copa del Rey dhidi ya Athletic Bilbao, Pedro akafunga mabao mawili kwenye dakika 25 za mwanzo kuitengenezea Barca mwanzo mzuri na kushinda fainali hiyo kwa 3-1.
No comments:
Post a Comment