Kuna nafasi tunaweza tukashuhudia El Classico kwenye fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kwenye dimba la Wembley baada ya Real Madrid na Barcelona kutengenishwa kwenye droo ya nusu fainali iliyofanyika muda mchache uliopita jijini Geneva Uswis.
Kikosi cha Jose
Mourinho Real Madrid kimepangwa kucheza dhidi ya Borussia Dortmund wakati
Barcelona wamepangwa kucheza na Bayern Munich, hivyo kumaanisha kwamba ikiwa wapinzani wa ligi mbili tofauti - Spain na Ujerumani wanaweza kukutana kwenye fainali ya Wembley May 25.
Dortmund ndio timu pekee ambayo haijapoteza mechi hata moja kwenye michuano hii, na watacheza na Real kwa mara pili ndani ya msimu huu wa UCL. Dortmund waliweza kushinda na kuongoza kundi gumu lilokuwa likihusisha timu za Real, Manchester
City na Ajax.
Mabingwa wa sasa wanaosubiri kuvikwa taji tu la Bundesliga Bayern
Munich wapo kwenye form ya kutisha msimu huu, wakitoka kuikanyaga Juventus nyumbani na ugenini.
Mechi za kwanza za nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya zitachezwa April 23 na April 24, na marudiano zitafanyika wiki inayofuatia tarehe April 30 na May 1.
Wakati kwa upande wa UEROPA LEAGUE - Chelsea wamepangwa na FC Basel wakati Fenerbahce watakipiga na Benfica
No comments:
Post a Comment