Search This Blog

Sunday, April 14, 2013

NDANI YA UKUMBI WA MALKIA NI NGUMU KUTAMBUA NI NANI ATAKUA BWANA HARUSI WA BINTI MREMBO WA KIFARANSA.


21 April 1926 alizaliwa binti mmoja mrembo katika nchi ya Uingereza. Binti huyo mtoto wa Prince Albert alipendwa sana katika jumba la ufalme. Ilimchukua miaka 26 kua malkia wa Uingereza na kiongozi wa jumuiya ya madola.licha ya sifa nyingi za malkia huyo mrembo kuu ni muumini wa mchezo wa mpira wa miguu.Malkia huyu alisimamia kidete ujenzi wa uwanja mpya wa wembley.Malkia huyo anatamani siku moja arsenal icheze kwenye uwanja wake wa wembley,Hicho ndo kitu pekee malkia anachokiota kwenye soka.Pole sana malkia watoto wako wamebarehe ila hawajapevuka kuoa.Nashukuru kwa kuwaachia ukumbi mashababi walopevuka labda watakupa kadi ya kua mgeni rasmi.May mwaka huu ndani ya ukumbi huo mashuhuri kutakuwa na harusi kuu ya mwaka.Baba wa kifaransa mzee platin ameshamtanguliza binti yake mpendwa jijini London bila kufahamika kwa bwana harusi na best man wake.Borrusia Dortmund,real Madrid,Barcelona, na Bayern munich nani kua bwana harusi na yupi angalau atapata nafasi ya kua best man?

Huku howard webb akijiandaa kupewa shavu la kuwa mshereheshaji (mc) wa sherehe hiyo tuanze kuangalia nani ana nafasi gani ya kuwa bosi katika sherehe hiyo? Bila kusahau vijana wote walishawai kumiliki mwanamwali kama huyo apo kabla.

Borrussia Dortmund. Mabingwa wa ulaya mwaka 1997,bingwa mtetezi wa Germany bundesliga.unataka soka safi la kitabuni? Hapa ndo nyumbani kwake.Ikiongozwa na viungo wadogo,waongo Mario gotze na marco reus huku babu mkongwe wa kipoland jakub blaszczykowiski akisimama nyuma yao,hapo ndipo mourinnho na kina khedira wake wanapoishiwa nguvu.Uwanja wa signal iduna ni mara chache sana timu pinzani zinatoka salama.Vinara hao wa kijerumani wanaolingia sana safu yao ya kiungo watapambana na real Madrid katika nusu fainali ya kwanza ndani ya signal iduna uwanja unaoingiza washabiki zaidi ya watu 80,000.hii si mara ya kwanza real Madrid kukutana msimu huu. Timu hizi hapo awali zilikutana kwenye kundi la kifo , na katika mechi hizo Dortmund alishinda mechi moja na sare mya 1-1 kwenye uwanja wa bernabeu.kwa uwezo wa timu ina uwezo wa kuchukua ndoo hiyo japo inapewa nafasi ya mwisho.

Real Madrid. Mabingwa wa kihistoria wa klabu bingwa ulaya.Hawa ndo mababa wa klabu bingwa ulaya japo wana ukame wa kufika fainali na kuchukua kombe hili.Los blancos wana sababu tatu kuu ya kuchukua kombe hili.Kwanza ni kurudisha heshima ya klabu iliyopotea kwa muda mrefu,Pili jose morinho anataka kua kocha wa kwanza kuchukua champions league akiwa na timu tatu tofauti, la tatu ni Kwa mreno christiano Ronaldo,Mreno huyu akibeba kombe hili itakuwa karata dume kwake kutawazwa kua mchezaji bora wa dunia na kumpiku mpinzani wake leonel messi. Real Madrid wana nafasi kubwa ya kuchukua kombe hili licha ya kukabiliwa na mtihani mgumu kwa borrusia Dortmund.Usikose mechi hii ujionee vita ya Kijerumani kati kati ya uwanja.Huku gotze na reus,kule ozil na khedira.

Bayern munich.Kama kuliwa na niliwe tu nipo pamoja na vijana wa karl Heinz rummenigge.ndani ya miaka mitatu ilopita imecheza fainali mbili,ikicheza fainali hii itaweka rekodi ya kucheza fainali tatu ndani ya miaka mine. Mwaka huu timu imefungwa mechi moja tu dhidi ya arsenal.hawa ndo wajerumani halisi.hii ndo timu pekee ilokamilika kila idara kuanzia kipa mpaka washambuliaji.mabingwa mara nne wa klabu bingwa ulaya wana kila sababu ya kujipoza na machungu ya kufungwa na Chelsea katika uwanja wao wa alianz arena kwenye fainali ya kombe hili mwaka jana.nawapa nafasi kubwa Bayern wa kuchukua kombe hili baada ya kuitoa miamba ya soka barani ulaya Arsenal na juventus.

Barcelona.Unataka kula hela ya muhindi? Weka alama ya ndio kwa Barcelona.ikichagizwa na viungo bora duniani kwa sasa andres iniesta na xavi hernandez bila kumsahau mchezaji bora wa dunia leo messi anayekamilisha utatu mtakatifu, inaifanya timu hii kuwa tishio duniani.Barcelona pia itafurahia urejeo wa kocha wao tito vilanova.napata mashaka sana na beki mbovu na dhaifu ya Barcelona mbele ya washambuliaji hatari kama madzukic,Ronaldo na lewandoski.kama Barcelona hawatachukua kombe au kufika fainali basi utakua uzembe wa beki zake.



UTABIRI WANGU


Fainali

BARCELONA Vs REAL MADRID 80%

BAYERN MUNICH Vs REAL MADRID 80%

BARCELONA Vs DORTMUND 55%

BAYERN MUNICH Vs DORTMUND 50%

UBINGWA

BARYERN 0.35

MADRID 0.3

BARCELONA 0.3

DORTMUND 0.05

BY KAIJAGE Jr


Middle ya juu

5 comments:

  1. Ha ha ha ha ha! Mpira wa miguu huccmua sana pale matokeo yanapokuwa kinyume na matarajio ya wengi, mm mzigo wangu namdhamini Bayern Munich!

    ReplyDelete
  2. kaka...
    B. Munich vs Madrid > final hiyo with confidence 0.99, hiyo o.o1 iliyobaki ni kwa sababu no one is perfect.

    ReplyDelete
  3. Daaah yani iyo ya gotze reus vs ozil khedira AIBU kaka!.,but karata yangu bado kwa kina ozil na jembe ronaldo.,,Barca mpaka apo kashatoka,.final bayern vs madrid.,Bingwa Madrid..Halla madrid

    ReplyDelete