Bechi la ufundi la Timu ya Market Fc leo dhidi ya Kilwa Fc likionekana lenye faraja kubwa, (Market Fc 6-Kilwa Fc 0)Bechi la Ufundi la Timu ya Kilwa Fc wakifuatilia mchezo kwa makini, (Market Fc 6 – Kilwa Fc 0)
Wachezaji wa Market Fc wakishangilia moja ya magoli yao leo hii dhidi ya Kilwa Fc (Market Fc 6 – Kilwa Fc 0)
Na: Fungwa K, Lindi
Leo Ligi daraja la Tatu Mjini Lindi iliendelea ikiwa ni Mechi ya Tatu ikiwakutanisha Market Fc ya mjini lindi na Kilwa Fc ya wilayani Kilwa Mkoani Lindi, Hapo jana Mechi zilizochezwa ilikuwa ni Beach Boys ikiikaribisha Kusini Soccer zote zikiwa ni za mjini Lindi na hadi mwisho wa Mchezo Kusini Soccer ilitoka Kifua mbele kwa magoli 2 – 1.
Market Fc leo ikionesha Kandanda Safi imejikusanyia Point tatu muhimu mara baada ya kupoteza mchezo wake wa awali baada ya kukubali kichapo cha magoli 4 – 1 dhidi ya Kariakoo Fc, Leo hii imeitundika Kilwa Fc Magoli 6 – 0. Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kiliisha kwa Market Fc kutoka kifuambele kwa goli 3-0, wafungaji wakiwa ni Mustafa Makacha 18dk, Yahaya Mkweche 36dk, Mohamedi Salumu 43.Kilwa Fc walianza kipindi cha pili kwa kufanyamabadiliko kidogo sehemu ya kiungo lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwani Mlinda mlango wao alionyesha udhaifu mkubwa na kuruhusu Magoli ya Kizembe.
Ni Idrisa Benedict alieendeleza wimbi la magoli kwa timu yake kwa kufunga goli la nne mnamo dakika ya 56, dakika 65 Yahaya Mkweche Kwa maraya pili alimchungulia golikipa huyo na kuandika goli la nne kwa timu yake ya Market, huku yeye akiweza kuonngeza idadi ya magoli mnamo dakika ya 73 kwa kufunga harttrick yake ya kwanza katika mashindano haya. Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa Market Fc 6 - Kilwa Fc 0. Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa kuzikutanisha Kariakoo Fc Vs Kusini Soccer katika uwanja wa Ilulu, mchezo huo unatarajia Kuanza mnamo saa 10:00 jioni.
KATIKA PICHA UWANJA WA ILULU: MPIRA HAKUKOSI VIOJA HEBU ANGALIA....
No comments:
Post a Comment