Manchester City waliweza ushindi kwenye derby na kurudisha matumaini hafifu ya kuutetea ubingwa wao wa Premier League. Sio tu City waliweza kurudisha kisasi cha kufungwa 2-3 kwenye me chi ya kwanza bali pia walipunguza pengo la point kutoka 15 mpaka 12 kwenye derby ya 165.
Huu ni uchambuzi wa kiufundi katika kile kilichotokea Theater of Dreams usiku wa Jumatatu.
Kipindi cha Kwanza
Mechi ilianza kwa timu zote zikishambuliana, huku Man City wakionekana kuwa kwenye kiwango bora kama msimu uliopita. Pamoja na kutokuona goli hate moja kipindi cha kwanza, ilionekana wazi kwamba United bado walikuwa wana kumbukumbu mbaya ya kipigo kutoka kwa Chelsea siku ya jumatatu ya Pasaka, pia ilionekana wazi Robin Van Persie na Patrice Evra walikuwa na uchovu wa me chi za kimataifa - hawakuwa wakicheza kwa kiwango cha 100%. Tangu walipoenda kwenye timu zao za taifa wawili hawa wamekuwa kwenye kiwango kibovu. Pamoja na kuanza vizuri msimu, Robin van Persie amepata mkosi unaomsumbua Fernando Torres, akicheza mechi 11 bila kufunga goli. Patrice Evra alikuwa na kiwango kibovu dhidi ya Chelsea, na kiwango alichoonyesha dhidi ya majirani zao hakikuwa na afadhali kabisa.
Sir Alex Ferguson, sio kwa mara ya kwanza, alimtumia Danny Welbeck kama winga - nafasi ambayo inamfanya Welbeck apogee - pia lilikuwa ni kosa ambalo Manchester United liliwagharimu kwa kiasi kikubwa. Labda sara Fergie anaweza kufahamu umuhimu wa kumchezsha mchezaji nafasi yake anayopaswa.
Matukio kadhaa ya picha hapo chini kutoka kwenye kipindi cha kwanza yanaonyesha namna gani City walivyocheza kwa kujiamini. Safu ya ulinzi ya United kwa hakika haikucheza vizuri, huku Phil Jones pamoja na kupambana vilivyo lakini alikuwa ndio sababu ya mabao ya City.
Picha ya hapo chini inaonyesha Ashley Young akiwa hayupo kabisa katika kuisadia safu ya ulinzi akimuacha Patrice Evra akiwa hana msaada akipigwa mande na James Milner and David Silva.
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha pili yalipatikana mabao matatu, wakati United waliyafanya mambo yakawa magumu upande kwa uzembe wao na mwishowe Manchester City wakaondoka na ushindi wa mabao mawili kwa mona.
Bao la James Milner ( 51′)
Ukiangalia hip picha hapo juu, unaweza ukaona vita viwili. Kwanza, tunaona City wakielekeza miili yao kwenye goli la United, huku wakiwa wamepewa nafasi kubwa na walinzi wa United, na kutokuwepo kwa Rafael kwenye ukuta wa watt wanna nyuma kunamuacha Gareth Barry nafasi ya kutosha ya kuingia ndani ya eneo la hatari, kosa la Ryan Giggs likaleta balaa hili. Michael Carrick amempoteza mtu aliyepaswa kumlinda na Silva anakuwa yupo huru kuingi ndani, Phil Jones ndio alikuwa mtu pekee aliyekuwa akifanya kazi aliyopewa kumlinda Carlos Tevez.
Hapa, unaona namna City walivyojipanga, na inarudisha lie kumbukumbu ya 6-1 msimu uliopita. Unamuona Evra akiwa amemuacha Milner na kwenda ndani ya eneo lao la hatari.
Kutokana kutokukabwa Milner anapata nafasi ya kukutana na mpira unaorudi na anapiga shuti kali linaloenda kuipa City bao la kuongoza.
Bao la Vincent Kompany (og) ( 58′)
The comeback kings wakajitahidi kujaribu kurudisha goli na wakafanikiwa huku Kompany akiusindikiza mpira wa kichwa wa Phil Jones ndani ya lango lao. United walitumia vizuri faulo ya Van Persie iliyompita Joe Hart na kuweza kusawazisha goli.
Bao la Sergio Aguero (78′)
Akitokea benchi kutokana na kuwa na kwa muda mrefu kwa majeruhi, Kun Aguero aliingia kuchukua nafasi ya Samir Nasri na akamlipa mocha wake kwa imani juu yake kwa kufunga goli zuri na la ushindi kwa timu yake.
Picha ya hapo juu, kwa mara nyingine, United wakaacha nafasi kubwa kwa maadui zao. Hapa unaona, Ashley Young akiwa hana ufahamu juu ya kuchomoka kwa Gael Clichy nyuma take. Inaonyesha kadri safu ya ulinzi ilivyojitahidi kumkaba Tevez, jambo ambalo liliwapa wachezaji wengine wa City nafasi ya kusogea mbele na kutengeneza nafasi. Pia unaona ushahidi mwingine kwamba David Silva na Sergio Aguero wakiwa huru kabisa.
Picha ya chini inaonyesha sababu ya City kutumia fedha nyingi kumsaini Aguero, kijana huyu wa Argentina pamoja ukuta wa watu wanne, anaconda mbele na kuwapita na hatimaye anafunga bao.
No comments:
Post a Comment