Search This Blog

Monday, April 29, 2013

MAKAMPUNI 12 YATHIBITISHA KUSHIRIKI SPORTS BAR & SPORTS XTRA DAY BONANZA CHINI YA UDHAMINI WA VODACOM NA NMB



TIMU 12 za makampuni zimethibitisha kushiriki bonanza la soka la Mei Mosi lijulikanalo kama Sports Bar & Sports Xtra Day litakalofanyika Mei Mosi mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mratibu Shaffih Dauda kutoka waandaaji wa bonanza hilo, Clouds Media Group, alisema timu 12 ndizo zilizothibitisha kushiriki bonanza hilo ambalo ni maalum kwa kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi duniani.

“Tunashukuru jumla ya timu 12 zimethibitisha kushiriki bonanza la Sports Bar & Sports Xtra Day litakalofanyika siku ya Mei Mosi mwaka huu, nadhani huu ni mwanzo mzuri na timu nyingine zinakaribishwa kuja kushiriki.

“Lengo la bonanza hili ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa kampuni mbalimbali ili waweze kufahamiana na pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao,” alisema Dauda.

Dauda alisema timu nyingine zinakaribishwa kushiriki bonanza hilo na zinaweza kuwasiliana na waandaaji kwa maelekezo zaidi.

“Wanaotaka kushiriki au kudhamini wanaweza kuwasiliana na waandaaji muda wowote na watapewa masharti ya kushiriki bonanza hili,” alisema Dauda.

Alizitaja timu zilizothibitisha ushiriki wao ni pamoja na, NMB, CRDB, Vodacom, Tanesco, TCC, Fastjet, Infinity Communication, DHL, Simba Net, TBL,NHC na Clouds Media.

Katika bonanza hilo litakaloanza saa 3:00 asubuhi hadi jioni, burudani itapambwa na bendi ya Sky Lite na kundi la Nyumba ya Vipaji Tanzania (Tanzania House of Talents- THT).

Hadi sasa bonanza la Sports Bar & Sports Xtra Day limedhaminiwa na Benki ya NMB na kampuni ya utoaji huduma ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.

1 comment:

  1. Shaffih acha unazi wako kwa Yanga umezidi mno. Yanga wamefunga goli siku ya mechi na jkt ruvu, kila siku unatuonesha falsafa ya soka la kiholanzi lakini simba wamefunga goli la kiufundi jana dhidi ya polisi moro unajifanya kama huna habari nalo badala yake unatuletea bongo movie,hebu niambie wana jipya gani ktk soka la bongo

    ReplyDelete