Search This Blog

Wednesday, April 17, 2013

MAENDELEO YA SOKA LA TANZANIA YAKO MIKONONI MWA NANI?

Ukizungumzia soka hapa nchini Tanzania unaweza kupata kigugumizi kidogo kutoka na na hali halisi iliopo katika shirikisho la mchezo huo hasa kwa kipindi hiki ambacho utandawazi umekua na muamko kwenye mchezo huo nao umekua kwa kasi kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma. Watu wengi wamekua na maoni mbalimbali kuhusu maendeleo ya soka letu hasa pale ambapo mgogoro ulipoibuka kuhusiana na uchaguzi wa shirikisho hilo (TFF) miezi michache iliyopita. Hii nikutokana na kile wengi walicho kiita ‘madudu’ yaliofanywa na baadhi ya kamati za shirikisho hilo wakati wa kuwachuja  wagombea watakao ingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo.

 Watu wengi wakiwemo waandishi wa habari za michezo katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini  waliliongelea swala hili kwa hisia na kwa nguvu nyingi ili kufanya walichokiita ‘kuliokoa soka la Tanzania’ . Hii ilitokana na kamati izo kuwatoa wagombea wengi kwenye uchaguzi huo kwa vigezo ambavyo wengi hawakukubaliana navyo ikiwemo serikali kupitia Wizara ya habari utamaduni na michezo. Kamati ya rufaa ya TFF, pamoja na kamati nyingine za TFF zilisikiliza mapingamizi yaliofikishwa mbele yao dhidi ya baadhi ya wagombea walio chukua fomu ya kugombea na fasi mbalimbali za uongozi kwenye shirikisho hilo na kufikia hufikia maamuzi ya kuwasimamisha baadhi ya wagombea kuendelea na mcakato huo.

Kikubwa kilicholeta mgogoro ni kutokana na baadhi ya vigezo ambavyo waliviweka ikiwa ni pamoja na wagombea ilikua ni lazima wawe wameukubali waraka wa kubadilisha katiba ya TFF waraka ambao vyama vingi vya mikoa viliukataa kitu ambacho kimewafanya wagombea wengi kutolewa nje ya kinya’anyiro hicho. Waraka huo ulikua wa kubadilisha katiba ambao ulipingwa kwa kutofuata utaratibu wa kubadilisha katiba kama katiba ya mwanzo ilivyokua inaeleza. Kigezo hicho kilitumika kumuengua mgombea mmoja ambaye katika uchaguzi uliopita alishiriki na kukosa kwa wingi wa kura dhidi ya mpinzani wake aliyeko madarakani hivi sasa ikiwa bado uwepo wake ni kinyume na katiba kwani muda wake umeshapita.

Kuna wagombea wengine wametolewa kwa kigezo cha kutoifahamu katiba ya TFF kikamilifu kitu ambacho pia kililalamikiwa na baadhi ya wadau wa mchezo huu hapa nchini. Walisema sii kwamba wagombea hao hawaijui katiba ila ni kwamba hawajaikariri kifungu kimoja kimoja kitu ambacho pia kiliwaengua baadhi ya wagombea.

Kingine kilichowaengua ilikua ni pamoja na uzoefu katika shirikisho. Mgombea alitakiwa awe na uzoefu wa miaka mitano katika chama kitu ambacho pia kilizungumziwa sana na wadau kutokana na upotoshwaji wake katika mchakato mzima.







Baada ya mgogoro huo serikali haikukaa kimya nayo ikaibuka na kusema yake ili kupunguza ukali wa mgogoro huo ambao ulionekana kama ungeigharimu nchi yetu kwa upande huu wa soka. Serikali iliwataka wasimamishe shughuli nzima ya uchaguzi waite mkutano mkuu wa kubadilisha katiba na wasitumie katiba mpya watumaie ya zamani hadi hapo katiba hiyo itakapo kua imepitishwa kihalali.
Tamko hilo la serikali  lilionekana kuleta matumaini kwa wadau wengi wa soka hapa nchini kwakua  iliwataka  TFF nao kufika ofisini kwao (wizarani) kuongea nao na kuwaelekeza cha kufanya ili kilinusuru soka letu. Walitoa siku ambazo TFF iwe imeshafika ofisini kwao lakini ujumbe hou wa serikali kwa TFF ukawa umeingiliwa na kupunguzwa makali na Shirikisho la mpira wa miguu dudiani FIFA kuingilia kati na kusema ni kinyume na katiba yao kwa serikali kuingilia shughuli za chama chochote cha mpira kitu ambacho adhabu yake ni kufungiwa kucheza michezo ya kimataifa kwa kipindi kisicho julikana.

Habari hii ilivyotufikia watanzania wengi tulishtuka na wengine tukaanza kupeana lawama wenyewe. Serikali ilijitetea kupitia kwa naibu waziri wa michezo na TFF nao wasema yao kupitia kwa afisa habari wao na mgogoro kuonekana kama unataka kuchukua sura mpya. Ndipo FIFA wakatoa agizo la kulifuatilia swala hili hadi sasa tunasubiria kauli kutoka kwao.


  JE NANI WA KULIOKOA SOKA LETU?

Kiukweli si jukumu la FIFA kuja kutusaidia uchaguzi wa chama cha mpira wetu kwa sababu tunauwezo wa kufanya hivyo. Uwezo huo uko kwangu mimi na wewe lakini hadi tunafikia kwenye hali hii ni wazi kuwa kuna watu wana masilahi binafsi katika sekta hii. La sivyo leo tungeshakua na viongozi wapya katika shirikisho letu. Watanzania tunalipenda soka letu lakini hatujui wajibu wetu katika kuliendeleza, hii ni kwasababu mchango wetu mkubwa umekua ni kukosoa na kulaumu kuliko kutoa mawazo endelevu katika kuliendeleza. TFF nao wanatuchukulia sisi sijui kama nini wakati wao ni wawakilishi wetu pale kutokana na kwamba wote tusingetoshea pale kwenye zile ofisi za TFF kufanya kazi za kundeleza mpira wetu kwa hiyo tukaamua kuweka wawakilishi.

Wawakilishi hao sasa wamegeuka na kuweka masilahi yao mbele na kuishia kutumia kivuli cha FIFA kujilinda kitu ambacho kinaonesha kuwa hata FIFA nao wanahusika katika kuua soka letu. Hii ni kwa sababu serikali ilipotaka kurekebisha madudu ndani ya TFF wenyewe walitoa taarifa kwa FIFA kuishtaki serikali kuwa ina waingilia na kusingizia vyombo vya habari na basi hata wao wanahusika kupitia kwa afisa habari wao.

Rais wa TFF tunaamini ni msomi na ni mwanasoka lakini kwamwenendo anaoelekea nao ni wazi kuwa anajidhalilisha na kuwaaibisha wale walio mpigia kura kwa imani zote kwakua yeye angetakiwa kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi ili kutusaidia sisi kupata kiongozi bora ambaye atafanya kitu kitakacho kuwa msaada kwa kizazi kijacho cha soka.



Tunachotakiwa watanzania nikuamua kua na kauli moja ya kumtaka rais anayemaliza muda wake kutumia elimu na uzoefu wake kujaribu kuleta muafaka ambao hauta tegemea FIFA kuhusu jambo hili haraka iwezekanavyo ili kutoa fursa kwa watu wengine wenye mawazo endelevu na soka letu waliendeleze kuliko kuendelea na migogoro isiyo na tija yenye muonekano wa kimaslahi kwa kundi la watu flani hasa hao waliopo madarakani kwa sasa.
Inaonekana kuwa hawa viongozi waliopo madarakani wana mpango wao unaowanufaisha ndo maana wanajaribu kila wawezalo kuweka watu ambao hata likitokea la kutokea watakua safe.

Ni jukumu letu watanzania kuendelza soka letu na sio kuwategemea FIFA wakati sisi wenyewe tuna mawazo na akili zakuzaliwa na zakusoma  zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli kutokana na uzalendo ambao tutautumia wakati wa kutoa mawazo hayo. Tofauti na FIFA sisi tunaweza kutoa mawazo ambayo yatasaidia na vizazi vijavyo na pia tutazingatia hali halisi ya maisha yetu ya kitanzania ambayo yatakua suluisho lakudumu la maendeleo ya mpira wetu.

Cha msingi TFF sasa igeukie upande wetu na kubadilisha uhusiano wetu kwao kutokana na hali ilivyo sasa ambapo uhusiano si mzuri sana ili tuangalie tulikwama wapi na tufanye nini ili tusifikie pabaya zaidi ya hapa wakati kuna vipaji vipya vya soka vinakuja kwa kasi sana ukilinganaisha na miaka ya nyuma.

hesabu                         TFF+FIFA = KIFO SOKA LA BONGO
                                    SERIKALI

Hiyo ndo hali halisi ya soka la Tanzania na suluisho ni sisi wenyewe tuamue kuunda vikundi vya kuliokoa soka letu vitakavyo ishurutisha TFF na serikali kulitatua hili swala na kuiambia FIFA ukweli kua inazuia mabadiliko katika soka letu na kuendeleza ukiritimba uliopo TFF unaotufanya tushindwe kushiriki hata kombe la mataifa ya afrika kwa kuendelea kuwakingia kifua wanaoturudisha nyuma kimaendeleo katika soka letu.


   Prepare by:
   Urio Innocent W.

5 comments:

  1. Bwana Urio nadhaniupo nyuma ya wakati sana. Hayo maoni yako yamekuja wakati ambao tayari FIFA wameshakuja na kuanza kazi! Acha FIFA waje wakate mzizi wa fitina. Sioni sababu ya juanza kuweweseka na kujipendekeza kwa upande wowote ule. Tunahitaji independent party kutatua hili suala kwani kuna muingiliano wa masilahi wa waziwazi. Nadhani waote tunajua kuna wagombea wanafungamana na wanakamati wa TFF na pia wapo ambao ni swahiba wa serikali hasa mmoja wapo wa kigogo wizarani. Na jinsi matukio yalivyo hata waandishi wa habari pia wanaegemea kwenye baadhi ya kambi za wagombea. Acha waje FIFA waamue tujue mbivu na mbichi! wala tusianze kuweweseka na kuanza kujifanya tunaweza kutatua migogoro wakati tuna unafiki na kukosa weledi katika maamuzi yetu.

    ReplyDelete
  2. Mumeshajua kilichoamuliwa na fifa nini, sifikirii kama fifa wamekuja kutuamulia cha kufanya, maneno ya haya ndio ya shaffii toka mwanzo. Namuheshimu sana huyu jamaa lakini kwa hili la uchaguzi yupo bias, ana mtu ila hataki kuwa wazi, anajificha kwenye kivuli cha uanaharakati. Tuambieni matokeo ya fifa na sio kutuandaa kupinga matokeo hayo.

    ReplyDelete
  3. NAPENDA KUUNGA MKONO HOJA KWA ASILIMIA MIA MOJA KUWA SOKA LETU WENYE DHAMANA YA KULIOKOA NI SISI WENYEWE SIYO FIFA WALA NINI..NA NI KWELI MASLAHI YA WATU BINAFSI NDIYO YAMETUFIKISHA HAPA TULIPO.

    KAKA SHAFII NAOMBA KUBORESHA FOMULA YAKO ISOMEKE IFUATAVYO.....

    (TFF + SERIKALI)/ FIFA * 100 = KIFO SOKA LA BONGO

    HAPO NIMEBADILI IWE TFF+SERILAI KWAKUWA WAO NDIYO WATU WA KARIBU NA TUNAGAWANYA NA MCHANGO WA FIFA ZIDISHA KWA MIA ILI TUJUE KUWA MCHANGO WA KILA MMOJA HAPO (TFF, SERIAKALI NA FIFA) TUKIURANK THEN TUKAWEKA KATIKA HII FOMULA NA KUTAFUTA ASILIMIA KWA KUZIDISHA NA MIA NDIYO TUTAJUA HALI HALI YA KIFO CHA SOKA KATIKA HILI...

    SERIKALI IMEUNDA TUME YA KUSAIDIA STARS ISHINDE MBONA TFF HAWAJALALAMIKA KUINGILIWA....? AU KOCHA WA TIMU YA TAIFA ANAPOLIPWA NA SERIKALI MBONA TFF HAWALALAMIKI KUINGILIWA...TENA KIPINDI KILE JK ALIPOMLETA MAXIMO TOKA BRAZILI MBONA HAWAKUSEMA WAMEINGILIA....?

    ReplyDelete
  4. Someni vizuri hadi mwisho jamani aliyeandika haya makala si Shaffih ni Urio Innocent W.ameweka na email yake hapo(Hii ni kwale wanaomshambulia Prof.Shaffih.)

    Nirudi kwenye Mada-Wa kuokoa soka letu ni sisi wenyewe.Napendekeza muda kuongoza TFF uwe miaka miwili tu(uwe umechaguliwa kwa kura au umeajiriwa) na hakuna kuongeza muda hata kama bado 'unapendwa.Haya mambo ya kukaa TFF miaka 8 kama wanasiasa ndiyo yanawafanya hawa akina Tenga wanabadilika na kuwa na tamaa(ubinafsi)

    Mdau David V

    ReplyDelete
  5. Hivi waliokwenda FIFA kuomba ije kutuamulia si Malinzi na Wambura?sasa badala ya kuwalaumu Malinzi na Wambura tunamlaumu Tenga,huu ni upuuzi.Tenga alishandaa uchaguzi ambao unazingatia Kanuni na ulipangwa kufanyika tarehe 24 februari,wale wenye sifa wakapita wale wasio na sifa hawakupitishwa,ndio hao wamesababisha Tenga aendelee kuwepo madarakani leo.Tusidanganyane ,hawa wanaonunua waandishi wa habari na wanaotumia nguvu na fedha nyingi kutaka madaraka ya TFF ndio watakuwa wagumu kweli kuachia madaraka muda wao utakapomalizika kwani hawana maslahi na soka bali kuitumia soka kuingia kwenye siasa.Wambura ni mtu wa kriketi na Malinzi ni mtu wa ngumi wanang'ang'ania nini kwenye soka?

    ReplyDelete