Search This Blog

Thursday, April 11, 2013

LIG KUU BARA, WANA TAMTAM WAKABWA, PRISONS WANG`ARA, POLISI WAJIHATARISHA ZAIDI!


Na Baraka Mpenja
Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea kushika kasi kwa mechi tatu kushuhudiwa katika miji ya Mbeya na Morogoro.
Maafande wa jeshi la magereza, Tanzania Prisons wameshuka dimbani kuwakaribisha Mgambo JKT  katika uwanja wa Sokonne. Dakika tisini za mchezo huo zimemalizika kwa Prisons kuwabamiza wageni wao  bao  1-0.
Akizungumza kwa furaha nyingi kutoka jijini humo, katibu mkuu wa Prisons, Sadick Jumbe, amesema bao pekee la ushindi limefungwa na nyota wao Nurdin Issa Chona.
Jumbe alisema ushindi wa leo ni faraja kubwa kwa mashabiki wa soka mkoani humo, na sasa wanapanga upya majeshi yao kuwakaribisha Ruvu Shooting ya mkaoni Pwani, mchezo utakaopigwa jumamosi ya wiki hii jijini humo.
Pia aliongeza kuwa leo hii uwanja ulifurika mashabiki wengi sana ambao wameishangilia timu hiyo kwa muda wote wa mchezo, na kama itakuwa hivyo mechi zilizosalia lazima wapate ushindi.
Kwa upande wa Mgambo JKT kupitia kwa katibu mkuu wake, Antony Mgaya, wamesema matokeo ya leo ni mabaya sana kwao na yameathiri hesabu zao za kupambana kushuka daraja.
Mgaya alisema soka ni matokeo matatu, kufunga, kufungwa na kutoa sare, leo wamefungwa, basi wanapiga hesabu za michezo inayofuata.
Mkoani Morogoro katika dimba la Jamhuri, Polisi Moro wameshindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimisha suluhu pacha ya bila kufungana na maafande wa jesi la kujenga taifa, Ruvu Shooting kutoka mkaoni Pwani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Clemence Banzo amesema wameyapokea matokeo ya leo kwa shingo upande kwani mechi inayofuata wanakutana na mabingwa watetezi, wekundu wa Msimbazi ambao kwa sasa wanahitaji kupata ushindi.
Banzo alisema kushindwa kuibuka na ushinid katika mchezo wa leo, kumewafanya wazidi kujihatarisha zaidi na mstari wa kushuka daraja.
Kwa upande wa Ruvu Shooting kupitia kwa afisa habari wake Masau Bwire, wamesema wamepokea matokeo hayo kwani pointi moja ugenini si haba.
Masau alisema ingawa wameshindwa kufanya vizuri leo, lakini maamuzi ya waamuzi wa leo yamechangia kuwanyima ushindi.
Mbali na mchezo huo, huko mashamba ya miwa ya Manungu, wana tamtam Mtibwa sugar wameshindwa kupata ushindi baada ya kukabwa koo na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya vijana wa mitaa ya kishamapanda Mwanza, Toto Africa.
Afisa habari wa Mtibwa, Tobias Kifaru Lugalambwike, amesema mabao ya Mtibwa yamefungwa dakika ya tatu na John Ndanda, na dakika ya 17 Hassan Banda alipachika bao la pili kwa mkwaju wa penati.
Kifaru alisema kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi huku vijana wa Toto wakicheza soka safi na katika dakika 74 Mohamed Hussein aliandika kimiani bao la kwanza la kusawazisha, na dakika ya 87 nyota huyo aliisawazishia klabu yake bao la pili.
Afisa habari huyo alisema mchezo wa leo umeharibiwa na hali ya mvua iliyonyesha  asubuhi na kuharibu hali ya uwanja Manungu Complex uliokumbwa na utelezi.
Baada ya mitanange ya jana, ligi hiyo itaandelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa dimba la Chamazi, Azam fc watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Africa Lyon.


No comments:

Post a Comment