Equatorial Guinea wapo kweye hatari ya kuvuliwa ushindi wao wa 4-3 dhidi ya Cape Verde katika michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 kwa kumchezesha mchezaji ambaye hakupaswa kuichezea nchi hiyo.
Shirikisho la soka duniani mpaka sasa halijataja jina la mchezaji husika ambaye hakupaswa kuichezea nchi hiyo.
Wakati wachezaji wote kikosi kinachoanza cha Equatorial Guinea hakuna hata mmoja aliyezaliwa ndani ya nchi hiyo - zipo sheria na kanuni zinazowaruhusu wachezaji hao kuiwakilisha nchi yao.
Kwa mujibu wa Andiko 17 la shirkisho la soka duniani, mchezaji anayepaswa kuichezea nchi fulani inabidi atimize japo moja ya masharti yafuatayo:
- Awe amezaliwa ndani ya mipaka ya nchi iliyopo chama cha soka husika.
- Wazazi wake wa damu, aidha mama au baba awe amezaliwa ndani ya nchi husika.
- Babu yake au bibi yake awe amezaliwa ndani ya nchi husika.
- Awe ameishi mfululizo kwa miaka mitano au zaidi ndani ya nchi husika baada ya kutimiza miaka 18.
Fifa inasisitiza "nchi wanachama na vyama vya soka ndio wenye jukumu la kujiridisha kama masharti yametimizwa."
Burkina Faso , Gabon na Sudan wote wameshapokonywa pointi kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia 2014 kwa kuchezesha wachezaji ambao walikuwa hawapaswi kucheza mechi kutokana na sababu mbalimbali.
Equatorial Guinea kwa sasa wapo nafasi ya 3 kwenye kundi B la kugombea kwenda Brazil 2014 nyuma ya vinara Tunisia, ambao wameshinda mechi zote tatu mpaka sasa
Katika kesi inayofanana na hii ya sasa, mwaka 2011, FIFA waliizuia timu ya wanawake ya Equatorial Guinea kushiriki kwenye mashindano ya kufuzu kucheza Olimpiki na kumfungia mshambuliaji Jade Boho Sayo kwa miezi miwili kutokana na masuala ya kutokuwa na uraia halali wa kuitumikia nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment