Search This Blog

Tuesday, April 2, 2013

BARCA VS PSG: WACATALUNYA HAWAJAFUNGWA KATIKA ROBO YA FAINALI TANGU 2003 - PSG HAWAPOTEZA MECHI KWAO KWA MIAKA 7

Mchezo wa robo fainali wa ligi ya mabingwa wa ulaya kati ya PSG-FCB unatoa namba ya takwimu nyingi za kuvutia baina ya klabu hizi mbili kama zinavyoelezewa hapo chini:

• Mechi ya leo Jumanne itakuwa mechi ya nne inayozikutanisha timu hizi mbili katika michuano ya ulaya. PSG walishinda 2-1 kwenye robo fainali ya 1993-4 ya Champions League  wakati wakitoa suluhu ya moja moja pale Camp Nou katika mechi ya kwanza na katika fainali ya kombe la washindi mwaka 1997 Barca ilishinda 1-0.

• Timu hizi mbili pia zilikutana kwenye mechi ya kirafiki August 4th 2012 kwenye dimba la Parc des Princes mchezo ukaishia kwa matokeo ya suluhu ya 2-2.

• Barça imecheza dhidi ya timu za Ufaransa mara 15, wakishinda mara 9, na kutoa suluhu na kushinda mara tatu tatu. Nchini Ufaransa, wameshinda mara tatu, wamefungwa mara mbili na kutoa suluhu mara mbili.

• PSG wamezifunga timu za La Liga mara 9, wamefungwa mara 5 na kutoa suluhu mara 4, lakini wamefungwa mara moja kwenye dimb lao la nyumbani na timu kutoka kwenye La Liga.

• Ingawa hii mara ya pili kwa PSG kucheza kwenye robo fainali, hawajafungwa nyumbani kwao kwenye michuano ya ulaya tangu mwaka 2006 November, walipofungwa Hapoel Tel-Aviv 2-4 katika  UEFA Cup. Kwenye michezo 23 tangu wakati huo, hawajafungwa.

Barça wameshinda mechi zao zote za robo fainali ya Champions League, mara ya mwisho kufungwa kwenye robo fainali ilikuwa msimu wa 2002/03 dhidi ya Juventus.

• Barça watakutana na wachezaji wake wawili wa zamani mjini Paris - Maxwell na Ibrahimovic, mwingine, Motta ni majeruhi.

• Mara ya mwisho Barça ilipocheza rasmi ya mashindano nchini Ufaransa ilikuwa mwaka 2006, walipoifunga Arsenal 2-1 katika Champions League final kwenye dimba la Saint-Denis.


• Kwa wachezaji saba wa Barca -Valdés, Piqué, Busquets, Xavi, Iniesta, Cesc na Villa - huu watakuwa mchezo wao wa pili ndani ya siku ya saba jijini Paris, baada ya kuhusika kwenye na mchezo wa Spain dhidi ya Ufaransa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment