YAYA TOURE: HIZI NDIO NJIA YA KUTAWALA DIMBA LA KATI
Know when to stick or twist
Don’t be too forceful with your challenges
Doing light weights will keep you light
Barbell squats and box jumps
Know when to stick or twist
Yaya Toure anaelezea siri ya mafanikio yake kwenye kutawala nafasi ya kiungo kwa kutumia nguvu, kujipanga na namna ya kutoa pasi
Kujipanga
“Nikiwa Barcelona, nilianza kwenye nafasi ya kiungo na nilimaliza kwenye nafasi hiyo hiyo. Hawakunihataji niende mbele. Kazi yangu ilikuwa kutawala nafasi ya kiungo, kunyang'anya mpira kutoka kwa adui na kuigawa kwa mchezangu mwenzangu.I started in midfield and finished in midfield. Nilipaswa kuifanya kazi hiyo kwa muda muafaka, ingawa inabidi nifanye lolote ili kutengeneza nafasi kubwa. Ukiona nafasi ifuate, ikiwa hakuna tengeneza ulinzi wa nafasi yako na toa pasi. Haupaswi kwenda mbele tu ili mradi umeenda. Muda mwingine ni vizuri kufanya hivyo lakini muda mwingine inabidi utumie uwelevu wako vizuri na kutoa pasi kwa haraka.”
Tumia nguvu lakini kucheza madhambi
“Inabidi uwe mwangalifu sana ukiangalia ni nani unakabiliana nae. Wakati unapopambana na wapinzani imara, labda unaweza ukawalazimisha kutenda madhambi, sio kwa vurugu lakini inabidi utumie nguvu. Lakini kwa wachezaji wafupi, wepesi, inabidi uwe mwangalifu zaidi. Inabidi usubiri, na kukabiliana nae huku ukiwa mwangalifu kutokutumia nguvu sana. Ni rahisi sana kupewa kadi siku hizi. Pia kuna ukweli kwamba kuna wanakuwa wanakutegemea hivyo unapopata kadi nyekundu ya moja kwa moja , unakuwa unawaletea ugumu usiohitajika kwa upande wao."
Jenga mwili gym
“Makocha wa viungo ndio watu muhimu zaidi kwangu klabuni; wananisaidia kuuweka mwili wangu vizuri, kitu ambacho ni muhimu kwa kazi yangu ya uwanjani. Nafanya mazoezi ya kila kiungo changu kila siku; mikono na miguu, mgongo, mabega - na vingine muhimu. Lakini jambo muhimu sio vizuri kubeba vitu vizito sana, ila inabidi nibebe vitu vyepesi kiasi mara nyingi sana. Huwa nafanya marudi zaidi ya mara 10 au 12 inategemea na zoezi, lakini sizidishi sana, kwa sababu sitakiwi kuwa mzito uwanjani. Uzito mwepesi unamaanisha unakuwa mwepesi uwanjani."
No comments:
Post a Comment