Search This Blog

Thursday, March 14, 2013

TFF YATOA USHAHIDI KUHUSU FIFA KUTISHIA KUIFUNGIA TANZANIA - TENGA AWATAKA WADAU KUWA WATULIVU

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amewataka wadau wa mchezo huo kuwa watulivu kwa vile tofauti zilizojitokeza kati ya Shirikisho na Serikali zitamalizwa kwa taratibu za mpira wa miguu.

Amesema nia ya TFF ni kuhakikisha Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) haliifungii Tanzania kwani tayari Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alishaahidi kuwepo kikao kati yake na viongozi wa TFF kitakachofanyika Jumanne (Machi 19 mwaka huu).

“Suluhu itapatikana kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala hili tutalimaliza baada ya kikao cha Machi 19 ambacho kimepangwa na Waziri kutokana na maombi ya TFF,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tatizo lilianzia kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA.

FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika, na yenyewe kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia suala hilo.

Rais Tenga amesema lisingetokea tatizo hilo, TFF tayari ilishaitisha Mkutano Mkuu ambao ungefuatiwa na uchaguzi. Lakini kwa vile FIFA ndiyo iliyosimamisha mkutano huo, TFF inalazimika kusubiri hadi FIFA itakaposhughulikia suala hilo na kutoa maelekezo ikiwemo lini mkutano ufanyike.

Amesema kwa kuamini tatizo hilo litamalizwa ndani ndiyo maana TFF hadi sasa haijapeleka FIFA maagizo ya Waziri Dk. Fenella ya kutengua marekebisho ya Katiba ya TFF ya mwaka 2012, kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, kwani ingefanya hivyo Tanzania ingefungiwa mara moja.

TFF inasisitiza kuwa FIFA ilijua tatizo la Serikali kutoa maagizo kwake kupitia vyombo vya habari, hivyo kumuandikia Rais Tenga na kueleza msimamo wake iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu.

Uhalali wa kuwepo kwa barua ya FIFA kwenda kwa Rais Tenga juu ya suala hilo ulihojiwa pia na mwandishi wa Reuters, Brian Homewood baada ya kusoma kupitia vyombo vya habari nchini kuwa Shirikisho hilo huenda likaifungia Tanzania ikibainika Serikali inaingilia shughuli za TFF. Mawasiliano kati ya FIFA na mwandishi huyo ambapo majibu yake pia TFF ilipewa nakala yameambatanishwa katika taarifa hii.

BARUA YA FIFA
Dear Brian,

Thanks for your message.

We can confirm that FIFA Secretary General Jérôme Valcke has sent a letter to the President of the Tanzanian Football Federation, Leodegar Tenga, concerning alleged governmental interference in the internal affairs of the TFF.

FIFA is in contact with the TFF President who is optimistic that the matter can be sorted out within TFF, FIFA and the Tanzanian authorities. Furthermore, we can confirm that FIFA is also planning to send a mission to assess the situation with regard to the electoral process as soon as the current matter of alleged interference has been clarified.

Kind regards

FIFA
Media department
Enquiries: media@fifa.org
Twitter: @fifamedia    YouTube/FIFAtv

11 comments:

  1. Tenga ni mpuuzi tu na mtu asiyesoma alama za nyakati,hana jipya tofauti na ufisadi waliokuwa wanafanya ndani ya Tff

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe sio mtanzania mitusi yote hiyo, hivi kweli mna edit comment hizi? Utake usitake serikali ilikurupuka kwa hili, na lazima irudi chini

      Delete
  2. Hapana ndugu mwananchi wewe ndiyo mpuuzi na usiyesoma alama za nyakati Taratibu za masuala ya mpira wa miguu yanajulikan Dunia nzima kua hayahitaji kuingiliwa na selikali katika nchi husika mpaka sasa Tenga amefanya kazi kubwa kwani shirikisho bado linafanya kazi zake kwa amani kabisa huku taratibu zingine zikifuatwa... Mwanachuo TUMAINI UNIVERSITY.

    ReplyDelete
  3. Nyie watu mlisoma na kusoma Tumaini University ndiyo mmetuletea matatizo haya yote mnakitia aibu chuo kuwa kinatoa watu wababaishaji ambao wanaleta uhuni kwenye mpira

    ReplyDelete
  4. Hivi mlitaka tenga aingilie maamuzi ya kamati? Halafu hawa hawa wakina wambura wangesema tenga amevunja katiba.. maana katiba haimruhusu. Si kwamba nawatetea TFF ila kwa hali ilivyokuwa busara ni kuwaita FIFA. Waziri hakushauriwa vizuri. Sasa kwa kufuata katiba ya 2006 mambo yote yaliyofanya kuanzia 2006 yankuwa batili. Huku ni kurudisha nyuma mandeleo ya soka. Wadau wa mpira waelewe mpira ni FIFA na TFFA inawajibika kwa FIFA. Nadhani badala ya kupiga kelele hawa wakina wambura waende FIFA tu. Ningependa sana TFF iendeshwe kiuweledi. Hali ya sasa hairidhishi hasa kwenye kamati kwani kuna mgongano wa maslahi wa wazi ila kama tupo makini tutatambua Tenga alifanya sahihi kulipeleka suala hili FIFA. Narudia tena maamuzi ya ile kamati ni ya mwisho. Hakuana mtu wa TFF angeweza kutengua..

    ReplyDelete
  5. Ndugu wa Tumain serikali wala haikuingilia maamuz ya tff ila imefuta usajili wa hii katiba amby imepitishwa kwa waraka kwasbb katiba inasema mabadiliko ya katiba yataidhinishwa na mkutano mkuu kwhy tenga na watu wake wamekiuka katiba ya tff,fifa na hata serikali.

    ReplyDelete
  6. Hivi mlitaka tenga aingilie maamuzi ya kamati? Halafu hawa hawa wakina wambura wangesema tenga amevunja katiba.. maana katiba haimruhusu. Si kwamba nawatetea TFF ila kwa hali ilivyokuwa busara ni kuwaita FIFA. Waziri hakushauriwa vizuri. Sasa kwa kufuata katiba ya 2006 mambo yote yaliyofanya kuanzia 2006 yankuwa batili. Huku ni kurudisha nyuma mandeleo ya soka. Wadau wa mpira waelewe mpira ni FIFA na TFFA inawajibika kwa FIFA. Nadhani badala ya kupiga kelele hawa wakina wambura waende FIFA tu. Ningependa sana TFF iendeshwe kiuweledi. Hali ya sasa hairidhishi hasa kwenye kamati kwani kuna mgongano wa maslahi wa wazi ila kama tupo makini tutatambua Tenga alifanya sahihi kulipeleka suala hili FIFA. Narudia tena maamuzi ya ile kamati ni ya mwisho. Hakuana mtu wa TFF angeweza kutengua..

    ReplyDelete
  7. wewe ndo kilaza kabisa, hv unadhan TFF bila kulikoroga wenyewe serikali ingewaingilia? Tenga na wenzake ni lazima wakubali walichemka.

    ReplyDelete
  8. kujengaaa nyumbaaa ni kaziii kubwa na inakuchukuaaa muda na recource nyingi sn ila kuibomoaaa ni kazi ya dakika tano kumiiii umemaliza,,,,ndivyo ilivyomtokea kaka yang Tenga,,,,amefanyakazi kubwa kuijega TFF,kujenga jina lake na heshima yake ila ndani ya dakika chache 2 vyote alivyovifanya ni sifuriii,hivi ameshindwa nini kutii amri ya serikali na kuitisha mkutano mkuu wapitishe katiba yao na irudii kwa msajirii mambo yaishe,hadi waamue ku2nishana misuri na serikali...naanza kuamini kua labda Bro hakutakaaa kutokaaa tff so anatengeneza mazingira yakuundelea tff kwa mlango wa nyuma..bro fuata taratibu itisha mkutano wa wawachama watoe maamuzi mpira uchezwe,,,maana hata wewe uko madarakani kimakosaaaaaaaa

    ReplyDelete
  9. Naona sasa mnashindana kwa matusi, tuheshimiane jamani, tutake tusitake ni lazima busara itumike kama tenga anavyotupeleka, hizi hasira hazitasaidia wakubwa huo ndil mpira,jamaa wana dunia yao, ukiwaingilia umekwisha. Ona bratter alivyogombea sasa hayatoj. Ila kuna tetesi wanaltaka tufungiwe eti simba sababu hawana nafasi mwakani, nipeni uhakika wa hilk ila sio kwa mitusi mlioanzisha

    ReplyDelete
  10. kweli nyie watu wa tumaini mnatia aibu wala hujui kitu gani kinaendelea wewe fuata masomo yako mpira tuachie sisi kama wameyakoroga tunyamaze?

    ReplyDelete