Search This Blog

Saturday, March 2, 2013

TENGA: TFF HAITAKIWI KUINGILIWA - WAZIRI AMESHAURIWA VIBAYA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema ipo haja kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kufikiria upya uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya TFF ya mwaka 2012 na kutaka itumike ya mwaka 2006, kwani hautekelezeki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema ni muhimu jambo hilo likaangaliwa upya kwa sababu athari zake ni mbaya, na pengine Dk. Mukangara hakushauriwa vizuri kabla ya kufanya uamuzi huo.

“Kamati ya Utendaji ya TFF haitaki kubishana na Mheshimiwa Waziri hata kidogo, ila tunaamini wakati anatamka haya hakufahamu madhara yake, athari zake na ugumu wa utekelezaji wake. Kwa waliomshauri hili, wamemshauri vibaya,” amesema Rais Tenga.

Amesema rai ya TFF kwa Waziri ni kuwaita ili wamweleze ni kitu gani wafanye kunusuru mpira wa miguu wa Tanzania, kwani wanaamini jambo hili litakwisha baada ya kumwelimisha hasa kutokana na ukweli kuwa kabla ya kufanya uamuzi huo hakuwasikiliza.

Katika mkutano huo, Rais Tenga alianza kwa kusema kuwa TFF inaiheshimu sana Serikali, hivyo inaheshimu maagizo yaliyotolewa na Waziri, lakini akaongeza kuwa TFF ina wajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya maagizo hayo.

Amesema lengo la kuelezea historia ya TFF ilikotoka ni kubaini migongano ya maagizo hayo na taratibu za TFF ambazo kwa bahati mbaya zinasigana na maagizo hayo.

Rais Tenga amesema TFF ni chombo cha wanachama, ambapo wanachama wake ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, na ina taratibu za kufanya uamuzi kwa mujibu wa Katiba yake na za wanachama wake ambazo zimeidhinishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema si TFF pekee, bali vyama vya nchi zote ambavyo vimeunganishwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), zinaheshimu na kufuata maagizo na miongozi ya shirikisho hilo la kimataifa la mpira wa miguu.

Rais Tenga amesema TFF haitakiwi kuingiliwa katika uongozi na uendeshaji wake, kwani jambo hilo likitokea rungu la FIFA litaiangukia TFF, na madhara yake ni makubwa. Miongozo ya FIFA inasisitiza uhuru wa wanachama wake katika uendeshaji shughuli za mpira wa miguu, na iko kwenye Katiba ya TFF.

“Sheria za nchi ndizo zilizozaa Katiba ya TFF. TFF ni chama kamili kinatakiwa kufanya uamuzi wake ili mradi uzingatie madhumuni ya kuanzishwa kwake. Leo TFF ikiacha mpira wa miguu na kuanza kujishughulisha na gofu, hapo Msajili ana haki ya kuingilia,” amesema Rais Tenga.

Kuhusu maagizo ya Waziri, Rais Tenga amesema kifungu cha 11 cha Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kinazungumzia usajili wa chama, na si marekebisho ya katiba, ingawa kanuni zinahusu marekebisho ambapo ameongeza kuwa uamuzi wa marekebisho ni wa Mkutano Mkuu na si Msajili.

“Ukienda kuomba viza, fomu unapewa na yule anayekupa viza. TFF tulipowasilisha marekebisho ya Katiba hatukupewa fomu. Msajili akasema sawa. Jambo la kujaza fomu si la TFF, ndiyo maana tunasema ipo haja ya jambo hili kufikiriwa upya.

“Usajili tayari umepita, kwamba Msajili hakutoa fomu, mwathirika anakuwaje TFF? Tunaona ni muhimu jambo hili likaangaliwa upya,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa utaratibu wa kusajili Katiba ya 2006 ambayo ndiyo Waziri ameagiza itumike ulikuwa huo huo uliosajili Katiba ya 2012.

Akizungumzia historia ya TFF kutoka mikononi mwa BMT, Rais Tenga amesema ni zao za Katiba ya 2004 ambayo ilifanyiwa marekebisho ukumbini na kugongwa mhuri na Msajili hapo hapo na kuingia kwenye uchaguzi. Katiba hiyo ndiyo iliyoiondoa BMT kuisimamia TFF.

“Huko ndiko tulikotoka, si kwa kulazimishwa, bali kwa kupewa Katiba ya 2004. Katiba ina utaratibu mzima wa kufanya uamuzi. Maelekezo ya Waziri yamesahau huko tulikotoka siku nyingi. Uhalali wa marekebisho unatokana na ridhaa ya Mkutano Mkuu. Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba yenyewe, hakuna nafasi ya BMT,” amesema.

Amesema katika maagizo ya Waziri, ameitaka TFF kufuata Katiba ya 2006 na kanuni za BMT, lakini Katiba hiyo hiyo ya 2006 haina nafasi ya BMT, na hata kama TFF ingetaka kutekeleza hilo haliwezekani.

“Kwa maagizo haya inaonekana Waziri kashauriwa vibaya. Tunajua hakuwepo katika nafasi hiyo (2004) wakati wa makubaliano kati ya Serikali na FIFA kuacha mpira wa miguu ujiendeshe wenyewe,” amesema Rais Tenga.

Pia amezungumzia umuhimu wa Katiba toleo la 2012, kwani kuna marekebisho mengi yalifanyika mwaka 2007, 2008, 2009 na 2011 ambapo ukiyafuta maana yake unakiweka pembeni Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Bodi ya Wadhamini, wanachama wapya (mikoa), Bodi ya Ligi, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi, Leseni za Klabu na Kanuni za Fedha.

“Kwa uamuzi huu yote yaliyofanyika hayana maana. Waziri sidhani kama alikuwa anafahamu athari za maagizo yake. Kama angelijua asingefanya uamuzi huo. Si rahisi kurudi katika Katiba ya 2006. Hao wajumbe wa Katiba ya 2006 unawapata wapi? Maana yake hata vyama wanachama ni batili kwa vile vimerekebisha Katiba zao 2009 na 2010,” amesema Rais Tenga.

Amesema kwa Serikali kufuta, maana yake ni kutengua uamuzi wa TFF ambapo madhara yake ni nchi kufungiwa, ambapo timu za Taifa hazitacheza mpira, klabu hazitashiriki michuano ya kimataifa na wadhamini nao watakaa pembeni kwa vile hawawezi kudhamini timu ambazo hazishindani kimataifa.

“Dhana kwamba tukae tu tusicheze nje, ni dhana ya watu walio nje ya mpira wa miguu. Dhamira yetu ni kuhakikisha hatufungiwi. Waziri ametuagiza tupeleke barua FIFA kuwa ametengua marekebisho ya katiba. Hatupeleki hivyo, kwani hiyo ni Government interference, watatufungia.

“Nia yetu bado ni Waziri kutupa nafasi ya kutusikiliza,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa kuhusu uchaguzi kwa vile FIFA wanakuja ombi la TFF kwa Waziri ni kuacha kwanza mchakato uendelee hadi ufike mwisho.

“FIFA wanakuja, tuwasubiri. Nilidhani utaratibu huo utaheshimika. Kama mtu wa mpira haitaki FIFA anataka nini? Ahadi yetu ni kuhakikisha watu wanapewa haki. Hiyo ndiyo ahadi yetu na tumeisimamia, na ndiyo maana FIFA wanakuja,” amesema.

Akijibu swali kuhusu waraka, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba hayakufanywa kwa siri, ridhaa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kufanya marekebisho hayo kwa njia ya waraka ilipatikana ambapo 70 waliunga mkono na 33 walikataa.

15 comments:

  1. Wewe Tenga ndiye umeleta vurugu zote hizi TFF.Huna lolote

    ReplyDelete
  2. NINYI WAANDISHI MUWE WADADISI, ALITAKIWA AULIZWE KIPENGELE CHA KULAZIMISHA UZOEFU WA MIAKA MITANO HAMUONI KAMA NI KUKINZANA NA HAKI ZA BINADAMU KWAMBA HATA HIZO NGAZI ZA CHINI MAANA YAKE HUWEZI KUMPATA MTU MPYA KABISA !! HAMUONI KAMA NI USULTANI AU KWA MAANA HALISI KUWAMILIKISHA WATU FULANI TU AMBAO WAMO HATA KAMA WATAKUWA HAWAFAI,
    PIA NI HATARI GANI ITAPATIKANA KAMA TUKIFUNGIWA KULIKO HUU UTAWALA MBOVU WA KUMILIKISHANA KIJOMBA JOMBA . AU NI FAIDA GANI KWA WATANZANIA AMBAYO WATAJIVUNIA KWA KUENDELEA KUWAMO ILIHALI NI WASINDIKIZAJI DAIMA,KAMA HAMJUI HUU NAO NI UFISADI, TENGA ANAACHA TFF AKIWA NA LENGO LA KUSONGA NGAZI ZA JUU AKIWA ANAJUWA FAIDA ZAKE.
    ACHA TUFUNGIWE ILI TUJIPANGE UPYA !!!!!!!

    ReplyDelete
  3. ni bora kufungiwa kuliko kuona tff inaendeshwa kama Mali ya tenga watanzania tumechoshwa na namna tff inavyoendeshwa

    ReplyDelete
  4. tenga tenga tenga heshima zote zimepotea ondoka tuachie mpira wetu,utaka elimu we mbona unaelimu lakini madudu tuuuuu,acha uzanditi watu wameshakujua nenda kwenye siasa c ndo mnavyotaka kupata umarufu alafu then kuingia kwenye siasa? GO GO GO TUMECHOSHWA NA UBABAISHAJI WENU

    ReplyDelete
  5. MIMI NAONA NI BORA TUFUNGIWE TU KWANZA USHIRIKI WETU NI SAWA NA KUFUNGIWA TU...WADHAMINI WAKIJITOA WACHA WAJITOE ILE TENGA NA WENZAKE TUONE KAMA WATANG'ANG'ANIA HAPO MAANA HIZO PESA ZA WADHAMINI NDIYO ZINAWAFANYA WASITAKE KUTOKA HAPO.......DO U MEAN FIFA WANAINGILIA HATA KATIBA ZA NCHI...TENGA USITUCHANGANYE..NA NINA KUMBUKA SIKU MOJA NILITOA MAONI HAPA KUWA HAWA JAMAAA WANAFANYA MAKUSUDI KWA KISINGIZIO CHA FIFA......WE ARE NOT FOOL AS YOU THINK TENGA ULIINGIA WATU WAKAKUAMINI NA KUKUHESHIMI SO PLEASE LEAVE TFF PEACEFULLY......USIJEMGEE UADUI USIO NA MAANA NA USIKATE KUPOTEZA HESHIMA YAKO NA KUNUNUA DHARAU TOKA KWA WAPENDA SOKA KWA BEI NAFUU....!!

    ReplyDelete
  6. Tenga hana mpya kwa hili tusubiri Rungu tu la FIFA

    ReplyDelete
  7. Tenga swali kwako kama serikali haihusiki kwann mlipeleka katiba kwa msajil wa serikali?Na je FIFA wanaitambua katiba ya TFF bila kupitia kwa msajili?
    Tenga umeenda nje ya point kabisa sisi hayo yote tunayajua madhara ya kufungiwa,swali la msingi katiba uliopitisha kwa walaka ni sahihi?wazir ameangalia katiba yenu na kuona general assembly ndio inabadil katiba na tff hamkufanya mkutano mkuu kwa hyo kisheria sio katiba halari.
    Wewe tenga ndio unatupeleka huko na kama unayajua haya kwann ulifanya kosa la kizembe kama hilu?
    Plz tuliza kichwa......STOP AND THINK......

    ReplyDelete
  8. Nilikuwa namuheshimu sana huyu jamaa, lkn kwa hili anaonekana yeye ndio engineer wa michezo yote michafu kwenye uchaguzi huu. Anaongea kisiasa sana na anakwepa hoja zote za msingi za madudu waliyofanya. Kwanini anakwepa kukiri mapungufu ya mchakato mzima wa uchaguzi na maloloso ya ajabu kabisa ya akina Agape Fue?? Mkutano mkuu gani uliridhia mabadiliko ya katiba kwa mujibu wa katiba ya TFF?? Tamaa na ufisadi wa hizi rogue elements pale TFF zitaharibu mpira wa nchi hii!

    ReplyDelete
  9. Duuh hii kaili, watu wanataka tufungiwe.... sababu malinzi na wambura? hawa fifa si wanakuja? nimesikia watapitia mchakato wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza wadau wa uchaguzi na wagombea waliotemwa, jamani kama hawana sifa kikatiba hata akiwa nani ni lazima atoswe, sasa kama wanazo sifa si watelezwa uoga unatoka wapi? kama mdau wa soka sitaki kusikia kufungiwa na fifa, huu ni ujinga kushabikia hii kitu,kwa maelezo ya waziri kufuta katiba kwa sababu ya kutojaza fomu sijalielewa kabisa. Mi naona waziri ndio kaja kutuvuruga kabisa, ni uamuzi wa ajabu ila umetolewa na watu wale wale ambao hawapo kwenye mpira, JAMANI MPIRA SIO SIMBA, YANGA NA TFF TU, VILABU MITAANI VINAHITAJI VIONGOZI KAMA KINA MALINZI NA WAMBURA, WANGEKUWA VIONGOZI KUANZIA HUKO WASINGEPATA TATIZO LA UZOEFU, MAANA UZOEFU UNATAKA WA MPIRA NA SIO NGAZI KUBWA TU

    ReplyDelete
    Replies
    1. TUNASHUKURU ILA HUJATUAMBIA WEWE AU TAIFA LIMENUFAIKAJE NA MPIRA, KAMA SIO NA WEWE KUWEMO KWENYE KUNDI HILO, HAIWEZEKANI WEWE KATIKA WIZI HUU NA UPOTOSHAJI WA MAKUSUDI, HATA KAMA SIO WATU HAO WAWILI ULIOTAJA KWA SABABU ZAKO MAANA WAKO WENGINE, AMBAO KAMA WEWE MDAU KWELI ILIBIDI PIA UWATAMBUE KWANZA HAO USIO WAJUA NDIO WAMEFUNGUA NA KESI, HUU NI UJINGA VINGIVYO UNATIA MASHAKA KWA KUTETEA MRIJA WAKO USIKATWE

      Delete
  10. tatizo la wachangiaji wengi humu ni wafuasi tu, ni kama mambo yale yale ya simba na yanga. hoja iliyoleta yote haya ni matumizi ya katiba ya mwaka 2012 na utaratibu uliotumika kupata katiba hiyo. kwa kuwa kamati ya uchaguzi ambayo ni chombo huru cha TFF(siyo ile ya rufaa iliyolalamikiwa sana) ilishaona mapungufu ya kikanuni na kusimamisha uchaguzi, tungeanzia hapo nadhani tungetoka salama. vurugu zimekuja baada ya baadhi ya wagombea kwenda kulalamika FIFA, kisha FIFA nayo kusimamisha uchaguzi hadi watakapofanya uchunguzi wao. Cha kushangaza (kwa nchi hii) ni pale ambapo hatua zimeshaanza kuchukuliwa, na kwa jambo lile lile tena waziri wa michezo anatoa amri zake za kuikataa katiba ambayo kimsingi imepitisha na vyombo husika vya TFF. sasa Tenga afuate maagizo ya chombo kipi? yale ya kamati ya uchaguzi (ambacho ni chombo halali kikatiba)? au ya FIFA (ambacho ni chombo halali kirufaa na kikatiba)? au ya serikali (ambacho sio chombo halali kikatiba)?
    nadhani Tenga anavyosema uamuzi wa serikali hautekelezeki ni kwa misingi hiyo ambayo asili yake ni pale ilipozaliwa TFF mwaka 2004.

    ReplyDelete
  11. Watoa maoni wengi hawapendi kuona mpira unakua hata kidogo, mnapenda ushabiki zaidi. Mtu utasemaje eti wacha TUFUNGIWE! This is nonsense, unajua hasara gani wanapata vilabu, wadhamini, wapenda soka, ajira kwa vijana nk?

    Kama unapenda mpira, uelewe kuwa hauendeshwi kisiasa na una taratibu zake. FIFA ndio baba wa mpira utake usitake. Msisahau waliopitisha KATIBA YA TFF ni SERIKALI kupitia msajili wake. Hawa hawa serikali wanasema WALIKOSEA kupitisha!!!? Kama walikosea kupitisha unalaumu TFF na kufuta katiba KIVIPI!!??

    TFF walitangaza utaratibu wa kubadili katiba yake na wote tulisikia. 70% waliapprove na tulitaarifiwa na TFF, na wakasema mabadiliko yamepita na KATIBA itabadilishwa! Hakukuwa na SIRI! Mbona wakati huo msipige kelele? Kukatwa kwa Malinzi hakuhusiani na KATIBA! Naamini atakuwa president mzuri tu, ila hili la katiba katiba na namna serikali ilivyoliendesha, SORRY, wamechemka kabisa!

    Kamati za TFF ziko au ziko supposed to be INDEPENDENt. Kama kuna moja ya kamati imetoa maamuzi tata, kwanini mnamlaumu Tenga!? Tena Tenga huyohuyo amesema anangatuka. Trust me, angeamua kuendelea na Upresident sioni wa kumshinda. Tujivunie huyu bwana kuamua kuachia watu wengine waje na fikra mpya na si kumponda hapa!

    Kama mnapenda soka wacheni lichezwe jamani twende taifa tukafurahi, hakuna sababu ya msingi ya kufungiwa hata kidogo! Mi naona serikali ndio ya kublame hapa...nadhani Makalla ndio tatizo coz yuko zaidi kwenye soccer, mama waziri Fenella nadhani kaingizwa mkenge! TFF na serikali wakae waongee. Actually serikali ingewasummon TFF kabla hata ya kutoa directive ya ajabu kabisa ya kufuta katiba! Shame on govt!

    ReplyDelete
    Replies
    1. wacha TUFUNGIWE! This is nonsense,INAWEZEKANA KAMA WEWE UKIYAJIBU HAYA MAPUNGUFU
      NINYI WAANDISHI MUWE WADADISI, ALITAKIWA AULIZWE KIPENGELE CHA KULAZIMISHA UZOEFU WA MIAKA MITANO HAMUONI KAMA NI KUKINZANA NA HAKI ZA BINADAMU KWAMBA HATA HIZO NGAZI ZA CHINI MAANA YAKE HUWEZI KUMPATA MTU MPYA KABISA !! HAMUONI KAMA NI USULTANI AU KWA MAANA HALISI KUWAMILIKISHA WATU FULANI TU AMBAO WAMO HATA KAMA WATAKUWA HAWAFAI,
      PIA NI HATARI GANI ITAPATIKANA KAMA TUKIFUNGIWA KULIKO HUU UTAWALA MBOVU WA KUMILIKISHANA KIJOMBA JOMBA . AU NI FAIDA GANI KWA WATANZANIA AMBAYO WATAJIVUNIA KWA KUENDELEA KUWAMO ILIHALI NI WASINDIKIZAJI DAIMA,KAMA HAMJUI HUU NAO NI UFISADI, TENGA ANAACHA TFF AKIWA NA LENGO LA KUSONGA NGAZI ZA JUU AKIWA ANAJUWA FAIDA ZAKE.
      ACHA TUFUNGIWE ILI TUJIPANGE UPYA !!!!!!!
      TENGA ASIDANGANYE UMMA, KWAMBA KWA SABABU TFF INAJITEGEMEA NDIO IACHWE IVUNJE KATIBA YA NCHI NA HAKI ZA BINADAMU. YEYE MWENYEWE ANAPASHWA KUHOJIWA NA VYOMBO VYA DOLA ILI KUONA UNDANI WA MAMBO KAMA KUNA KITU ANAFICHA, NA HUU NI UFISADI AMBAO WATANZANI NA VIONGOZI WA VYAMA VY SIASA INA BIDI WAVIKEMEE PIA , HAKI IKO WAPI KWA KUTAKA WENYE UZOEFU, HIYO NI SHERIA AMBAYO HATA NGAZI ZA CHINI PIA INABIDI WAIFUATE LINI UTAPAT MTU MPYA,HII MIZENGWE IACHWE, SERIKALI IMEIFUNGIA MWANAHARISI NA REDIO MBILI NCHINI KWA UCHOCHEZI, SASA KAMA SERIKALI HIYO HIYO INATOA MAELEKEZO KWA CHAMA CHA MPIRA KINA BISHA SASA HII NI HATARI INAMAANA TENGA ANGEKUWA NA JESHI ANGEINGIA MSITUNI. HAIWEZEKANI LAZIMA MAMBO YAFANYIKE KWA MASLAHI YA WATANZANIA BADALA YA KIKUDI CHA WATU WACHACHE HUU NI UFISADI NA WIZI , CAG YUKO WAPI ? SERIKALI IKO SAHIHI ACHA TUFINGIWE KAMA KWELI ANAMAINISHA HIVYO NA YEYE TENGA NDIYE ALIZALISHA HILI NA HISTORI ITAMFUNGA. KWANZA AMEFANYA NINI MPAMOJA NA KUAMINIWA, ASHUKURU WATANZANIA SIJUI NI WAVUMLIVU AU ? IMETOSHA TUFUNGIWE HAMNA FAIDA KUENDELEZA MADUDU.
      NATOA USHAURI YEYE KAMA TENGA AHOJIWE ZAIDI KUANGALIA ANACHOKIFICHA, PIA MKAGUZI WA HESABU ANGALIE URALI WA MATUMIZI YA FEDHA, KUNA VYANZO VINNE AU ZAIDI VYA FEDHA
      1. FIFA WANATOA FEDHA KWA TFF
      2. MAKATO KUTOKA KILA MECHI (WANANYONYA WAVUJA JASHO- WACHEZAJI)
      3. WAFADHIRI WA NDANI WANAOJITOLEA, TAIFA STARS INAPOKUWA NA MECHI
      4. MAKAMPUNI YANACHANGA FEDHA
      5. WADHAMINI WA LIGI WANATOA FEDHA
      HIVI WEWE MTANZANIA MWENZANGU HUYU TENGA AU TFF KWANI WASITILIWE MASHAKA KWAMBA NI WEZI AU KWA MAANA NYEPESI NAO NI MAFISADI, KESHO HATA AKIINGIA KWENYE SIASA UNADHANI ATAFANYA NINI.
      NANYI VIONGOZI WA VYAMA MBALIMBALI PANUWENI UWIGO WENU WA KUTETEA NCHI NA HASA KUNDI LA VIJANA LILOWEKWA REHANI NA TABAKA LA WAJANJA, ANGAZENI SEHEMU ZOTE KWA LENGO LA KUSAIDIA VIJANA KIMAENDELEO. VINGINEVYO MTAONGOZA KWA MIUJIZA IPI MKITEGEMEA KULETA MAENDELEO, MIMI SIAMINI MAANA
      A. MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUWAVYO
      B. UKIPANDA BANGI USITEGEMEE UPATE MCHICHA. N.K
      KUMBE KUNA WATU WANAWEZA KUFANYA MAMBO SAHIHI SIJUI TATIZO LIKO WAPI ? KWA NINI UMWAMWANDAE MTU AWE KIONGOZI PASIPO NA YEYE MWENYEWE KUONYESHA KWA VITENDO KUWA ANAWEZA ? HILI TUSIPO LIANGALIA KWA UMAKINI LITATUPELEKA PABAYA WATANZANIA

      Delete
  12. Tenga yupo kwenye wakati mgumu sana, sijui atarudishaje tena imani ya watanzania kwake!

    ReplyDelete
  13. Mkutano mkuu unafanyika kwa njia ya simu. Minutes au kumbukumbu za kikao unaziandaaje na zinasainiwa vipi na wajumbe. Huu ni upuzi mkubwa wa Tenga au anafikiri TFF ni mali yake

    ReplyDelete