Search This Blog
Monday, March 18, 2013
SIMBA YAJIBU TUHUMA ZA TIMU KUSHINDWA KWENDA KAGERA KWA NDEGE
Nauli ya bei nafuu kabisa kutoka Dar-Luanda-Dar ni dola 1000 kwa kichwa. Simba imekwenda Angola pasipo kutembeza bakuli kwa mtu. Na wote waliosafiri wakalipwa posho kwa USD (si kwa fedha za madafu). Fedha hizo ni mara kumi ya zile ambazo wachezaji walikuwa wakilipwa miaka minne hadi sita iliyopita wakiwa safarini na Simba....
Leo inazushwa kwamba eti Simba haina fedha za kwenda Kagera ndiyo maana inapita Dodoma, Tabora, Shinyanga kucheza ndondo!!!!!! Inachekesha. Gharama ya mafuta, kwa sababu Simba ina basi lake, haifikii hata nauli ya mtu mmoja kwenda Angola... Sasa vije leo isemwe eti Simba haina fedha za kwenda Mwanza? Yaani za kwenda Angola zipo ila za Mwanza hakuna? Kuna sababu kubwa mbili kwanini timu inakwenda Kagera TARATIBU. Mosi, zaidi ya nusu ya wachezaji waliosafiri wanatoka TIMU B na wengine hawajawahi kufundishwa na Patrick Liewig.
Benchi la ufundi liliona ni vema hawa wapate nafasi ya kujaribiwa katika mechi ya kirafiki ili wajue kocha anahitaji nini na kocha awafahamu zaidi wachezaji wake. Ikumbukwe pia, kiufundi, Simba haikutakiwa kuwa na mechi kwa wiki zaidi ya mbili kutokana na ratiba iliyozingatia ushiriki wake kwenye Ligi ya MABINGWA. Hiyo ni sababu ya kiufundi. Kuna sababu ya 2 ambayo ni ya kimantiki. Kwamba Simba ni klabu ya Watanzania wote na si wale walioko Dar es Salaam na mikoa yenye timu za Ligi Kuu. Kuna mikoa kama Tabora ambayo Simba haijacheza kwa takribani miaka 10 lakini wapo Wana Simba ambao wangependa kuiona.
Vivyo hivyo kwa Shinyanga ambapo tulipata sapoti kubwa sana tulipokwenda mwaka jana. Tunahitaji kuwafurahisha wapenzi wetu wa kona zote. Tunahitaji pia kutengeneza fan base kubwa zaidi hata kwa watoto ambao wataiona Simba ikicheza Tabora.... Mwaka jana tulipeleka Kombe letu katika baadhi ya mikoa. Mara baada ya kumalizika kwa ligi msimu huu, tuna mpango wa kwenda kwenye mikoa ambayo Simba haijakwenda kwa miaka mingi... Mikoa kama vile Rukwa, Kigoma, Singida, Mara, Iringa n.k... Jamani huko kote kuna washabiki wa Simba na watafurahi kuiona ikicheza mbele ya macho yao. TUNASUBIRI KWA HAMU pia tuambiwe tunaenda kucheza ndondo wakati huo ! Watu wanafikiri Man United inakwenda China kufanya mazoezi pekee!!!! Hapana, inakwenda kutangaza brand yake ili wapate pa kuuza merchandise yao... Tutakwenda kote itakakowezekana, INSHALLAH... Ili mradi Simba ikianza kufanya biashara huko tuendako, na wakati huo utafika tu, tusianze kuulizana tulimtumia MGANGA gani kufanya biashara ya merchandise yetu vizuri.... Hiki ndicho kile rafiki yangu John Shibuda huwa anakiita kwa maneno mawili tu; FIKRA MCHAKATO....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Big up Simba tupo nyuma yenu mdomdogo tutafika.safari njema kagera nawatakia ushindi vijana wanaweza,hu ni mpito tu tutaseto
ReplyDeleteTumewaelewa simba, ila nadhani sikila hoja niyakujibu tu.
ReplyDeleteTumewaelewa Simba, ila nadhani sikila jambo mnatakiwa kujibu. Lamsingi nipale mnapofanya maamuzi nakuamini niyamsingi
ReplyDeletePorojo tupu, tuangalie hiyo mantiki unayodai. Simba ina wachezaji wa timu ya taifa kama Kiemba, Ngasa, Kaseja, Kapombe nk haiingii akilini uwaburuze kwa bus mpaka Mwanza wakati mwisho wa wiki wana mechi ya kimataifa na Morocco! Hiyo mantiki ya kucheza ndondo za Shinyanga, Tabora na Mwanza inatoka wapi wakati wachezaji hawatakiwi kucheza zaidi ya mechi 2 kwa wiki?
ReplyDeleteSemeni ukweli acheni longo longo simba yetu sote lakini haya mnayoyafanya ni kichekesho sasa
aingii akilini acheni longo longo hicho mnachofanya huwa kinafanyika kujiandaa na msimu na sio ndani ya msimu
ReplyDeleteTatizo ni kuwa watu mnataka matokeo mazuri tu uwanjani!!yanapatikana vp hamjui!! kuna haja gani ya kupanda ndege kwenda huko wakati una muda wa mazoezi mwingi tu na unaweza tumia hiyo jinsi unavyotaka!
ReplyDeletePlani za timu zipo kwa utawala na benchi la ufundi.Wengine nyie ni mashahidi tu. Sasa shahidi unataka nn zaidi ya kusimulia! au unataka na kupanga mipango ya timu inaendeshwaje!! timu nyie endeleeni na utaratibu wa kujenga timu ya vijana. mwakani ishallah watakuwa poa sana.mambo ya majina eti fulani si tija sana,kwani wenye majina wana nn sas hivi!! mbona tunachoka nao mtaani tu.
Mshafulia nyinyi SIMBA. si mkubali kuwa pesa ndio tatizo baada ya matajiri wenu kususa. mtaisoma namba mwaka huu. na namba zenyewe ni T yanga AZAM (itatumika miaka kama kumi kuanzia sasa)
ReplyDeleteSoka la Bongo litakuja kuendelea pale washabiki na waandishi wa habari watakapo acha kuingilia mambo ya kiufundi ya Timu husika na michezo kwa ujumla. Bongo kilamtu fundi... Akisoma gazeti au akisikiliza Redio anajiona fundi. Tena na hizi Ligi za Ulaya ambazo kila mtu anaangalia siku hizi ndio balaa kabisa. Watu tunaposhindwa kujenga hoja za msingi na kukaa kupiga porojo na majungu ndio mwanzo wakuwapa nafasi viongozi kuboronga! Niwajibu wetu kutulia na kujenga Hoja za msingi ili kuwapa changamoto viongozi wetu wajue tunawatu wanaoelewa kinachofanyika na hivyo kuwafanya wafanye mambo kwaumakini! Mi naamini kwa mwanzo huu ambao Club ya Simba imeanza nao kuna mafanikio mbeleni kama hakutatokea mwendawazimu akahalibu huu mfumo wa SIMBA B ambao utatuondolea kasumba la kununua wachezaji ambao wanachama huonekana kudai pesa za MAUZO ya wachezaji hao ila huwa SIONI WAKIJARIBU KUJUA PESA ZA KUMNUNUA MCHEZAJI ZIMEPATIKANA wAPI!!!
ReplyDelete