Search This Blog

Thursday, March 14, 2013

MUSSA MGOSI: NIPO TAYARI KURUDI SIMBA MSIMU UJAO

MUSSA Mgosi amesema anaweza kurejea Simba kama watampa fedha nzuri msimu ujao  na amedai timu hiyo bado ina nafasi ya kutwaa nafasi moja za juu.
Mgosi ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio msimu wa 2009 alisema kuwa timu yoyote itakayomuhitaji kwenye ligi yuko tayari ili mradi maslahi yawe mazuri.
Mimi nacheza popote, iwe Simba, Oljoro zote sawa tu ili mradi maslahi nitakayotaka yawepo" alisema.
Akizungumzia mwenendo wa Simba kwenye Ligi Kuu Bara, Mgosi alisema bado ina nafasi ya kuchukua nafasi tatu za juu kama watafanya maandalizi mazuri kwa mechi zilizobaki.
"Siwezi kujua maandalizi yao zaidi ya kuisikia tu au kuwaangalia katika baadhi ya mechi, sijui wamejipangaje, lakini mimi naamini kabisa kama watajiandaa katika mechi zilizobaki basi nafasi mbili za juu moja watachukua.
" Ujue hiii ni ligi huwezi kujua ya mbele, unaweza ukawa juu ya mwenzako sasa hivi lakini ukaja kushangaa mwenyewe baadae mambo yamebadilika hivyo Simba bado wana nafasi, watu waache kuwasema sema sana" alisema Mgosi.
Aliongeza:"Simba na Yanga ni timu kubwa ina mashabiki wengi na hakuna shabiki ambaye anapenda timu ipate matokeo mabaya, hivyo yanapotokea matatizo kama haya yanayokumba Simba, mchezaji kama mchezaji anatakiwa afanye kazi yake ipasavyo ili kujiepusha na matatizo hayo, bado naamini wanaweza kutoka mahali walipo na kupanda juu zaidi" alisema Mgosi.

4 comments:

  1. wewe baki uko au uende toto simba utapata namba ya nani?

    ReplyDelete
  2. utakujaaa kutuharibiaaaa vijana we2,bhanaaa we njoo umchukue kaseja mwende huko orjoro simba ye2 m2achie hawa vijanaa wacheze bila miba ya nyie msiotaka kufanya mazoezi,

    ReplyDelete
  3. bora amchukue boban,nyoso,kaseja,maftah waende ASHANTI hapa pamejaa,awezi mweka benchi EDDO au CHANONGO,mgosi ni mzuri sana lakini kwa sasa tunataka vijana wenye njaa ya mafanikio ya soka,simba wabakize watoto B +kapombe+kiemba+cholo+redondo,

    ReplyDelete
  4. Kashazeeka huyo na hatumtaki.

    ReplyDelete