Search This Blog

Tuesday, March 5, 2013

MAN UNITED VS REAL MADRID: VITU VITANO (5) VINAVYOWEZA KUAMUA MECHI LEO

Manchester United wanaikaribisha  Real Madrid leo jumanne katika mechi ambayo inaaminika itakuwa kubwa kuliko zote katika raundi ya 16 bora ya ligi ya mabingwa wa ulaya. 

Real Madrid hivi karibuni wameshinda mara mbili mfululizo dhidi ya mahasimu wao Barcelona, lakini wanasubiriwa na mtihani mwingine mgumu leo pale Old Trafford.

Kikosi cha Sir Alex Ferguson kiliweza kulazimsisha sare ya  1-1 wiki tatu zilizopita kwenye uwanja wa Bernabeu, hivyo Mourinho na Madrid yake leo itakuwa na kazi kushambulia zaidi ili kuweka hai matumaini ya kupita.

Hivyo inamaamisha leo hii kutakuwa na vita kubwa sana katika washambuliaji wa Madrid dhidi ya walinzi wa lango la United. Lakini vita haitokuwa hiyo tu - hivi ni vitu vitano vingine vitakavyoamua nani katika ya magwiji hawa wa soka barani ulaya anaendlea kwenye hatua ya robo fainali.


ANGEL DE MARIA VS MABEKI WA UNITED
Angel Di Maria, muargentina aliye kwenye fomu nzuri sasa hivi, amekuwa akipangwa kwenye kila mechi muhimu wakati Madrid wakitumia mfumo wa kuchezesha washambuliaji watatu. Akiwa anahama kutoka winga moja mpaka nyingine kuhakikisha Madrid inatamba.

Katika mechi ya kwanza wiki tatu zilizopita, Di Maria alitoa krosi safi iliyomfikia Ronaldo na kuwa goli - krosi ikitokea upande wa kushoto ambao ndio Ronaldo anaanzaga kwenye mechi.

Di Maria na Ronaldo wanaweza kuwa upande wowote wa uwanja muda wowote. Ronaldo kwa hakika atatolewa macho zaidi, lakini Di Maria na krosi zake, uharaka na ujuzi wa kupenya yeye mwenye au mipira yake unaweza ukawa hatari kubwa kwa upande wa Man United.

Wapinzani wa Di Maria watakuwa mabeki wa pembeni wa United Evra na Rafael, na ikiwa Di Maria atacheza vizuri sana kwa hakika hali haitokuwa salama langoni mwa Mashetani wekundu. Ni mmoja ya watu wanaoweza kuamua mechi hii.


VIUNGO WA ULINZI WA MADRID VS WASHAMBULIAJI WA UNITED
Kuna taarifa kwamba Ferguson anaweza asimuanzishe Wayne Rooney leo hii, inaweza ikawa kweli au ni mbinu tu za mscotland huyo kuwachanganya Real Madrid.Vyovyote itakavyokuwa leo, tunafahamu kwamba Real Madrid hawapaswi kuruhusu nyavu zao kuguswa usiku wa leo. Kuruhusu goli hasa mapema itamaanisha inabidi wacheze sana na kufunga mabao mawili ili kuweza kupita. Hivyo ushirikiano mzuri wa beki ya madrid utakuwa mchango muhimu sana. Walinzi wa kati na viungo wakabaji wanapaswa kuwa makini zaidi.
 
Mjerumani Sami Khedira mhispania Xabi Alonso mara nyingi huwa wanaanza pamoja na wanatengeneza ushirikiano mzuri sana kama viungo wa ulinzi mbele ya ukuta. Kazi yao na kuwalinda walizni wanne wa nyumana kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji. Pamoja na uwezo wake wa kuzuia, Alonso anatambulika kwa pasi znuri na zenye maana.
 
Khedira na Alonso ni wazuri sana kwenye eneo hilo, lakini United wana washambuliaji hatari. Machaguo kama Robin Van Persie, Rooney, Danny Welbeck na Chicharito.

Wikiendi iliyopita, Shinji Kagawa alifunga hat-trick katika ushindi wa United 4-0 dhidi ya Norwich City. Pia kuna winga wazuri kama vile Nani, Ashley Young na Valencia ambao kama wanakutana safu ya ulinzi isiyokuwa imara wanaweza wakaleta madhara makubwa.


MICHEAL CARRICK VS OZIL
Cristiano Ronaldo, Robin van Persie na wafungaji wengine wanaweza kuwa wanatajwa sana kwenye vyombo vya habari. Japokuwa viungo wanaweza kuwa waamuzi wa hii mechi.

Mjerumani Mesut Ozil usiku zote huwa anacheza kama kiungo mchezashaji wa Real Madrid, akicheza nyuma ya Karim Benzema au Gonzalo Higuain. Au iwe tofauti meneja Jose Mourinho achague kumpanga Kaka  au Luka Modric kuanza, lakini ishara zote leo zinaonyesha Ozil ataanza kwenye mechi leo.

Mpinzani wake mkuu atakuwa kiungo aliye kwenye fomu msimu wa United Micheal Carrick, ambaye hucheza nyuma kidogo ya kiungo cha United huku akicheza part kubwa ushambuliaji wa United.

Ozil inawezekana akawa anaonekana bora zaidi kwenye levo ya kimataifa zaidi ya Carrick, lakini mchango wa muingereza Carrick kwenye timu ya United hasa msimu huu umekuwa muhimu sana. Upinzania baina ya wawili hawa unaweza ukaaamua mechi.


MBINU(FERGIE VS MOURINHO)
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson na wa  Real Madrid Jose Mourinho wamekuwa na upinzani mkali sana tangu Mourinho alipokuwa Chelsea. Sasa hivi japokuwa ni marafiki, lakini wawili hawa hawajaacha upinzani wao, na wote bado wanatajwa kuwa amkocha bora duniani. 

Babu Ferguson aliiwezesha United kupata sare wiki tatu zilizopita. Matokeo ambayo yanamaanisha Real Madrid watacheza mchezo wa kushambulia sana leo Old Trafford. Hilo litafanya kuwepo na ushindani wa mbinu kali za soka baina ya wawli hawa na mabenchi yao ya ufundi.

Pia kutakuwa na vita baina ya wawili hawa kwenye mstari wa uwanja kama ambavyo wote wanajulikana wazuri wa kuhamasisha maamuzi kutoka kwa marefa.
CRISTIANO RONALDO
 BBC Sport, kupitia mwandishi wa kihispania Andy West walitoa makala ya namna ya kumzuia Cristiano Ronaldo yenye maneno zaidi ya 800.
Badhi ya maneno hayo yalikuwa haya:
 "Wanachotakiwa kufanya United ni kuzuia Ronaldo asipige shuti na mguu wake wa kulia, au kushoto, au kuwa wa mwisho kufikia na krosi kwenye eneo la hatari. Wajitahidi kutokutoa faulo karibia na eneo la hatari, au kumuachia nafasi yoyote Ronaldo kuweza kukabiliana na ukuta."
Kama ambavyo inavyoonekana kufanyika kwa haya yote ni vigumu karibia na kutowezekana, ukweli unaweza ukawa unatisha zaidi kwa United. Ronaldo, ambaye aliichezea United kwa kipindi cha miaka 6, amefunga mabao 37 kwenye mashindano yote msimu huu. Anapokuwa kwenye fomu, ni vigumu sana kumzuia kihalali pasipo kucheza madhambi.

Kama alivyoonesha kwenye mechi ya kwanza, Ronaldo ni hatari hewani. Lakini wote tunafahamu moja ya vitu vinavyomtofautisha Ronaldo na wengine yeye ni hatari kwenye eneo lolote la uwanja.

Na kuifanya hali kuwa mbaya zaidi kwa United ni majeruhi ya mlinzi Phil Jones, ambaye hatocheza leo kwa mujibu wa kocha Sir Alex Ferguson.

Kizuizi kikubwa cha ushindi wa United leo kwa hakika ni mtoto wao wenyewe waliowauzia maadui zao kwa £80millioni - Cristiano Ronaldo.T

3 comments:

  1. uchambuzi mzuri.. lakini refa amesahaulika.

    ReplyDelete
  2. wapi kaka shafii 4ril referee kaamua match man utd alikua ashinde hata ukichek replay nani alikua anageuka kucontrol mpira bila kuajua km palikua na m2 pia alikua hana kusudi la kumchezea rafu yule arbeloa by kamrani mtoto wa fisadi kutoka same ila naishi rombo.

    ReplyDelete
  3. Ushindi wa Mourinho hauna utata wowote kabisa yaani Man U kiulaini kabisa wamekubali kichapo, lawama eti kocha kaionea Man U hazina msingi wowote coz kadi nyekundu kwa Nani ni ya halali, Nani kamchezea rafu mwenzake halafu anajifanya yeye ndio kaumizwa ( anamdanganya refa--cheatinga), bora hata angeapology nahic angeonywa 2 kwa yellow card .Tusiegemee kwenye ushabiki tu lazima tukubali ukweli kua Madrid ni wakali na ni wababe wa Man U.N hayo tu-----Makala (korogwe)

    ReplyDelete