KOCHA wa Yanga, Mdachi Ernie Brandts ametamka kuwa mabao mawili aliyofunga Niyonzima katika mechi mbili za ligi kati ya Azam FC na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa ni mazuri na hayana mfano.
"Ni magoli mazuri. Pia, ni muhimu kwetu. Tumevuna pointi sita ambazo zimetuweka kileleni na pointi 42." alisema Brandts.
Kocha huyo alisema; "Nafikiri yamekuja wakati mwafaka tukiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi."
Kwa upande wake, Niyonzima alisema siri kubwa ya staili ya mabao aliyofunga akiwa nje ya eneo la penalti ni mazoezi.
"Mara nyingi nimekuwa nikijifua mazoezini kupiga mashuti na kufunga nikiwa mbali na lango. Nafikiri hiyo ndiyo siri yangu kubwa." alisema Niyonzima ambaye anachezeshwa nafasi ya winga wa kushoto.
Mabao yake na Kavumbagu
KWA taarifa yako ukae ukijua, kati ya mabao tisa ambayo Kavumbagu amefunga, Yanga imenufaika na pointi mbili pekee. Tofauti na mabao mawili aliyofunga Haruna Niyonzima. Yanga imenufaika na pointi sita katika mabao mawili ya Niyonzima aliyofunga katika mchezo wa Azam na Kagera.
Endapo Kavumbagu angegoma kufunga mabao hayo, bado Yanga ingepeta kilele na pointi 40 kibindoni na kuiacha Azam FC nafasi ya pili na pointi zake 36.
Lakini Niyonzima angesusa kufunga mabao hayo, Yanga ingekuwa na pointi 36 sawa na Azam FC.
Kwa akili ya kawaida, itakuwia vigumu sana kuamini. Lakini huo ndio ukweli wa mambo yenyewe.
Huwezi kuamini kwa akili ya haraka. Lakini hiyo ndio hali halisi ya mambo.Kavumbagu amefunga mabao hayo katika mechi nane ambazo Yanga ilishinda zaidi ya bao moja.
Kwa kawaida ushindi wa aina yoyote ile unaipa timu husika pointi tatu. Hali hiyo imefanya mchango wa Kavumbagu kuoneka mdogo tofauti na idadi ya mabao yake aliyofunga.
Ubingwa wa Ligi
KATIKA hali ya kushangaza, nyota huyo amefunguka na kutamka maneno mazito kuwa endapo Yanga itashindwa kunyakua ubingwa wa ligi msimu huu ataondoka zake.
"Kuna malengo ambayo nilijiwekea. Kwa hiyo kama yatashindwa kutimia sina budi kuondoka na kusaka timu nyingine."
Mnyarwanda huyo alisema wakati anajiunga na Yanga alitamka ataisaidia timu hiyo kutwaa taji la ligi na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Naweza kujivunia tumetwaa Kombe la Kagame mwaka jana. Lakini kiu yangu kubwa kwa sasa ni taji la ligi." alisema kiungo huyo.
Hata hivyo, itakuwa vigumu kwa Niyonzima kutimka Yanga endapo itashindwa kutimiza malengo yake kutwaa taji la ligi kutokana na mkataba wake kumalizika mwaka 2015.
Tunawashukuru wote wawili niyonzima na kavuMbagu.namkumbusha kocha aangalie kadi za njano hasije akapanga wachezaji yakatokea kama yale ya kipndi kile tukanyanganywa point na coastal union.shaffi tunashukuru kwa taarifa za sports huku kampala ni kama tuko bongo.naomba uweke ratiba ya ligi kuu kwenye blog yako.francy kampala.
ReplyDeleteKatika mabao yote mawili kushangilia anamkimbilia nirdhan halfan vipi ndo mwana wake saba
ReplyDelete