Search This Blog

Sunday, March 17, 2013

KEI KAMARA: MKIMBIZI KUTOKA SIERRA LEONE MPAKA KUWA STAR WA LIGI KUU YA ENGLAND

Mkimbizi, mwanasoka, mwenye kujitolea kwa jamii, balozi. Unaweza ukamuita majina yote hayo hapo juu Kei Kamara.
Lakini, kuliko kitu kingine chochote utaifa wake unamtambulisha zaidi star mshambuliaji huyu wa Norwich City. 

Kei Kamara alizaliwa nchini Sierra Leone miaka 28 iliyopita.

Kamara aliondoka kwake kutoka na vita vya kiraia, akahamia Marekani, halafu akaanza kucheza kwenye Major League Soccer na sasa yupo Norwich, klabu ya Premier League aliyojiunga nayo kwa mkopo mwezi January.
 
Wakati The Canaries walipomsaini mshambuliaji huyo mpaka mwishoni mwa msimu kutoka Sporting Kansas City, hawakuwa tu wanampata mcheza soka, walikuwa wanamsajili kijana ambaye bado ana makovu na maumivu ya vita vilivyoipasua nchi yake ya Sierra Lione.
Akiwa na umri mdogo sana Kamara alimuona mama yake akiondoka Sierra Leone kwenda US kufanya ili aweze kutuma nyumbani kwa familia yake. Akikulia maeneo ya Kenema, kusini mashariki mwa Sierra Leone, na shangazi, na ndugu zake, alikuwa na miaka 7 wakati vita vilipoanza. 

"Alikuwa darasani na wenzie mara wakaanza kusikia milio ya milipuko na wakaanza kukimbia ovyo," anasema Dave LaMattina, ambaye ameiongoza documentary Kei, ambayo inaelezea story ya Kamara kutoka kuwa mkimbizi wa vita mpaka kuwa nyota wa taifa.

"Anaruka maiti zilizolala barabarani na anawapoteza wadogo zake inabidi arudi kwenda kuwatafuta.
"Tangu siku mabomu yalipoanza kulipuka maeneo karibu na shule alikuwa mkimbizi. Alienda mji mkuu wa nchi hiyo - Freetown, then akaenda Gambia na mwishowe Marekani.
"Masomo yake yaliharibiwa na hivyo akapoteza mwelekeo. Akageukia soka na michezo kwa ujumla - alikuwa mchezaji mzuri sana wa volleyball." 
      
Kama sehemu ya programme ya wakimbizi, alipofikisha miaka 16, aliunganishwa na mama yake huko California, ambapo akarudi tena shule na kujiunga na California State University, Dominguez Hills, na hapo ndipo akaanza safari ya kucheza kwenye Major League Soccer, alianza kwa kujiunga na Columbus Crew, kabla ya kwenda San Jose Earthquakes na Houston Dynamo.
"Kei ni mtu mzuri sana," anakumbuka maneja wa Houston  Dominic Kinnear.
"Anapenda kutania wenzie na angeweza kufanya kitu kutufanya tucheke.

"Lakini pamoja na kupenda masikhara, alikuwa ni mtu makini sana linapokuja suala la kucheza soka. 
"Kuona hatua hii aliyopiga na kufikiria alipotoka kwangu mimi stori kubwa na nzuri inaymhusu mtu aliyepitia shida nyingi na akafaisika kwa kuzungukwa na watu wazuri." 

Kamara amekuwa na mchango mkubwa tangu ajiunge na Norwich City, mechi yake ya kwanza ilikuwa droo 0-0 dhidi ya Southampton na baadae akawa mchezaji wa kwanza kutoka Sierra Leone kufunga goli kwenye Premier League, akitokea benchi kwenye mechi dhidi ya Everton mapema mwezi huu.

Kujituma kwake uwanjani na umakini wake kwenye kazi yake nyuma kuna lengo la kuipa sifa nchi yake Sierra Leone -  kupitia kipaji chake cha soka huku akiendelea kujitoa kwa kujenga shule huko kwao - akijaribu kufuta taswira ya vita vya kiraia vilivyofadhiliwa na almasi za damu na kuipa nchi yake sura nyingine mbele ya macho ya dunia.

"Watu wengi wangekuwa hasira na roho mbaya na wangeachana kabisa na nchi yao baada ya matatizo na shida alizopata wakati akiwa mtoto wa umri mdogo, lakini Kei ni mtu mwenye upendo, mzalendo kwa nchi yake," anasema LaMattina.
"Ni mtu ambaye ameiweka Sierra Leone karibu na moyo wake na mtu ambaye anajaribu kusambaza ujumbe kwamba Sierra Leone sio Sierra Leone ya blood diamonds.
"Ni nchi inayojaribu kuinuka, inayojitibu na majeraha ya vita, lakini ina watu wengi wakarimu kama alivyo Kei." 

Peter Makieu, mwandishi wa habari za michezo huko Sierra Leone, ameshuhudia namna story ya Kamara ilivyoongezwa mwamko na mapenzi ya soka kwa vijana wa nchi yake. 

"Premier League ndio ligi maarufu zaidi nchini Sierra Leone," anasema.
"Watu wamekuwa wakiomba mchezaji japo mmoja wa Sierra Leone acheze kwenye Premier League.
"Unawaona watoto wadogo kwa makundi wakicheza soka kutokea asubuhi mpaka jioni. Kila mwanasoka hapa Sierra Leone anataka kucheza la kulipwa."

Norwich Chris Hughton, anaangalia zaidi uwezo wa dimbani wa  mchezaji wake mpya.
"Kwa miaka mitatu iliyopita nilijua ni mmoja ya wachezaji bora kwenye ligi ya MLS," alisema Kinnear, ambaye alikuwa kocha wa  Kamara kuanzia 2008 na 2009.
"Uhamisho wa kwenda England niliamini ni sahihi kabisa kwake. Ameimarika sana kama mchezaji.
"Kila kitu alichokifanya kwenye MLS ndani ya miaka mitatu iliyopita inamuweka kwenye levo ya wachezaji wa dunia, hivyo sikushangazwa na timu za England kumtaka. Na pia sishangazwi anavyofanya vizuri huko."
LaMattina aliongeza: "Kei anazidi kuimarika. Hakuwa mwanasoka mzuri kule nyumbani kwao, ndugu zake walikuwa wachezaji kumzidi.

"Lakini alipoenda college huko California na akaweza kuwa mmoja ya wachezaji bora kwenye MLS na sasa yupo kwenye Premier League. Anaendelea kuwa bora."
Raia wa Sierra Leone wamekuwa na uwezo wa kumuona mwananchi mwenzao akipambana na akina Rio Ferdinand kupitia majumba ya cinema wakilipa kiasi cha 1,000 Leones (karibia £0.15) ili kuonja utamu wa Premier League na kumuona Kei.

"Kwa kila mechi ya Norwich City majumba ya sinema yanajaa watu wakimuangalia Kei Kamara," alisema Makieu.
"Wamekuwa wakisikitishwa kwasababu mechi nyingi huanzia benchi.
"Alipofunga goli dhidi ya Everton nchi nzima ililipuka kwa shangwe. Sikuweza kujizuia na hisia nilizokuwa nazo.
"Hakuna anayejali kuhusu Norwich. Lakini sasa kila mtu hapa Sierra Leone anataka kuangalia mechi ya Norwich." 
 

No comments:

Post a Comment