Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bia ya Serengeti ya "Tupo pamoja katika shangwe za mafanikio" hii leo |
Ratiba |
Machi 14, 2013, JB BELMONTE,
DAR ES SALAAM: Leo katika hafla iliyohudhuriwana waandishi
wa habari, wageni na wadau mbalimbali Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua
kampeni mpya na ya kipekee inayoenda kwa kauli mbiu ya TUPO PAMOJA. Katika hafla hiyo iliyofana asubuhi ya leo
pia ilihudhuriwa na wadau wa bia hii katika ishara ya kushereheka mafanikio na
shangwe za bia hii.
Akiongea na waandishi wa habari asubuhi la yeo, Mkurugenzi
wa mMasoko wa kampuni ya bia Serengeti Bw. Ephraim Maguru alisema kwamba, “ kwa
miaka kumi saa, tumeona na kushuhudia ukuaji na mafanikio makubwa”. Bia hii inajulikana kwa kampeni ya ‘raha
kamili kwa wengi wanaifahanu kama Chui.
Pia kwa udhamini wa Taifa stars ambao uliinua hadhi ya soka la Tanzania
kwa kiwango kikubwa. Kuna ufadhili wa
Fiesta, ambao wote mnajua mchango Fiesta inatoa katika ukuaji wa tasnia ya
muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
Aliendelea Bw. Mafuru
Bia ya
Serengeti ni bia ya kipekee ambayo ndio bia ya kwanza Tanzania yenye kimea
halisi kwa asilimia mia. Mwaka jana
bia hii pia ilizindua muonekano mpya wa
nembo yake huku ikibaki na ladha ile ile.
Baada ya utafiti, Kampuni ya bia ya Serengeti na wadau wake, wamebaini
kwamba watanzania wanahitaji shangwe za
mafanikio yao katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, kijamii, kimichezo na
kadhalika.
“Tunawakaribisha wote katika hafla mbali mbali
ambazo tutaandaa ili kueneza kampeni hii ya Tupo Pamoja kama mlivyoona katika
matangazo niliyowaonyesha, tutaleta shangwe popote mlipo., Alieleza meneja wa
kinywaji hicho Bw. Allan Chonjo, baada
ya kuonyesha matangazo mbali mbali yatakovyokuwa katika vyombo vya habari.
Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali
wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo wasambazaji wa bia. Kampeni hii inawatambua na kuwathamini watanzania wote kwa mafanikio yao katika sekta mbalimbali za
maendeleo.
Kampuni ya bia ya bia ya Serengeti inajihusisha na biashara ya vinjwaji vyenye vileo kama bia- Premium Serengeti Lager, Tusker
Lager, Tusker Malt Lager, Tusker Lite, Uhuru Peak Lager, Pilsiner, Guinness na vinywaji vikali kama Johnnie Walker, Smirnoff Vodka, Richot, Bond
7 and Gilbeys. Pia vinywaji visivokuwa na kileo kama Malta Guinness
Serengeti Breweries Limited is subsidiary of EABL/ DIAGEO.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Mawasilianao na Mahusiano SBL: Email: evans.mlelwa@serengetibrew.com
Meneja Mawasiliano- SBL imani.lwinga@serengetibrew.com
No comments:
Post a Comment