Kiingilio
cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania
(Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
kijani.
Viti
vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000
viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni
sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897
ni sh. 10,000.
Viingilio
vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni
sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A
yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
Tiketi
kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza
kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo
vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa
wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni na Dar Live Mbagala.
Katika
vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia
yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda
kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika
maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa
fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment