Taarifa za ndani kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ni kwamba kikao cha serikali kupitia wizara ya habari na michezo na shirikisho la soka nchini kuzungumza juu ya suala la serikali kuondoa usajili wa katiba mpya ya TFF kimeishia kwa serikali kuliagiza shirikisho hilo kuwataarifu wanachama juu ya mkutano mkuu ndani ya siku 5 zijazo, na kuandaa mkutano wa kufanya mabadiliko ya katiba katika kipindi cha siku 40 zijazo kutoka leo.
Kwenye kikao hicho TFF iliwakilishwa na Katibu Mkuu Angetile Osiah, mwanasheria Alex Mgongolwa, na Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Sunday Kayuni - taarifa za kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kwamba TFF ilionekana haikufuata taratibu za kufanya marekebisho ya katiba na hivyo serikali ikafikia maamuzi ya kuwaagiza waandae mkutano mkuu wa wanachama wote wa TFF ili kukidhi matakwa ya kufanya marekebisho ya katiba.
Pia baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu, serikali imeagiza uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ufanyike katika kipindi cha siku 40 baada ya mkutano mkuu kufanyika.
Angetile na wenzio haya sasa za mbavu hizo kwepa sasa maana wewe kwa mikwara haujambo
ReplyDeleteKikao kimeombwa na TFF,maagizo mapya yanatoka wapi?labda makubaliano au maazimio
ReplyDeletekwani nini Tenga hakuhudhuria ?
ReplyDeletebwana mwandishi naomba TUJULISHE
Haitoshi! uwajibikaji nao muhimu,sio mtu kufungwa au lah! kulipa gharama zinazotokana na makosa hayo! hilo litaongeza umakini katika siku za usoni!
ReplyDeleteMimi Wallace Karia Mjumbe wa kamati ya utendaji TFF,Napenda kukanusha uwepo wangu kwenye kikao cha waziri na watendaji wa TFF(Secretariat),aliyesema nimehudhuria kikao hicho anaupotosha Umma,mimi kama mjumbe wa kamati maombi ya kukutana na Waziri ilikuwa ahamisi tarehe 7 machi au 13 machi kwa hiyo nisingeweza kuhudhuria,Lakini nadhani kutokana na kauli ya Naibu waziri yaelekea kuna Maagizo ambayo nadhani watendaji(secretatiat ya TFF) watatupatia na tutayafanyia kazi kwa mujibu wa Taratibu,naomba aliyetoa taarifa kuwa nilihudhuria asahihishe na kuniomba radhi kwa upotoshaji mimi ni mtumishi wa umma muda huo wa kikao nilipewa majukumu na mwajiri wangu isije ikaonekana sikutekeleza majukumu ya umma na kushiriki kikao kisichonihusu natoa siku saba ya utekelezaji wa kurebisha kasoro hiyo
ReplyDeleteHaya yote yanatokana na ukweli kwamba Dioniz Malinzi tayari ameshaweka sawa kila kitu kuanzia serikali, wajumbe wa mkutano mkuu wa tff na vyombo vya habari,hivyo hakuna ambacho kina Tenga wanaweza kufanya zaidi ya kuwapisha Jamal Malinzi na kundi lake waingie madarakani TFF,KWANI hata wakisema TFF haina fedha za kuandaa mkutano huo basi Dioniz Malinzi na Cargo Star yake watajitokeza kugharamia mkutano huo na kupenyeza ajenda ya kumng;oa Tenga na kamati yake ya utendaji.Jambo la kujiuliza ni kwa nini hawa watu akina Malinzi wanatumia nguvu kubwa namna hii kutaka uongozi wa TFF hivi sasa?WANA UCHUNGU WA MPIRA KWELI? ni maandalizi ya uchaguzi 2015?na nyinyi vyombo vya habari imekuwaje mpaka mmeitupilia mbali miiko na maadili ya kazi yenu?Serikali kuna maslahi gani kwenye uchaguzi huu hadi muwapangie TFF ajenda za mkutano wao mkuu,kwamba marekebisho ya katiba 2012 yasiingizwe ili kamati ya Mtinginjola isiwepo?soka la tz linaelekea kaburini
ReplyDelete