Search This Blog

Wednesday, March 27, 2013

EXCLUSIVE: KUONDOKA KWA THOMAS MLAMBO NA MAMADOU GAYE SUPER SPORT

Thomas Mlambo wa kwanza kushoto,Mamadou Gaye ni wa pili kutoka kushoto.


Katika siku za hivi karibuni wapenzi wa kipindi cha soccer Africa kinachorushwa kwenye Super Sport wamekuwa wakijiuliza ni wapi walipo wachambuzi mahiri waliokuwa wanaounda timu ya watangazaji wa kipindi hicho Thomas Mlambo na Mamadou Gaye.

Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa Mamadou Gaye na Thomas Mlambo ni kwamba wawili hao kwa sasa sio wafanyakazi tena wa kituo hicho.

Thomas Mlambo ameacha kazi Super Sport na kujiunga na shirika la utangazaji la South Africa (SABC) baada ya kupewa mkataba mnono zaidi na shirika hilo ambalo lipo chini ya serikali ya Afrika Kusini.

Kwa upande wa Mamadou Gaye ambaye mara ya kwanza alisimamishwa baada ya kutoa shutuma nzito kwa baadhi ya vyama vya soka na viongozi wake ndani ya bara la Afrika, hasa kwa shirikisho la Zambia na Raisi wake Kalusha Bwalya.

Akizungumza na mtandao huu Mamadou amesema alisimamishwa na kituo hicho baada ya kutoa shutuma za ukweli kwa Shirikisho la soka la Zambia na Raisi wake Kalusha Bwayla kuhusu kuwa mmoja wa vibaraka wa Issa Hayatou, na kutokana na ushawishi alionao Bwalya kwa kufanya biashara na Super Sport kwa kuwapa dili la kuonyesha ligi kuu ya Zambia, hivyo akasimamishwa. Pindi walipomuita kurudi kazini Mamadou akagoma kwa sababu aliamini alisimamishwa kwa kuifanya vizuri kazi yake.

4 comments:

  1. bado maulid kitenge anashabikia sana upande fulani katika mgogoro wa TFF NA FAMILIA YA MALINZI

    ReplyDelete
  2. nitammis sana tom mlambo i like the guy.and mamadou alikuwa akiongea ukwel yy co mnafiki kazi kwao tk na idah.

    ReplyDelete
  3. Dah,ntawamiss sn majembe yang,mana sasa naona kipnd kmepoza sn.Na nahis walobaki wameambiwa cha kufanya ili yasiwakute ya Mamadou na Mlambo.John Mwakalebela

    ReplyDelete
  4. sio tu kitenge hata shafih dauda naye ana ushabiki sana has kuiponda TFF hata kwa mazuri waliyofanya

    ReplyDelete