Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Watu wa Ivory Coast wameupokeaje ushindi wa Tanzania dhidi ya Morocco ikizingatiwa kuna pengo la pointi moja inayowatenganisha na Taifa Stars kwenye msimamo wa kundi lao?
Mamadou: Ushindi wa Tanzania umetengeneza sana vichwa vya habari vya magazeti. Pia nadhani ushindi huu umeiletea heshima kubwa nchi yenu kwenye soka, ni mafanikio makubwa.
Ni lini ilikuwa mara ya mwisho kwa Ivory Coast kucheza mechi ya mashindano ya ukubwa kama wa mashindano haya bila uwepo wa nahodha aliyeachwa Didier Drogba?
Mamadou: Hii sio mara ya kwanza kwa drogba kutokuwemo kwenye kikosi cha Ivory Coast, nakumbuka hata kwenye mechi za kuwania kufuzu kwenye AFCON 2012 Drogba hakucheza mechi nyingi, pia kwenye AFCON 2013 kuna baadhi ya mechi alianzia benchi. Timu yetu ya Taifa haina upungufu kwenye ushambuliaji, Drogba kwa sasa hana umuhimu mkubwa, na kwa upande wangu nadhani hakustahili hata kuwemo kwenye kikosi kilichoshiriki AFCON 2013.
Hatimaye uchaguzi wa CAF hivi karibuni umemrudisha tena Issa Hayatou madarakani kwa kipindi kingine. Je ni yapi maoni yako kuhusu ushindi wake?
Kamati kuu ya CAF. |
Mamadou: Nadhani hii ni aibu kubwa kwa soka la Afrika, kwa kitendo cha Issa Hayatou kuwarubuni maraisi wa vyama vya soka barani Afrika kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ili kuweza kumuondoa kwenye kugombea nafasi ya uraisi bwana Jacques Anouma.
Hii inanikumbusha miaka ile ya nchi za Afrika kufanya uchaguzi kwa kuchagua mtu mmoja kupitia mfumo wa sera ya chama kimoja. Hili suala linarudisha nyuma maendeleo ya mpira ndani ya bara letu. La kusikitisha zaidi kuhusu wafanya maamuzi wa CAF, ni kwamba Amadou Diakite wa Mali ambaye alifungiwa na FIFA kwa tuhuma za rushwa michezoni anaruhusiwa kuingia kwenye kamati ya utendaji ya CAF ambayo inatoa maamuzi ya kumpitisha Hayatou agombee pekee yake.
Pia Anjorin Musharraf ambaye alifungwa nchini kwake kwa kugundulika kujihusisha na rushwa michezoni pamoja na kula fedha za udhamini, na baada ya kutoka kwa dhamana, Issa Hayatou akamruhusu kuingia kwenye kamati ya utendaji ya CAF. Hili linakupa picha kwamba CAF ni nyumba inayonuka rushwa chafu yenye sumu ambayo imeanza kusambaa kwenye vyama vya soka vya nchi wanachama, ambao baadhi yao wameonekana kuanza kuiga njia ya Hayatou kwa kubadili katiba au sheria za uchaguzi kwa manufaa yao.
Na pindi baadhi ya watu au serikali inapoingilia utaratibu huo mbovu, viongozi wa shirikisho wanakimbilia FIFA kusema vyama vinaingilia na mamalaka nyingine za nchi ili FIFA watishie kuifungia nchi na hatimaye serikali ziogope na viongozi wa mashirikisho waweze kutimiza azma zao.
Kamati kuu yote ya CAF imejaa wala rushwa na viongozi wabinafsi wenye kuangalia maslahi yao binafsi. Hayatou na wenzie wote ni wamoja. Raisi wa sasa wa shirikisho la soka la Tanzania ni mjumbe wa kamati kuu, yeye ni mmoja ya wafuasi wa Hayatou. Kama sio kama anaona upuuzi wote unaofanyika chini ya kamati yao ilibidi awajibike kujitoa kwa kujiudhuru kwenye kamati hiyo, lakini hakuna anayefanya hivyo. Wajumbe wote wa kamati kuu ni wamoja na wanasapoti vyote anavyofanya Issa Hayatou."
Na mwenye masikio na asikie! Ndo maana hata soka la Africa limeshuka sana katika viwango duniani.Uozo dhahiri kabisa lakini wajumbe wote wa CAF eti hawaoni!! Madudu hayo hayo si ajabu ndio yamechangia watu kushikana mashati uchaguzi TFF,ati tuwasubili FIFA waje kutuamulia.kikundi kimejiwekea wigo hakuna mtu mwingine kuingia.Hiyo ni aibu.
ReplyDeleteMara Tenga ni m2 safi,wiz m2pu yeye Karusha nlitegemea wangekuwa mstari wa mbele kupinga ile sheria mpya bt ni waoga na wabinafsi wakubwa wanaogopa vi2mbua vyao kuingia mchanga.Kuna mambo machachi Tenga kajitahid lkn bado pale panapotakiwa maamuzi magum anaogopa kufanya.Niliumia sana pale Hayatou alipoalikwa Kampala kwenye ufunguz wa Kagame Cup.John Mwakalebela DSM
ReplyDeleteHili ndilo soka la Afrika, Sio siri kama mambo haya yanayozungumziwa na Mamadou hayata tazamwa kwa jicho la tatu, hakika soka la Afrika litabaki kitendawili, na si Afrika hata Tanzania pia tusipo liangalia hili soka letu litakuwa ni sawa na HADITHI ZA PAUKWA PAKAWA. "Tuyazingatie haya"
ReplyDeleteHayo ni maoni yake Gaye,siyo lazima yawe ndio maoni ya watu wengine.Kama alitaka kutumia Supesrport kumpigia debe mtu wake awe Rais wa CAF inabidi akubali matokeo.Kuna kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja,uamuzi ukishafanyika unakuwa ni uamuzi wa wote walioshiriki kikao hata kama wapo walioupinga ndani ya kikao.Hii ndiyo nidhamu ya vikao.Kuhusu kujiuzulu Tenga hiyo ni hiyari ya Tenga mwenyewe na sio lazima kama anavyotaka Gaye.Yeye yuko CAF kwa mambo mengi na sio uchaguzi tu.Watanzania lazima tukubali kwamba soka linasimamiwa na FIFA duniani pote kama hutaki unaachana nao na kuunda FIFA yako.Serikali ibakie na wajibu wake wa kisera kuweka mazingira wezeshi ya uendeshaji soka lakini uamuzi wa mwisho wa uendeshaji soka unabaki kwa watu wa soka wenyewe na wakihitaji msaada wa serikali wataomba.
ReplyDeleteGaye alikuwa na mtu wake ambaye alitaka awe Rais wa CAF,baada ya mtu wake kukosa nafasi hiyo ndiyo anaongea yote hayo.Kwako mmiliki wa blog hii hata kama hupendi maoni yangu yasomwe na wasomaji wengine kwa sababu zako binafsi lakini Vyombo hivi vya habari ni vya wananchi/wasomaji,sio vya wamiliki au watangazaji au waandishi au wachambuzi wa soka hivyo ni vema vikatumika kwa maslahi ya wengi lakini bila kukandamiza wengine wasiokuwa na nafasi ya kuvitumia kama alivyofanya Gaye.Kama wajumbe wa kamati ya utendaji CAF walipitisha kanuni fulani na ikakubalika ndio uamuzi wao kwa maslahi ya Caf kwa wakati husika na sio lazima iwe kama anavyofikiri Gaye.
ReplyDeleteNadhani leo comments zilizohitajika hapa kwenye blog hii ni zile za kumuunga mkono Gaye kwa lengo la kuwaponda viongozi wa tff.Hata hivyo kwa bahati nzuri baada ya sakata la katiba ya TFF kumalizika limewafumbua maco wadau wengi kuhusu fitna zilizotaka kufanywa na kambi ya mgombea mmoja anayeungwa mkono na vyombo vya habari na sasa hawako tayari kudanganywa tena
ReplyDeleteNjaa ztawaua viongozi..njaa kali na ndoto za kufanikiwa bila kufanya kazi kwa bidii ndo kinachotuponza..Hayatou anajua wot wana njaa ndo maana anawacontrol anavyotaka.
ReplyDelete