Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji juzi uliwatambulisha rasmi wajumbe wa Bodi ya Baraza la Wadhamiini ambao watafanya kazi zote ambazo zitahusiana na klabu ya Yanga (Mali na Ufilisi) kufuatiwa kupitishwa na wanachama katika mkutano mkuu.
Yanga ilifanya mkutano mkuu mwezi Januari 20, 2013 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi Oysterbay ambao wanachama wa klabu walilridhia kuwaongezea tena mda Mama Karume na Francis Kifukwe amabao awali walikua wamemaliza mda wao wa miaka miwili.
Katika mkutano huo wanachama waliridhia kwa mwenyekiti kuongeza idadi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini kutoka wawili waliokuwepo na kufikia wajumbe saba, ambapo kwa sasa klabu itakua na wajumbe wanne na kamati ya utendaji itapata fursa ya kuongeza wengine watau ili kufikia idadi ya wajumbe saba.
Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, Manji amesema uteuzi huo wa bodi ya wadhamini umezingatia wasifu wa wajumbe hao ambao wamewahi kufanya kazi katika sekta mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Klabu ya Yanga awali ilikua na wajumbe wawili wa Bodi ya wadhamini ambao ni Mama Fatma Karume na Injinia Francis Kifukwe.
Kwa sasa bodi ya wadhamini itakua na wajumbe wa wanne (4) ambao ni Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, na wajumbe wapya waliotambulishwa leo ni Balozi Ami Mpungwe na Kaptain George Mkuchika.
Akitoa wasifu wa wajumbe hao, Manji alisemaBalozi Amir Mpungwe amekua ni kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbali mbali kwa miaka kadhaa, amekua Balozi wa kwanza Tanzania nchini Afrika Kusini mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru na kwa sasa anafanya shughuli zake binafsi.
Kaptain George Mkuchika ni waziri wa nchi ofisi ya waziri utawala bora pia amekua kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbalimbali na hata katika chama chake amekua kiongozi makini kwa muda mrefu.
Aidha kuhusu Mama Fatma Karume na Mzee Kifukwe mwenyekiti amesema wanafahamika kwa kazi zao walizozifnya kwa maendeleo ya klabu ya Yanga hali iliyopelekea mkutano mkuu wa wanachama kuwaongezea muda tena wa miaka miwili.
Mara baada ya kutambulishwa rasmi na kupewa katiba za Yanga mwenyekiti alitumia fursa hiyo kuwazungusha wajumbe kuona majengo na mali za klabu kabla ya kupiga picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment