Watazamaji
12,984 walikata tiketi kushuhudia mechi ya namba 99 ya Ligi Kuu ya
Vodacom iliyochezwa jana (Februari 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 ambapo jumla ya sh. 73,532,000 zilipatikana. Kila klabu ilipata
mgawo wa sh. 17,443,752.45 ambapo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
iliyolipwa ni sh. 11,216,745.76.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,869,704.64,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 5,321,822.78, Kamati ya Ligi
sh. 5,321,822.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,660,911.39 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,069,597.75.
PAMBANO LA YANGA, MTIBWA SUGAR LAINGIZA MIL 125/-
Mechi
namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka
sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 125,181,000.
Watazamaji
22,030 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 30,356,002.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi
sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 3,601,559.61.
Sasa lile swali la timu gani inamashabiki wengi Tanzania limejibiwa.
ReplyDeleteMbona hujasema SIMBA wameingiza ngapi?Habari iko biased!!!!!!!
ReplyDeleteHilo ni kawaida sana Yanga ina wapenzi wengi mzee...
ReplyDelete